Ni kweli hata mimi namwona mama Samia Suluhu Hassan kuwa Kiongozi shupavu na mwenye upendo Mkubwa. Alikwenda hadi Nairobi, Kenya Kumwona na kumpa pole Lissu alipopigwa Risasi tunaambiwa kwa amri ya mtu fulani. Naomba jambo la kwanza awaombe wote waliokimbia nchi warudi na wahakikishiwe usalama, tujenge nchi pamoja. Kisha awaondoe madarakani vibaraka wote walioharibu nchi wakiwemo wafuatao: Kabudi, Chalamila, Kihongosi, yule mkuu wa mkoa wa Mtwara, Kitila, Muro, Sabaya, Mollel, Gwajima, Nchimbi, Ngugai, Tulia n.k. Hawapaswi watu hawa kuwa tena kwenye uongozi wa Tanzania mpya.