Tulizeni Mioyo Watanzania: Taifa liko Salama Mikononi mwa Mama Samia Suluhu Hassan
Vipi muhula mwingine? Daah ule mdomo sahv umeganda tu na barafu
Mungu ibariki tz
Mungu mbariki rais wetu Samia
Mungu ibariki ccm chini ya jemedar wetu Samia hadi 2025 ili tuwagonge tena wale jamaa

R. I. P JPM
 
Mungu ibariki tz
Mungu mbariki rais wetu Samia
Mungu ibariki ccm chini ya jemedar wetu Samia hadi 2025 ili tuwagonge tena wale jamaa

R. I. P JPM
Mi nipo zangu majuu mtajuana wala vumbi huko!!

Daah magufulication ndo basi tena?
 
Kuna puppets wanadhani sasa nchi itasambaratika, wasahau. Uzuri ni kuwa nchi yetu iko imara chini ya Samia. Watanzania wengi sana tupo nyuma yake mh. Rais, kwa maombi na ulinzi. RIP MAGUFULI
Ni ajabu sana unamsikia mtu anasema kuna mtu ananisukuma huku yeye mwenyewe hamuoni na sisi hatumuoni pia. Tunamkubaliaje, kwa mfano. In reality tunatawaliwa na hisia kuliko uhalisia.

Kama unamjua X ni beberu kwa nini usimwambie live kuwa beberu ondoka kwangu badala yake unasemea pembeni tu. Tukitaka kuendelea tusimnyoshee mtu kidole bali tusonge mbele ikiwezekana tumsukumie mbali.
 
Masikini utishwe na nani? Naona bado una hangover ya siasa majitaka ya mwendazake. Usijibanze kwenye kivuli cha watanzania, maana watanzania wenyewe walikuwa hawaamini siasa zenu za propaganda za post colonial, bali walikuwa kimya kuhofia lile kundi lenu la watu wasiojulikana. Kaingia huyu mama hana roho chafu, hata mkimlazimisha kufuata siasa za kiharamia hawezi kupatia moja kwa moja maana haamini katika ushetani wenu...
Madam president ameona kwa macho na si kuambiwa na alivyo tufurahi kwa sababu yapo ya kuumiza ambayo hatayaruhusu.
 
huwa sikai kambi ya wahuni. kambi yangu ni ile ile...ya wazalendo.
Kwani Samia ni kambi gani?
Hata waliokimbia hawakuikimbia nchi bali mtu. Nchi haiponyi bali mtu aweza kuponya majeraha. Watu hutofautiana!
 
Wanabodi mnaweza mkawa mnanielewa vibaya sababu wengi wengi huwa tunapenda kuangalia sarafu upande mmoja.

Miaka mitanon ya hayati Dr Magufuli kuna baadhi ya mambo yalidhibitiwa vizuri hasa suala la upigaji mkubwa kama tuliokuwa tunausikia awamu ya nne ya Jakaya.

Japokuwa tupo tunaomboleza lakini kuna baadihi ya wanaCcm waroho wa madaraka na mafisadi wamefurahi sana. Maana wao kukwapua mali ya umma ni sehemu ya maisha yao.Na alipokuwepo JPM aliwadhibiti. Sasa ameondoka mtasikia mambo ya ajabu. Mtasikia kandarasi kama Escrow zinaibuka na mpaka tunakuja kishituka watu wameshakwapua mabilioni ya shilingi.

Mbali ya hayo tutarajie watendaji na wateule wa rais kufanya kazi kwa uzembe wa hali ya juu. Maana watanzania wengi hawajui wajibu wao mpaka wasukumwe kwa vitisho vya tumbua mtumbua.

Kwa ufupi tunaenda kurudi nyuma sana na huo ndio ukweli.
Haya ni maono ama utashi wa fikra zako?
 
Habari wadau!

Tangu mama kula kiapo cha kuiongoza nchi wengi tumeonyesha kuwa na imani kubwa na mama kama mama kutupeleka kwenye nchi ya ahadi bwana Mussa kashakufa ,tegemeo letu ni kwa mama yeye ndio Joshua wetu wa kutupeleka kwenye nchi ya asali na maziwa .

Ila sasa hata siku haijaisha kuna vidudu mtu vishaanza kuvuruga hali ya hewa ,kiukweli nchi ina rais mmoja tu naye ni Mama mh. Samia Suluhu Hassan haipaswi kumpangia pangia style ipi ya kuongoza au amteue nani au avunje au asivunje baraza hilo ni jukumu lake na chama chake cha Mapinduzi.

Ni ujinga kiwango cha GPA mtu wa Chadema kutoa maelekezo mtandaoni na kushauri nn cha kufanya mwacheni mama arelax afanye achape kazi na ss sote tumuunge mkono .

Mnapoteza maana halisi ya upinzani wa kweli sio kukosoa kila jambo,maana najua kuna mijitu imeshajipanga kwenye kukosoa kosoa tu hata haioni aibu .
 
Kwenye line bado wengineo wengi tena kwa mfululizo...
#Respect Science
#Covid_19_Denialism_Is_Lethal
 
Pumzika kwa amani ndugu na mfia Nchi Joseph Pombe Magufuli.

Kama nilivyosema,ni hakika yangu isiyo na shaka kwamba vyombo vya Ulinzi na Usalama kamwe havitakubali Nchi yetu kurejeshwa kwa wapiga dili.

Mheshimiwa Rais wa sasa anawajibika kwa hakika kuendeleza na ikibidi aongeze mbio kwa yale yeye ataona inafaa ayafanye kwa mustakabali mwema kwa Nchi yetu.

Lililo kuu sote na kwa umoja wetu hasa wapenda matokeo chanya inatubidi tumemwombee mheshimiwa Rais Samia ili asije kengeuka!
 
JWTZ pekee ndio wamebakia imara na ubaya ni kuwa wameapa kumtii amiri jeshi mkuu(kikatiba)

TISS ina makundi now day
1.TISS asilia(CCM)
2.TISS JPM
3.TISS wafia nchi
4.TISS wafichua siri
 
Wapiga dili walibadilika tu,haijawahi kutoka huko
 
Vyombo vya usalama mwisho wao ni kumtii Amiri jeshi mkuu yakiwemo maamuzi yake.

Kama Amiri jeshi ataingiliwa kichwani na wasaidizi wake vyombo vya ulinzi na usalama havitakuwa na lakufanya.
 
Back
Top Bottom