Uchaguzi 2020 Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) yamtangaza Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa awamu ya pili

Uchaguzi 2020 Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) yamtangaza Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa awamu ya pili

Yaani manamba yote yale waliyokuwa wanampa wakitangaza matokeo ya kura za urais majimboni jumla yake ndio milioni kumi na mbili tu.

NEC wameona aibu wamepunguza idadi ya kura za wizi, mabegi mengine watakuwa wameyatupa hawajayahesabu.

Inaonekana waliokua wanachapisha hizo karatasi walikua wanatoa offer za buy 5 get 1 free.
 
HONGERA Dr John Pombe Joseph Magufuli kwa akichaguliwa tena, kwa kura nyingi, kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Pale unapoandaa tafrija halafu wewe ndio Mc..kamati ya chakula..mapambo na vyote vihusuvyo function hiyo[emoji3]
 
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imemtangaza Dkt. John Magufuli, aliyekuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM kuwa mshindi wa Uchaguzi uliofanyika Oktoba 28. Pia imemtangaza Mama Samia Suluhu Hassan kuwa Makamu wa Rais Mteule.

Dkt. Magufuli ameshinda kwa kupata kura 12,516,252 akifuatiwa na aliyekuwa mgombea wa Urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu ambaye amepata kura 1,933,271.

Dkt. Magufuli ambaye pia ni Rais wa Tanzania amepata ridhaa ya kuongoza kwa muhula wa pili kama Marais waliotangulia.

Tume imesema walikuwa na jumla ya watu 29,754,699 waliojiandikisha kupiga kura, na waliopiga kura walikuwa 15,091,950. Kura halali zilikuwa 14,830,195 huku kura 261,755 zikiwa zimeharibika.

Kwi Kwi Kwi
 
Mkuu, unasema kweli? Ndo chadema wajue kuwa huyo siyo mwenzao.
Taarifa zinasema hivyo! Kwani leo umemuona popote hapa TZ? Inasemekana alioneka tarehe 29/10/2020 Namanga kumbuka pia ile tiketi yake ilikuwa ya tarehe 29/10/2020. Kesho kwenye mkutano wao tutajua kama yupo.
 
Back
Top Bottom