Uchaguzi 2020 Tume ya Uchaguzi yampitisha Tundu Lissu kuwania Urais kupitia CHADEMA


Tarehe 25 Agosti 2020
Dodoma, Tanzania

Urais, Fomu kuhakikiwa na Kutangazwa Kuteuliwa , kisha kusubiria kama kuna pingamizi

Baada ya fomu kuhakikiwa na kutangazwa kuteuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa kila kitu kipo sawa kuna zoezi muhimu la kubandika majina ili umma kuwafahamu.


Muda wa pingamizi ni kuanzi saa 10:00 jioni ya tarehe 25 Agosti 2020 hadi saa 10:00 jioni siku inayofuata yaani tarehe 26 Agosti 2020.

Zoezi hilo muhimu ni hatua inayofuata ni kusikia kama wagombea wamewekewa pingamizi na wale wadau wanaotambulika na Tume ya Uchaguzi, kisha wagombea wateuliwa kupata nafasi ya kujibu.

Wenye haki ya kuweka pingamizi ngazi ya Urais na Makamu ni hawa wadau watatu yaani Mkurugenzi wa Uchaguzi, Msajili wa Vyama Vya Siasa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Pingamizi ngazi ya Urais linatakiwa kuletwa kwa maandishi katika fomu namba 9A na pingamizi hilo liwakilishwe ndani ya muda muafaka unaoanzia muda uliotajwa hapo juu na sababu za pingamizi litajwe.

Hivyo waliotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ngazi ya Urais kama wateule baada ya kuhakiki fomu na nyaraka wote wanaweza kuwekewa pingamizi muda wowote kuanzia muda wa saa 10:00 jioni ya leo tarehe 25 Agosti 2020 na mwisho wa kuwakilisha pingamizi ni kesho saa 10:00 jioni tarehe 26 Agosti 2020.
 
Huyo Magufuli hiyo tume si ni yake na dunia nzima inafahamu hilo, sasa watu wewe ndio umewaajiri unategemea nini.

The NEC is comprised of the ccm puppets and the whole world knows this.
 
Siasa siyo uadui..... Tukutane October 28!
 
Hongera Rais wa wanyonge...Mungu akutangulie ..

Sasa wakati wa kutoka hao wahuni wasiojulikana wanaweza kumteka ili asiweze kujibu mapingamizi yake!! Pia wanaweza kumdhuru hata kwa sumu ya kupuliza!!

Hawana maana hao.
 
Mkuu inatakiwa uangalifu sana namna ya kuishi hapo Dodoma kwa Mh Lissu kwa masaa ya leo
 
wangemkata wangekiona cha mtema kuni kutoka kwa Bob Amsterdam!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…