Uchaguzi 2020 Tume ya Uchaguzi yampitisha Tundu Lissu kuwania Urais kupitia CHADEMA

Uchaguzi 2020 Tume ya Uchaguzi yampitisha Tundu Lissu kuwania Urais kupitia CHADEMA

..Duh!!

..wewe kweli una usongo.
Ndio ukweli wenyewe huo mkuu. Kama unabisha tutakuwekea na hati zake za kusafiria kwenda USA etc. Hatuwezi kukubali kibaraka awe kwenye sanduku la kura. Moto ni moto na uwake tu.
 
Muache kulialia sasa, ili mnyoshwe bila kisingizio.

Maana ilikuwa kila siku nyuzi kwamba tume imeamuriwa isimpitishe kugombea uRais.

Na msisahau kumpa uRais wa Ufipa baada ya uchaguzi.
Watampa uraisi wa twita mkuu, maana wa JMT hatumpi ng'oo!
 
Ndio ukweli wenyewe huo mkuu. Kama unabisha tutakuwekea na hati zake za kusafiria kwenda USA etc. Hatuwezi kukubali kibaraka awe kwenye sanduku la kura. Moto ni moto na uwake tu.

..hati siyo tatizo.

..umesahau Thabo Mbeki alikuwa na pasi ya kusafiria ya Tanzania?

..hata kama aliandikishwa ukimbizi, kitendo cha kurudi Tanzania kinamuondolea haki zake za ukimbizi.
 
Hapa Dodoma ndiyo kama hivi mida huu saa moja na dakika 28. Bado wingu ni nzito wakuu.
20200825_192811.jpg
 
Mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA wakili msomi Tundu Lissuameteuliwa na Tume kuwa mgombea urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Safari ya Ikulu kwa Tundu Lissu inaendelea kuiva-Goodluck Haule on twitter.

Wadau,hio taarifa sio ya kweli,mpaka muda huu bado wako katika ofisi za Tume wakisubiri hatima ya uteuzi huo.

Bado tupo ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi mpaka muda huu, sasa hivi wamemaliza kuhakiki orodha ya wadhamini now Mhe. Tundu Lissi ndo ameingia kwa Mkurugenzi wa Tume kwa ajili ya Uteu-Hilda Newton(25 minutes ago on twitter).

Hawa hapa katika picha wakiwa bado wanasubiri:

1598373694714.png
 
Mbona kama vile Lissu amekuwa mpole sana nilitarajia sasa hivi vitisho makamanda waende NEC, Amsterdam atoe tamko na mengineo.

Mwisho wa siku binafsi namuombea wampitishe ila apunguze ujuaji alikuwa na nafasi tangia tarehe 22 kupeleka form kama kuna lolote akabadili kabla ya kurudisha, wakati Membe anatumia fursa hiyo pengine CDM walikuwa wanamuona pimbi.
 
Nahisi hatopitishwa, giza limeanza kutanda na Tanesco wanataka kukata umeme maeneo ya Dodoma kwa ajili ya kerekebisha hitilafu.

Na TCRA wanasema wanataka kufanya marekebisho ya tower zao Dodoma.
 
Back
Top Bottom