Tumeshakaa mwezi hatuongeleshani. Nianzishe mahusiano mapya au bado mapema?

Tumeshakaa mwezi hatuongeleshani. Nianzishe mahusiano mapya au bado mapema?

Umejuaje kua yeye hajui anataka nini?

Huyo kisha kutema jiongeze,halafu wewe unaonekana ni mtu usiyejiamini na huna msimamo,ndio maana amekudharau kiasi hicho,

Alishakusoma toka kitambo sana,na sasa amefikia maamuzi tayari.
Hajui anachotaka Gentleman huwa anaongea na sio kununua.. mwanaume kununanuna ni tabia za wanawake

Anyway nimeshajiongeza ndio maana sijamshobokea mwezi mzima
 
Habari za usiku

Mimi napitia changamoto ya kimahusiano. Tumenyamaziana na mwanaume niliyekuwa na mahusiano hii ni week ya 4.

Kusema ukweli sina kosa lolote nililolifanya ila ni yeye ndio alikuwa na vitu alipaswa kuniambia (siwezi kuviweka hapa maana mhusika anaweza kuwa humu)

Nilijipa siku 3 za kujipendekeza kumtafuta kila siku ni mimi naanza nilivyomaliza hizo siku 3 nikauchuna; huwezi amini na yeye akakaa kimya ni ku-view status na ku-like. Hakuna kuongeleshana

Sihitaji kumtafuta.. na kama hatonitafuta nitafanya maisha yangu

Sasa nauliza; tumeshakaa mwezi hatuongeleshani - je naweza kuanzisha mahusiano mapya au bado mapema?
Aisee, jitahidi kujali niliyokueleza...

Rekebisha
 
Kuna mdada mwingine kwenye confession page alisema aliachana na wanaume wa 3 tofauti, hawakugombana, ila tu ni ile silent treatment, mtu anajiona akimtafuta mwenzake atakuwa anajishusha, mwishowe uhusiano unakufa.

Mahusiano mengine mengi ya sasa, hamna anayetaka kuonekana mnyonge kwenye mahusiano, mnaweza mkawa wote moyoni mnapendana, ila kuonesha upendo ndo kipengele, mwishowe mahusiano yanakufa, mnabaki single.

Watu wengi wanataka kuoneshwa upendo, ila wao kuonesha upendo ni kipengele
Two avoidants can never sustain a rlship
Na ndio wengi wako dating market
Mana kila leo wanaanza moja na wataachana hadi Yesu anarudi
 
Mimi sipo kwenye hilo kundi.. mimi huwa namtafuta bila kujiuliza ni mara ngapi amefanya hivo

Tatizo lilianza yeye aliposhindwa kunipa maelezo yoyote kuhusiana na issue iliotokea akapotezea jambo kama halijatokea

Nikampa muda labda ataongea akaa kimya then namtafuta anakuwa kama hataki kuongea mara ya mwisho alisema Ngoja nakucheck mpk Leo ni mwezi nangoja kucheckiwa
Tafuta jamaa mwingine wa backup
Huyo kama unampenda usiage wala nini mtaja endelea siku akianza kuongea
 
Two avoidants can never sustain a rlship
Na ndio wengi wako dating market
Mana kila leo wanaanza moja na wataachana hadi Yesu anarudi
Saa ingine hakuna cha kuwa avoidant, unajua kwenye dating market watu wengi hawapati machaguo yao wanaoyataka, kama ni wadada wanatongozwa na wanaume wasiowataka, vivyo hivyo wanaume wanapata tu wale wadada ambao hawajawapenda, hivyo mtu anaona kuliko akae single ni heri ajishikize tu huku akiangalia kwingine, hivyo anaona hana haja ya kuwekeza kwenye huo uhusiano KateMiddleton
 
Back
Top Bottom