Tuna hatari zaidi kwa Vyombo vya Habari kuliko wakati mwingine...

Kinacho itesa tasnia ya habari Tanzania ni haki ya matangazo,Na ikumbukwe kuwa matangazo ndo chanzo kikuu cha mapato kwenye vyombo vya habari na mtangazaji mkuu ni serikali.Hii imepelekea ukasuku na sycophancy reporting.

Pia Kuna mgongano wa kimaslahi,itikadi na taaluma.Wamiliki wengi wa vyombo vya habari ni wafuasi wa vyama vya siasa,hivyo habari yoyote ambayo ni kinyume na itikadi ni ngumu kupata airtime kwenye air room au space kwenye magazeti na hii imeleta changamoto nyingi kwenye taaluma ya uandishi wa habari.

Kulingana na utafiti uliofanywa na Twaweza,MISA-TAN,Jamii Forum na TAMWA asilimia 50% ya waandishi wa habari hukumbana na vitisho,ukatili na unyanyasaji wa kijinsia nchini.
Wametekwa na posho pekee
 
SI wahadhiri, si wanafunzi, wote ni wafu wanaotembea.
Sikajiona chuo chenye elites wa kuongea ama kukosoa jambo lenye manufaa kwa nchi. Ni chawa na waganga njaa wakubwa!
Hakuna intellectuals wa kukosoa vitu; wamebakia legends kama kina Ulimwengu, Prof. Shivji, na wachache wao. Walioko vyuoni sasa hivi hawawezi kuthubutu.
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Kuna kitu hakiko sawa. Inapotokea kuwa watawala wanashukuru, wanasifia, wanaunga mkono na wanaonekana kuwa wametulia na kuenjoy uhusiano wao na vyombo vya habari ni lazima tushtuke kidogo. Kwenye nchi zote zenye demokrasia ya kweli na zinazojaribu kujenga au zinazojenga utawala wa sheria mgongano kati ya vyombo vya habari na watawala ni matokeo ya lazima.

Inapotokea vyombo vya habari (vile vya zamani na hivi vya mitandaoni) vinajaribu kuwasiliana na watawala na kupeleka habari zake ili zihakikiwe basi tuna tatizo. Kama habari ikiandikwa halafu mtu anasema "itoeni hiyo habari" na chombo cha habari kwa kuogopa kuudhi au kwa kuhofiwa kuudhiwa kinakubali basi tatizo linazidi kukua.

Kuna watu wanaamini kabisa kuwa si lazima kuwe na ugomvi kati ya vyombo vya habari na serikali. Nakumbuka wakati wa mtawala fulani vyombo vya habari vilisifika sana kwa kupokea "bahasha". Matokeo yake nakumbuka mchorani vikatuni wa Kenya Bw. Gado alichora picha ikionesha vyombo vya habari vikimlamba miguu mtawala wa wakati ule. Inawezekana tumerudi pale tena?

Lakini cha kutisha zaidi ni kuwa kama watu ambao hata hawako serikalini na si watawala labda wana utajiri wa kutupa tu nao wanaweza kuamua nini chombo cha habari kinafanya au kinasema basi kile kinachoitwa "uhuru wa vyombo vya habari" si kingine bali ni kugeuka kuwa "kunguru wa habari". Wanaruka ruka, kula, na kupiga kelele, za hapa na pale, huku wakidonyoa donyoa kile wanachopewa. Hawatakiwi kuudhi watu au kumuudhi mtu.

Tunajuaje kuwa tuna uhuru wa vyombo vya habari; watu wengine wanasema sasa hivi vyombo vya habari na waandishi hawafokewi, hawapigwa, hawatekwi, hawaumizwi, wamekaa kwa starehe wanafikiri kuwa hili ni jambo zuri. Ni zuri kwa nani? Ni lazima uwepo mgongano kati ya vyombo vya habari na watawala.

Jukumu la vyombo vya habari si kuunga mkono serikali au kuipa maneno mazuri. Kile ambacho watu walisema kinatokea wakati wa JPM ndiyo hicho hicho kinatokea tena wakati huu wa SSH. Ukiangalia utaona kuwa ni shilingi ile ile ila upande mwingine tu. Sikuwahi kuwa na tatizo hata kidogo na watu au waandishi waliokua wanaikosoa na kumkosoa Magufuli.

Kuna watu wanafikiri tulimuunga mkono Magufuli halafu tukaegesha akili zetu pembeni wenyewe tukaondoka. Niliandika mada hapa ya kumtaka Rais Magufuli Ajiuzulu kama aliona kazi ya Urais ni ngumu (nina uhakika kuna watu hawakumbuki wanafikiri tulikuwa tunaimba sifa tu!). MADA HII HAPA BONYEZA HAPA.

Na mada hiyo nakumbuka ilipigiwa chapo na mkongwe MAYALA kwenye mada yake hii NYINGINE BONYEZA HAPA.
Ni lazima tuwe na uhuru wa kusema kisichopendeza, kuonesha kisichotakiwa, na kukataa kinachopendwa na wengine. Inapofika vitendo vya kifisadi vinahaririwa kwanza basi kile kinachoitwa uhuru wa vyombo vya habari hakipo tena. Ngoja tuone ili tufanye maamuzi saa hii. Nimeweka tena mada ya mwelekeo mpya wa ufisadi Tanzania uliorudi kwa nguvu.

UsiDOWNLOAD hii attachment; na ukidownload usiseme kilichomo.
Kwakutumia akili mnembo nimegundua kumbe tunakaribia kufanya uchaguzi hivyo kuna umuhimu kuwaasa waandishi wa habari kabla ya shari
 
Ukiona serikali inaungana na vyombo vya habari ujue hata sisi wachangiaji hatupo safe.

Jambo la msingi ni kuendelea na mazungumzo kuhusu umuhimu wa uhuru wa vyombo vya habari na kuchukua hatua za kulinda na kuimarisha.

Kwa kufanya kazi pamoja, tunaweza kuhakikisha kuwa vyombo vya habari vinaweza kutekeleza jukumu lao muhimu katika jamii yenye demokrasia.
yaani, sasa hivi nawaogopea kweli watu wanaoposti kwenye mitandao "rasmi"... enzi zile hatukuwa rasmi. Mtu ukitajwa unahusika na JF unaangaliwa mara mbilimbili... nakumbuka watu walikuwa wakiingia ofisini wanacheki JF lakini kwa kunyemelea...
 
Ulikuwa ukiwakosoa pia waliomkosoa (yaani mkiwa vitani halafu askari mwenzio anaelekeza silaha upande wako unaogopa), labda hapo ndipo wadau walipoona kwamba na wewe ulikuwa wa "mhimili uliojichimbia chini zaidi."
Hapana; sijawahi kumkosoa mtu aliyekuwa anamkosoa Magufuli labda tafuta mfano unioneshe ambapo nilimuambia mtu asimkosoe au anakosea kumkosoa Magufuli. Ntakaa nasubiri. Ni muumini wa uhuru wa maoni per excellence; hasa maoni yasiyopendwa.
 
Mkuu si uje na wewe uanzishe chombo chako kitakachokuwa kinapishana na Serikali. Kwani unafeli wapi?

Yaani mtu ametoa mtaji wake kama Family ya Reginald Mengi kujenga empire ya vyombo vya habari. Anatengeneza ajira kwa maelfu na kulipa kodi, wewe unataka aandike habari za kufurahisha wanaharakati!!
Kuwa mzalendo bas mbona mnajizimaga data hivyo?kwa hyo vyombo viwe tu na kazi ya kusifu na kuabudu!!dawa yenu ipo na inachemka ipo siku yenu yaja
 
Hapana; sijawahi kumkosoa mtu aliyekuwa anamkosoa Magufuli labda tafuta mfano unioneshe ambapo nilimuambia mtu asimkosoe au anakosea kumkosoa Magufuli. Ntakaa nasubiri. Ni muumini wa uhuru wa maoni per excellence; hasa maoni yasiyopendwa.
Mwanzoni ulikuwa ukiunga mkono ukosoaji wa serikali na ulikuwa ukiwatia moyo Chadema. Hata ulikuwa ukichapisha makala kwenye Gazeti la Tanzania Daima, ulipoanza kuunga juhudi, ukaanza hata kuwa against Chadema. Nikipata nafasi nzuri ya kupata baadhi ya michango yako ya wakati huo katika context hii nitaileta.
 
Sahivi ni aibu tupu, habari zote zinafanana kwenye TV ndiyo ujue tatizo linaanzia hapo
Imekuwa kama baadhi ya mainstream media za nchi za magharibi wakati Fulani.

1718776076320.png
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Kuna kitu hakiko sawa. Inapotokea kuwa watawala wanashukuru, wanasifia, wanaunga mkono na wanaonekana kuwa wametulia na kuenjoy uhusiano wao na vyombo vya habari ni lazima tushtuke kidogo. Kwenye nchi zote zenye demokrasia ya kweli na zinazojaribu kujenga au zinazojenga utawala wa sheria mgongano kati ya vyombo vya habari na watawala ni matokeo ya lazima.

Inapotokea vyombo vya habari (vile vya zamani na hivi vya mitandaoni) vinajaribu kuwasiliana na watawala na kupeleka habari zake ili zihakikiwe basi tuna tatizo. Kama habari ikiandikwa halafu mtu anasema "itoeni hiyo habari" na chombo cha habari kwa kuogopa kuudhi au kwa kuhofiwa kuudhiwa kinakubali basi tatizo linazidi kukua.

Kuna watu wanaamini kabisa kuwa si lazima kuwe na ugomvi kati ya vyombo vya habari na serikali. Nakumbuka wakati wa mtawala fulani vyombo vya habari vilisifika sana kwa kupokea "bahasha". Matokeo yake nakumbuka mchorani vikatuni wa Kenya Bw. Gado alichora picha ikionesha vyombo vya habari vikimlamba miguu mtawala wa wakati ule. Inawezekana tumerudi pale tena?

Lakini cha kutisha zaidi ni kuwa kama watu ambao hata hawako serikalini na si watawala labda wana utajiri wa kutupa tu nao wanaweza kuamua nini chombo cha habari kinafanya au kinasema basi kile kinachoitwa "uhuru wa vyombo vya habari" si kingine bali ni kugeuka kuwa "kunguru wa habari". Wanaruka ruka, kula, na kupiga kelele, za hapa na pale, huku wakidonyoa donyoa kile wanachopewa. Hawatakiwi kuudhi watu au kumuudhi mtu.

Tunajuaje kuwa tuna uhuru wa vyombo vya habari; watu wengine wanasema sasa hivi vyombo vya habari na waandishi hawafokewi, hawapigwa, hawatekwi, hawaumizwi, wamekaa kwa starehe wanafikiri kuwa hili ni jambo zuri. Ni zuri kwa nani? Ni lazima uwepo mgongano kati ya vyombo vya habari na watawala.

Jukumu la vyombo vya habari si kuunga mkono serikali au kuipa maneno mazuri. Kile ambacho watu walisema kinatokea wakati wa JPM ndiyo hicho hicho kinatokea tena wakati huu wa SSH. Ukiangalia utaona kuwa ni shilingi ile ile ila upande mwingine tu. Sikuwahi kuwa na tatizo hata kidogo na watu au waandishi waliokua wanaikosoa na kumkosoa Magufuli.

Kuna watu wanafikiri tulimuunga mkono Magufuli halafu tukaegesha akili zetu pembeni wenyewe tukaondoka. Niliandika mada hapa ya kumtaka Rais Magufuli Ajiuzulu kama aliona kazi ya Urais ni ngumu (nina uhakika kuna watu hawakumbuki wanafikiri tulikuwa tunaimba sifa tu!). MADA HII HAPA BONYEZA HAPA.

Na mada hiyo nakumbuka ilipigiwa chapo na mkongwe MAYALA kwenye mada yake hii NYINGINE BONYEZA HAPA.
Ni lazima tuwe na uhuru wa kusema kisichopendeza, kuonesha kisichotakiwa, na kukataa kinachopendwa na wengine. Inapofika vitendo vya kifisadi vinahaririwa kwanza basi kile kinachoitwa uhuru wa vyombo vya habari hakipo tena. Ngoja tuone ili tufanye maamuzi saa hii. Nimeweka tena mada ya mwelekeo mpya wa ufisadi Tanzania uliorudi kwa nguvu.

UsiDOWNLOAD hii attachment; na ukidownload usiseme kilichomo.
mtu kama balile ukimwangalia na ongea yake kwa sasa utagundua kabisa hakuna kitu serikali tayari imenunua ubongo wako hasa SSH,yeye ni kwenye msafara wa mama kula bata tu
 
Magroup ya vyuo vingi yanaweka kabisa masharti kuwa ni marufuku ku-discuss siasa. Na hamna group maalum Kwa siasa,na uki-discuss wenzako wanakuona wa ajabu sana nawenye ujasiri wa kipekee Ilihali utakuta mtu kaongea kitu Cha kawaida kabisa na hapo hapo utasikia unamwanasheria kaka?,kaka Kunawatu wanaku-zoom tu humu.Siasa itakusaidia nini wewe?

Kwahiyo lazima uwe muoga tu kujihusisha kivyovyote vile na habari za kisiasa.(Huo ni kwaupande wa vyuoni)
Ni tofauti sana na miaka ya 2000. Kipindi kile watu hasa vijana walikuwa wanapenda mijadala. Ukisikia kuna kongamano watu wanajaa. Kwa kumbukumbu zangu ilikuwa mkutano wowote vijana watajaa na wanataka kuuliza maswali. Ila leo vijana hawafikirishi fikra zaidi wataulizia kuna chakula? Posho? Ama utasikia ntapata nini?
Leo ukisikia kuna kongamano wanaojaa ni watu wenye muktadha wa vyama vya kujamii au siasa ambayo of course Wana malipo. Kuna shida sana
 
Kinacho itesa tasnia ya habari Tanzania ni haki ya matangazo,Na ikumbukwe kuwa matangazo ndo chanzo kikuu cha mapato kwenye vyombo vya habari na mtangazaji mkuu ni serikali.Hii imepelekea ukasuku na sycophancy reporting.

Pia Kuna mgongano wa kimaslahi,itikadi na taaluma.Wamiliki wengi wa vyombo vya habari ni wafuasi wa vyama vya siasa,hivyo habari yoyote ambayo ni kinyume na itikadi ni ngumu kupata airtime kwenye air room au space kwenye magazeti na hii imeleta changamoto nyingi kwenye taaluma ya uandishi wa habari.

Kulingana na utafiti uliofanywa na Twaweza,MISA-TAN,Jamii Forum na TAMWA asilimia 50% ya waandishi wa habari hukumbana na vitisho,ukatili na unyanyasaji wa kijinsia nchini.
Naunga mkono
 
Back
Top Bottom