Uchaguzi 2020 Tundu Lissu aahidi neema kwa Madaktari, Walimu na Vyombo vya Dola

Hizi ndio zile sera za kuahidi kuweka mabomba ya maziwa nchi nzima.

Utatoa wapi fedha za kulipa watumishi double the salary,

Labda tuamue tuache Kila kitu ili tuwe tunalipa watu mishahara tu.
 
Hizi ahadi kama za Mzee Hashimu Rungwe!
 

nani alikwambia mshahara ukiongezwa watu wanatumbukia kwenye umasikini mkuu ? emu tuletee hapa mifano ya nchi mbili tu ambazo watumishi waliongezewa mshahara nchi ikawa masikini alafu mimi nitaleta mifano sita ya nchi ambazo mishahara iliongezwa watu wakaishi vizuri.
kwa akili ya kawaida kabisa mshahara wa mtumishi ukiongezwa utaongeza pia na purchasing power ya huyo mtumishi ambapo akinunua bidhaa au akifanya shughuli za maendeleo kama kujenga atasaidia kipato kipatikane kwa familia za watu wengine pia na hata akitumia mshahara wake kwenye ulevi itasaidia ma bar maid nao kuishi vizuri.
 
Hizi ahadi kama za Mzee Hashimu Rungwe!
Hii inanikumbusha zile ahadi zaidi ya 60 za bw. Kikwete.
 
Ni jamaa aliyeelimika kisheria na kuongeza umbumbumbu kwenye mengine yooote!
 
Kamanda mwambie atueleze vyanzo vya mapato vya kulipa mishahara dabo hahahaha
Kuwaongoza nyumbu ni jambo rahisi sana hahahahha
Yaonekana Lissu hajui hata wage bill ya serikali ni kiasi gani!
 
Hizi ndio zile sera za kuahidi kuweka mabomba ya maziwa nchi nzima.

Utatoa wapi fedha za kulipa watumishi double the salary,

Labda tuamue tuache Kila kitu ili tuwe tunalipa watu mishahara tu.
Kadri pesa nyingi inapoingia mtaa inasisimua uwekezaji,hatimae mapato pia yanaongezeka
 

you have a lot to learn,
 
na ana wafuasi wa kutosha
Angalia na ubora wa wafuasi, Boss! Na mikoa watokayo. Baadaye utajua malengo ya wafuasi. Kumbuka pia kusoma taarifa ya NBS ili ufahamu demography ya nchi hii ili ujue uwezekano wa kupata kura ngapi. Huo ndo usomi na uelewa.
 
Kwani posho na mishahara minono ya wabunge inatoka wapi?

Hivi Lumumba misukule itaisha lini?
Badala ya kuelezea mipango yake kwamba hiyo pesa ataipata kutoka vyanzo vipi vya mapato, anaongelea kutumia!
Na nyinyi mnashangilia!
Kweli kuongoza chadema ni raha
 
Wewe hujui kitu, wachezaji tu wa ligi mbalimbali huko ulaya wanalipwa kwa wiki
 


kutopandisha mshahara haimaanishi utaendelea kuishi poor, its also a strategy akili zako zkiwa zpo vizuri inakua ni opportunity kwako! kuhusu uwekezaji just shut the hell up , ni vile tu haijakamilika ila chunga huo mdomo
 
Hakika Tundu Lissu ana lengo zuri la kuwavusha watumishi, kutoka kukata tamaa ya maisha mpaka kuwa na furaha na utumishi wao.
Watanzania Oktoba iko mbioni tusifanye makosa tena, maana usomaji namba za muhula wa pili utakuwa maradufu
 
Asisahau na swala la wahitimu kusotea nyumbani huyu jamaa wa chato alianza kwa mbwembwe sana kuwaondoa wa vyeti feki lakini mpaka sasa vijana Hawaoni tumaini
Wa vyeti feki walirejeshwa kazini kimya kimya kwa siri kukwepa Aibu baada ya wengi kuvipigia kelele vyeti vya Paul Makonda
 
kutopandisha mshahara haimaanishi utaendelea kuishi poor, its also a strategy akili zako zkiwa zpo vizuri inakua ni opportunity kwako! kuhusu uwekezaji just shut the hell up , ni vile tu haijakamilika ila chunga huo mdomo
Kutopandisha mishahara hupelekea watumishi wa umma kubuni mbinu za ufisadi kuomba omba Rushwa kutengeneza mazingira ya vipato vya ziada
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…