Pre GE2025 Tundu Lissu: Abdul alikuja nyumbani kwangu kunihonga akiwa na kiongozi wa CHADEMA

Pre GE2025 Tundu Lissu: Abdul alikuja nyumbani kwangu kunihonga akiwa na kiongozi wa CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA - Bara, Tundu Lissu akizungumza katika Mtandao wa Club House amesema kuna Kiongozi wa CHADEMA ambaye ameshanunuliwa kwa Fedha za Kuhongwa na mtu aliiyemtaja kwa jina la Abdul, alikwenda nyumbani kwake kwa lengo la kumhonga fedha ili aondoke CHADEMA na kujiunga CCM.

“Abdul aliletwa nyumbani kwangu kunihonga akiwa na kiongozi wa CHADEMA wakiwa na list ndefu ya waliokwishahongwa tayari”

Huyo jamaa anayetajwa na Lissu kuhonga watu huko CDM ana cheo gani huko Ccm au serikalini ?....

Hii rushwa Takukuru hawajapata habari zake?
 
Huyo jamaa anayetajwa na Lissu kuhonga watu huko CDM ana cheo gani huko Ccm au serikalini ?....

Hii rushwa Takukuru hawajapata habari zake?
Takukuru siyo wakurupukaji,issue haina ushahidi utaipeleka vp huko Mahakamani!? Wengine humu wanataka eti Abdul ndiyo atowe ushahidi wakati shutuma za rushwa kazitoa Lissu, mtoa shutuma ndiyo anawajibu wa kutoa ushahid wake,na siyo kutulisha maneno matupu tu kama ya kwenye kanga!!
 
Abdul anatoa wapi hizo hela?Huyu Abdul lazima amwambie mama yake abadili katiba ili kuondoa ukomo. Mama yake awe Rais mpaka siku anakufa.
 
Shida kila sehemu kumechafukwa.
Shida sana ndiyo maana mpaka wenyeviti wa mitaa wanauza maneno ya watu wenye hati miliki
Serekali inashindwa kutatua kwasababu ndiyo sera za Nchi iliyopararazi kimaadili

Mfano mdogo Dodoma kuna mgogoro wa Ndachi
Kweli inaingia akilini
Kama SI kubariki tabia chafu
 
Siyo kuchafua ni kweli Ezekia Wenje alimpeleka Abdul Tageta nyumbani kwa Lissu kumchombeza ahamie CCM, hivi unafikiri Lissu ni mjinga hakurecord mazungumzo yao? Nyie subirini kila kitu kitawekwa hadharani. Wenje baada ya kuona Lissu amechomoa kuchukua hela chafu ndiyo ametangaza kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti ili kumng'oa Lissu.
Mbona hakuyasema hayo kabla mpaka Wenje alipotangaza kuwania
Nafasi ya makamu mwenyekiti?
 
Sasa nimetambua kitu.
Kumbe anaetaka kuua chadema ni ccm ili mama apite kiurahisi.
Kama ndivyo why lisu aanze chokochoko dhidi ya chadema badala ya ku blast ccm.
Kumbe basi rushwa iko zaidi ccm na sii chadema.
Lisu angetulia kichwa na kuendelea kuunga mkono chama chake wangefika mbali ila kwa sasa aondoke ili chadema ipone
Aondoke ili awaachie chama waliopokea rushwa kukiua?
 
Mbona hakuyasema hayo kabla mpaka Wenje alipotangaza kuwania
Nafasi ya makamu mwenyekiti?
Alishasema zaidi ya mwezi mmoja nyuma, japo hakumtaja moja kwa moja Wenje kuwa ndiye alimpeleka Abdul nyumbani kwake Tegeta. Haya mambo ni mazito sana CCM imedhamiria kuiua kabisa Chadema .
 
Kichefuchefu kimeshaingia Chadema !
Sasa ni mwendo wa kutapika tu 🙄
Ngoja tuone mwisho wake !

Lakini kama hii ni kweli then tuendako siko kabisa !

Yajayo yanasikitisha ! Money speaks ?????!!!!! 😳😱😱😱😳
Wanasiasa aina ya Lissu ni kwenda nao kwa tahadhari .
Kanikumbisha hadithi za high school kwamba " Abduly" kamwambia nimeshatoka na Dem huyu na huyu etc . .. na yeye akaamini... Bila ushahidi na yeye anakuja nazo hadharani....

Chama ni chake na yeye ni boss... Kimeshindikana nini huko ndani anakosa busara akijua madhara yake anakuja kuropoka hadharani?
Atoke CDM alafu aende CCM ambapo anamtukana na Mwenyekit wake?
Kwamba ACT kuna nafuu? Au labda NCCR?
Ni wapi hakuna rushwa? Ni nani msafi?
Michango ya Kila siku anayopewa akiwa kwenye nafasi ya uongozi haiwezi kutafsiriwa kama indirect corruption?
Nchi yetu rushwa ni sehem ya karibu Kila kitu... Naming and cursing and pointing fingers ni sehem tu ya siasa za maji taka...
Alivyopigwa risas za mvua anafaham pesa iliyomuhudumia ilitoka wapi?

Leo anamsifia Msigwa kwenda CCM ambapo kwa maisha yake yote ya siasa wamekuwa wakimtarget yeye personally na kum bully hata baada ya kupata majeraha yaliyotaka kumtoa uhai...

He may be right ila busara ni kitu muhim sana.

Akigombea urais na bahati akapata atakuwa anapambana na Kila kitu na Kila mtu? Nchi itatawalika?

Lissu anaonekana mtu smart ila anaanza kuwathibitishia watesi wake kwamba yeye sio presidential material kama walivyokuwa Wana msema ....

Ni bahati mbaya kwamba anajiunga na wanaharakati uchwara kupambana dhidi ya chama chake....

Wana harakati Wana mbio lakini hawafiki mbali ... Ajiulize NCCR ya wanaharakati ilipoishia....

Lissu Fanya siasa, Wacha harakati.
 
Alishasema zaidi ya mwezi mmoja nyuma, japo hakumtaja moja kwa moja Wenje kuwa ndiye alimpeleka Abdul nyumbani kwake Tegeta. Haya mambo ni mazito sana CCM imedhamiria kuiua kabisa Chadema .
Vipi karipoti takukuru na kwenye mamlaka ya chama chake?
 
Wanasiasa aina ya Lissu ni kwenda nao kwa tahadhari .
Kanikumbisha hadithi za high school kwamba " Abduly" kamwambia nimeshatoka na Dem huyu na huyu etc . .. na yeye akaamini... Bila ushahidi na yeye anakuja nazo hadharani....

Chama ni chake na yeye ni boss... Kimeshindikana nini huko ndani anakosa busara akijua madhara yake anakuja kuropoka hadharani?
Atoke CDM alafu aende CCM ambapo anamtukana na Mwenyekit wake?
Kwamba ACT kuna nafuu? Au labda NCCR?
Ni wapi hakuna rushwa? Ni nani msafi?
Michango ya Kila siku anayopewa akiwa kwenye nafasi ya uongozi haiwezi kutafsiriwa kama indirect corruption?
Nchi yetu rushwa ni sehem ya karibu Kila kitu... Naming and cursing and pointing fingers ni sehem tu ya siasa za maji taka...
Alivyopigwa risas za mvua anafaham pesa iliyomuhudumia ilitoka wapi?

Leo anamsifia Msigwa kwenda CCM ambapo kwa maisha yake yote ya siasa wamekuwa wakimtarget yeye personally na kum bully hata baada ya kupata majeraha yaliyotaka kumtoa uhai...

He may be right ila busara ni kitu muhim sana.

Akigombea urais na bahati akapata atakuwa anapambana na Kila kitu na Kila mtu? Nchi itatawalika?

Lissu anaonekana mtu smart ila anaanza kuwathibitishia watesi wake kwamba yeye sio presidential material kama walivyokuwa Wana msema ....

Ni bahati mbaya kwamba anajiunga na wanaharakati uchwara kupambana dhidi ya chama chake....

Wana harakati Wana mbio lakini hawafiki mbali ... Ajiulize NCCR ya wanaharakati ilipoishia....

Lissu Fanya siasa, Wacha harakati.
Kwa hiyo unamshauri naye apokee halafu apige kimya?
 
Siyo "viongozi wenzake" tena.Bought and taken for good!
Una ushahidi wa hili mkuu?
Lissu anasema na yeye kaambiwa...

Nyerere aliwah kusema, ukiambiwa Mimi ni baba yako utaamini?

Nafikiri kuna mengine zaid ya hili.
 
Back
Top Bottom