Tundu Lissu adai Hayati Magufuli ndiye aliyeagiza shambulio la kupigwa risasi dhidi yake Dodoma

Tundu Lissu adai Hayati Magufuli ndiye aliyeagiza shambulio la kupigwa risasi dhidi yake Dodoma

Kwa mtazamo wangu nibora familia ya jpm na familia ya lissu wakae chini wayamalize kuliko kila siku kumsema jpm kuhusu taribio hili la mauaji.

Na kwahili familia nzima ya jpm inapata lawaza zote!
 
Kwenye mahojiano na kipindi cha Clouds 360 Lissu amesema aliyetoa mari, masaa mawili kabla hajapigwa risasi alisema kulikua na mtu anahutubia na kwenye hotuba yake alikuwa anapokea ripoti ya Bunge ya madini ya Almasi na Tanzanite, moja ya mambo aliyoyasema kwenye hotuba hiyo ni;

"Wale wanaopinga nchi wakati tupo kwenye vita ya kiuchumi nyie wanajeshi mnajua huwa wanafanywaje, hawastahili kuishi."

Ambapo masaa mawili baadae Lissu alishambuliwa Dodoma, akisema bayana kuwa anayemuongelea ni Hayati John Pombe Magufuli, ambapo hata baada ya tukio hilo Rais Magufuli hakuwahi kusema chochote juu ya shambulio hilo.

View attachment 2504783


Hakuna mtu makini atampinga Lissu kwenye hili maana ni ukweli mtupu. Watabadilisha mada tu hapa
 
Labda nikukumbushe

Jaji mkuu anateuliwa na Rais wa JMT

Spika wa Bunge anapendekezwa na CC ya CCM ambayo Rais wa JMT ndiye Mwenyekiti wake na vikao vyake hufanyikia Ikulu

CDF anateuliwa na Rais wa JMT

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi anateuliwa na Rais wa JMT

Msajili wa Vyama vya Siasa anateuliwa na Rais

Kwa kifupi Katiba ndio inampa Udikteta Rais

Usidanganywe na chochote kwa Tanzania Rais ndio Nchi yenyewe!
Kwa hiyo unakubaliana nami kuwa Magufuli aliposema anayeenda kinyume na nchi auawe, alimaanisha anayeenda kinyume na yeye Magufuli, auwe.
 
Huyu nae amezidi kujiona so special kwani yy ni nani!!???
kwani yy angekuwa wa kwanza kuuwawa!!??
Kenya yenyewe enzi za Moi miaka ya 1992 walimng'oa Robert Auko baada ya kuona anaenenda ndivyo sivyo.
Kenya hiyo hiyo 1969 Jomo Kenyatta through its inner circle walimuua Tom Mboya baada ya kubaini alikuwa ni CIA na msaliti
So hizi issue ni za kawaida popote pale duniani pindi unapoekwenda tofauti na maslahi ya serekali ya wakati huo (government of the day) nimeweka mifano ya jirani yetu Kenya ila mifano ipo kibao (so issue ya Lissu haistui)
Taifa lolote duniani ukiwa msaliti wanakung'oa hakuna ajabu hapo.
Mwambieni hii Kiki yake tumeichoka aje na mipango madhubuti ya kukuza uchumi sio blah blah za kizembe
Jichagulie jina mwenyewe linalomaanisha nguruwe mla mavi. Maana kwenye list ya binadam umeamua kujitoa
 
Kwa hiyo unakubaliana nami kuwa Magufuli aliposema anayeenda kinyume na nchi auawe, alimaanisha anayeenda kinyume na yeye Magufuli, auwe.
Hiyo iko duniani kote

Wanakijiji wa Njololo walimshuhudia Mwangosi

Wapemba walihamia Shimoni Kenya nk....nk

Udikteta wa kikatiba ni ule ule tofauti ni mbinu zinazotumika tu

Kama unabisha subiri uone kama Covid 19 hawatafika 2025
 
Mungu anawapenda sana wenye dhambi ili waifikilie toba!

Maana hata wewe unaibilisi wako na ndiyo maana unadhambi unazozificha machoni pa watu lakini kwa Mungu huna uwezo wa kuzificha
Mungu ni mwenye huruma, mwingi wa rehema na msamaha kwao wanaotubu, na siyo wanaonea fahari uovu wao. Mungu hutoa msamaha kwa yeyote anayemlilia, lakini Mungu hafungamanishwi na shetani. Mungu huonesha ukuu wake kwao wamliliao na huwapa ushindi wale wanamlilia na kumtegemea kwa wakati ufaao.

Mimi sina ibilisi wangu. Ibilisi au shetani ni mmoja tu kwa watu wote, japo ana mawakala wake hapa Duniani. Wanadamu, kuna wakati tunaanguka katika dhambi lakini haimaanishi kuwa kwa kuanguka katika dhambi, basi tumekuwa sehemu ya utawala wa shetani. Lakini wapo ambao ni wa utawala wa shetani, hawa humtegemea shetani kwa kila jambo. Hujasikia kuwa wapo baadhi ya watu, kabla ya kugombea madaraka wanaenda kwa mganga wa kienyeji? Hujasikia wapo ambao kabla hajalima au hajaanza ajira anaenda kwa mganga wa kienyeji? Hawa ndio wa utawala wa shetani, maisha yao wameyaegemeza kwa shetani. Kwao ushindi na mafanikio yao, yapo kwa shetani. Mimi siyo mtakatifu, lakini maisha yangu nimeyaegemeza kwa Mungu wa kweli aishiye katika nafsi tatu.
 
Huyo Tundu Lissu, ninachomsifu huwa haogopi kutamka lolote!

Kama ni nyeupe atasema ni nyeupe. Full Stop
Kwa hiyo lisu alikuwa msaliti?

Kama ni hivyo basi ilikuwa sahihi kwake kuuliwa
 
Ulikuwepo nchini wakati wa utawala wa dikteta Magufuli?

Yeye ndiye alikuwa nchi. Yeye ndiye alikuwa katiba. Yeye alikuwa bunge, yeye alikuwa mahakama.

Kwa hiyo kumpinga yeye ilikuwa unapinga nchi. Lisu alikuwa anampinga dikteta Magufuli kuzuia exports za concentrates bila ya kufuata sheria.
Lisu anajichanganya sana
 
Muuaji alipelekewa moto toka Mbinguni. Lisu ambaye alitakiwa kufa kwa maelekezo ya dikteta, akashuhudia msiba wa aliyetaka kumwua.

Lisu, daima simama katika haki, tembea katika haki, uishi katika haki. Maana ni kwa kupitia wewe, ukuu wa Mungu uliweza kudhihirika hata mbele ya maibilisi.

Mungu wetu, tunakuomba daima ulilinde Taifa letu na watu wake. Mashetani hata wakija, wasiweke makao katika Taifa hili, bali uwaondoshe kwa kadiri ya hekima yako Bwana. Tunaomba faraja kwaajili ya familia ya Ben Sanane, Aziry, Kanguye na wote walioondoshwa katika Ulimwengu huu kwa agizo la mtawala dhalimu.
Vipi wale walitupa bomu na kuua watu 5 pale kwenye mkutano wa chadema soweto arusha wao watapelekewa moto lini?

Vipi wale waliomtesa Ulimboka?

Vipi waliomsambaratisha mwangosi kwa bomu?

Vipi mungu wako anawapelekea moto ccm lini ili mjikomboe?
 
Angeweza kushtakiwa kwa vitendo vyake kama Magufuli na siyo Rais. Kuna avenue ya kumshtaki
Mbona Jk aliua watu watano kwa bomu kwenye mkutano wa chadema kule soweto arusha na yupo?

Mwangosi je?

Ulimboka?

Au lisu yeye ni nani?

Takataka kabisa
 
Kwa hiyo lisu alikuwa msaliti?

Kama ni hivyo basi ilikuwa sahihi kwake kuuliwa

..alitakiwa afikishwe MAHAKAMANI.

..Magufuli na serikali wangetoa tuhuma na ushahidi wake na Lissu angejitetea.

..baada ya hapo mahakama ndio ilipaswa kutoa hukumu stahiki.

..kama Mbowe alishtakiwa kwa ugaidi, Bibi Titi Mohammed alishtakiwa kwa uhaini, Thomas Zangira alishtakiwa kwa espionage, nini kiliwazuia kumpeleka Lissu mahakamani?
 
..alitakiwa afikishwe MAHAKAMANI.

..Magufuli na serikali wangetoa tuhuma na ushahidi wake na Lissu angejitetea.

..baada ya hapo mahakama ndio ilipaswa kutoa hukumu stahiki.

..kama Mbowe alishtakiwa kwa ugaidi, Bibi Titi Mohammed alishtakiwa kwa uhaini, Thomas Zangira alishtakiwa kwa espionage, nini kiliwazuia kumpeleka Lissu mahakamani?
Adhabu ya kusaliti nchi ni nini?

Yani kupoteza muda mahakamani?
 
Back
Top Bottom