Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ahusisha kauli ya Rais Magufuli na kupigwa kwake risasi

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ahusisha kauli ya Rais Magufuli na kupigwa kwake risasi

Swali langu kwa Tundu Lisu, je yeye ndio alikuwa anawasiliana na hao mabeberu kuwapa taarifa nyeti alizoiba toka selikalini na kuisaliti nchi..?

Kama jibu ni ndio, kama kweli alikuwa anafanya hivyo basi hastaili kuishi kabisa.
Hakuna mwenye haki yakukatisha uhai wa mwenzake mtalipia mtalipa
 
Je Lisu ndio aliekuwa analisaliti taifa kwa mujibu wa hayo maelezo hapo juu?
Wewe huujui aina ya utawala tulionao? Kwa utawala wa sasa, ukiwa msema ukweli, ukawa mkosoaji wa Rais au Serikali, wewe ni msaliti, wewe unatumiwa na mabeberu, wewe siyo mzalendo. Lakini anayepoteza 1.5 tr ni mzalendo. Anayegawa nyumba za umma kwa ndugu, marafiki na wapenzi, ni mzalendo. Anayetenda kwa kuvunja katiba ni mzalendo!! Huo ndio unafiki mkubwa.

Asili ya shetani ni muongo. Lakini kamwe shetani hayashindi mamlaka ya Mungu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Soma vitabu vya Dini vizuri, Mwenyezi Mungu anaadhibu pia, ...

Kasome kuhusu Huria Mhiti katika msahafu wa Kikristu. Mmoja wa makomandoo 30 mahiri na watiifu kwa Mfalme Daudi, Huria mhiti. Alishindwa kuelewa, kutafsiti na kutii amri halali ya mfalme Daudi ili afiche aibu ya mfalme. Aliamriwa aende akalale nyumbani kwake ambapo mke wake alipewa ujauzito na mfalme Daudi Huria akiwa mstari wa mbele vitani.

Huria akafikiri kwenda kulala nyumbani kwake maana yake ni lazima ulale na mkeo. Na ilikuwa mwiko kwa wayahudi kushiriki tendo la ndoa wewe ukiwa askari mstari wa mbele wakati wa vita. Ilikuwa ni kulinajisi jeshi lote. Huria akakaidi amri ya Mfalme akalala getini na walinzi wa jumba la mfalme. Matokeo yake lengo la kwanza la mfalme kuficha aibu yake halikufanikiwa. Ikabidi mfalme atumie njia mbadala ambayo iligharimu maisha ya wanajeshi wengi mno na kikosi cha jeshi la Isreli kilichokuwa mstari wa mbele kikapata kichapo cha mbwa koko na Huria alikuwa mmoja wapo walio uwawa siku hiyo

Ndiposa tunasema mamlaka hizi zinazo tawala watu zimewekwa na Mungu. Daudi aliadhibiwa na Mungu mwenyewe kadiri alivyoona inafaa Daudi akatubu na matokea yake mwanae mwingine Daudi aliyempata na mke wa huyu mhanga yaani mama Huria akawa ni Mfalme Suleinani mtu ambaye alikuwa ni mwenye hikma haijawahi kutokea duniani na hatatokea. Na Bwana Yesu akawa ni mzao wa Daudi.

Hivyo to some of us wala hizo kelele za Lissu ambazo anapayuka hovyoo bila ya kutafuta hekima ya Mungu ni kazi bure na uharibifu mtupu kwake. Yeye angalimuliza Mungu wake kwa nini umenipitisha njia hii? Kuliko kuendelea kupayuka payuka bila utaratibu akifikiri atapa huruma kwa wanadamu. Huruma ya kweli unaipata kwa Mungu mwenyewe mh, Wala si hii unayoitaka ya kimaslahi zaidi labda eti utakuwa rais.

Mimi nitamuambia sababu ninazo ziona ambazo zote zimejengwa katika msingi wa tamaa zake zakujipatia kipato bila ya kujali ana kipata vipi. Wamedanganya watu wakaingia kupambana na vyombo vya dola na baadhi yao wakapoteza maisha na wengine wakawa vilema. Makaninikia usaliti wake ni ili apate fedha. Hivyo hivyo ukodishaji wa cdm kwa EL.
 
Je Lisi alikuwa anasaliti taifa kama maelezo yake alivyosema
Wewe huujui aina ya utawala tulionao? Kwa utawala wa sasa, ukiwa msema ukweli, ukawa mkosoaji wa Rais au Serikali, wewe ni msaliti, wewe unatumiwa na mabeberu, wewe siyo mzalendo. Lakini anayepoteza 1.5 tr ni mzalendo. Anayegawa nyumba za umma kwa ndugu, marafiki na wapenzi, ni mzalendo. Anayetenda kwa kuvunja katiba ni mzalendo!! Huo ndio unafiki mkubwa.

Asili ya shetani ni muongo. Lakini kamwe shetani hayashindi mamlaka ya Mungu.
 
Sijaelewa, kwahiyo anaomba kuchaguliwa sababu alipigwa risasi? Yeye ni wakwanza kupigwa risasi? Tumeshuhudia hadi askari wakipigwa risasi sembuse yeye? Atupe sera ataifanyia nn TZ sio blah blah.
 
Tatizo taratibu zipo lakini hutaki kuzirejea, matibabu ya nje ya nchi yana taratibu zake mbona hapo unakwepa kueleza? Kama unajiamulia kuondoka nchini kwenda kutibiwa nje ya nchi bila kufuata taratibu, gharamikia matibabu mwenyewe usitafute watu wa kulaumu kwa kulazimisha utaratibu usiokuwepo
Nataka kudhani kwamba wewe hujawahi kuumwa. Katika terms za kibinadamu kusema hayo unayosema ni kutojua maana halisi ya kuokoa maisha. Hivi huko kwenu hamna dharura? Katika kuokoa maisha ya mtu aliyekuwa taabani kiwango kile angefuata taratibu zipi? Tatizo letu hata Mambo serious tunayafanya siasa.

Utaratibu wowote ambao hauwezi kupindwa linapokuja suala la kuokoa maisha ya mtu Ni utaratibu usiofaaa. La maana pale ilikuwa ni kusaidia mtu mgonjwa taabani na siyo kusisitiza utaratibu ambao hata ungekuwa wewe usingeufuata. Nasisitiza utu, utu, utu Kwanza.
 
Na sio huyo aliye mtaja tuu, hata Ndugai anahusika na mpango mzima wa tukio lile. Hii mabadiliko ya katiba ya juzi ya kinga kuzuia kushtakiwa mpaka spika wa bunge ni muendelezo wa kujiwekea kivuli...

Kwa hiyo kamanda una maanisha Tundu Lissu ndio alikuwa ana wasiliana na amabeberu kutuhujumu na kutusaliti?
 
Soma hata vitabu vya dini wasaliti walikuwa wanafanywaje?
Hakuna kitabu chochote cha dini kinachoidhinisha, nje ya mahakama, raia mmoja kumuhukumu raia mwingine kuuawa
 
E
IMG_20200821_081317_998.jpg
Tundu Lisu kaadhibiwa na Mungu, some punishment is just, na bado, ...
Tundu Lisu kaadhibiwa na Mungu, some punishment is just, na bado, ...
We kept it for the record hiyo sura yako na roho yako unaificha wapi
 
Mumekosa LA kusema hadi MNA kufuru. Mungu yupi huyo anayetumia risasi kwa binadamu aliye muumba kwa mfano wake?
Mashetani ni hatari sana kuishi nao!

Mkuu kwa hiyo unasema Lissu amekiri kuwa ni yeye ndio alikuwa anatusaliti? Ni yeye ndio alikuwa ana tuhujumu kwa kuiba taarifa? Kumbe ni yeye Lissu msaliti?
 
Back
Top Bottom