Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ahusisha kauli ya Rais Magufuli na kupigwa kwake risasi

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ahusisha kauli ya Rais Magufuli na kupigwa kwake risasi

View attachment 1543623
Mgombea Urais wa Chadema katika uchaguzi mkuu ujao mwishoni mwa mwaka huu, ametoa madai mazito mjini Njombe jana katika ziara zake za kutafuta wadhamini, akimuhususisha Rais, kuhusu jaribio la kuuawa kwake, lililofanyika September 7 mwaka 2017.

Akihutubia umati wa wananchi, alikumbushia historia ya tukio lake la kumiminiwa risasi, ambapo aliponea chupuchupu kuuawa na kukimbizwa nchi za nje kwa matibabu.

Akisimulia mkasa huo alieleza kuwa kuna "connection" kati ya hotuba aliyoitoa Rais Magufuli, ya uzinduzi wa ripoti ya tume ya madini, masaa takribani mawili, kabla ya kupigwa kwake risasi, aliyotoa akiwa Ikulu, jijini Dar-es-Salaam.

Aliendelea kueleza kuwa katika hotuba hiyo aliyotoa Rais Magufuli, ambayo alidai ipo ndani ya YouTube, alimnukuu Rais akiyatamka maneno yafuatayo "Katika mapambano ya kijeshi, huwa wana kawaida ya kumwua, askari yeyote ambaye anawasiliti katika mapambano yao, vile vile katika vita ya kiuchumi ambayo nchi yetu inapigana hivi sasa, hatuwezi kuruhusu ku-survive kwa mtu mmoja, ambaye imebainika amekuwa akiwasiliana mwanasheria wa kampuni hiyo ya madini, Deo Mwanyika, ili kumwibia taarifa mbalimbali nyeti, katika lengo lao wakishirikana na mabeberu kutoka nje ya nchi, katika kutuhujumu malipo yetu ya madini, hastahili kabisa ku-survive" mwisho wa kunukuu.

Tunajua kuwa katika tukio hilo la kupigwa kwake risasi mwaka 2017, Tundu Lissu, Jeshi la Polsi limekuwa likutaaminisha kuwa uchunguzi wa tukio hilo unakwamishwa na Tundu Lissu, muhanga mkubwa wa tukio hilo, pamoja na Dereva wake, ambao wote walikuwa wameenda nchi za nje kwa matibabu.

Hivi sasa Tundu Lissu amesharudi nchini na amewapa "hints" ya kilichompata siku ile ya kutisha sana, ambapo "watu wasiojulikana" walimpiga risasi mfululizo 16 mwlini mwake katika jaribio la kutaka kumwua na ameeleza mwenyewe nini kilimtokea siku ile, ambapo Jeshi letu la Polisi, limekuwa likidai kuwa limekwamishwa kuendelea na uchunguzi wake, kutokana na kukosekana ushahidi huo wa Tundu Lissu

Kwa hiyo nadhani Jeshi la Polisi lingeanza kufanyia uchunguzi wa tukio lile sasa, kwa "hints" alizozitoa yeye mwenyewe muathirika wa tukio lile Tundu Lissu.
msaliti mkubwa huyo hafai hata kwenye shimo
 
Dereva je? Anarudi lini maana yule ndo alishuhudia kila kitu.

Tunataka atuambie zile risasi alizopigwa lissu katika mguu wa kulia upande aliokua amekaa yeye zilimkosaje zikampata Lissu.
Hili swali fikirish! Kama Lissu ana majibu atupatie kwa niaba.
 
Tulia wewe. Hii kesi haijafa, watu wana akili zao timamu. Wanasubiria muda muafaka tu.

Hata Lissu alikua ana uwezo wa kwenda kufungua mashitaka ya shambulio dhidi yake. Jiulize why hajafanya hivyo, badala yake kakimbilia kuchukua fomu ya urais. Haya mambo ni mazito, mtakuja kubaki midomo wazi.

Tutakuja kubaki midomo wazi kwa kuwa bado mnatafuta pa kushikilia ila hampapati.

Kila mkijaribu hoja mfu na tuhuma za uongo zinakuwa hazina mashiko. Ni ukweli tu ndiyo utawaweka huru, katika hili AMINI NAKUAMBIA.
 
Kuua msaliti wa nchi ni sawa tu na polisi kuua jambazi
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

Mbona mnajificha kwenye kivuli cha wasiojulikana na kusema TL hana ushahidi kumbe mashahidi mko huku kwenye keyboard semeni kama mnavyotoa taarifa za kuuwa jambazi kama mnauhakika kuwa ni msaliti kuendelea kujificha ni dhahiri kuwa mnafahamu kuwa usaliti mnatumia kama kisingizio tu. Mara upepelezi unamsubiri Lissu amerudi kimyaa
 
Watu wa Sodoma na Gomola walijiumba!? Kama unawajua watu hao utakuwa umenielewa.
Nadhani najadili hili na mtoto mdogo au MTU mzima asiye jielewa.
Mungu anaadhibu wakosaji lakini haadhibu kwa usiri kutumia watu wasiojulikana.
Anaogopa nini mpaka afanye kwa usiri mkubwa? Ukitaka kumhusisha Mungu jambo lolote kaa chini utafakari kwanza ukuu wake na sio kuropoka tuu
 
Lisu kama alikuwa anafanya hivyo alistahili alichopata!

Nilitoa maoni humu kwamba, huenda Lisu zile harakati zake za toka miaka ya 90 kupigania madini zilikuwa zinamnufaisha yeye binafsi ndio maana alipoona Jpm yuko serious akaamua sasa ageuke kinyonga.

Kuhusi hao waliosaini mikataba, hao tunawasamehe maana walikuwa enzi na akili za kimangungo!

Lakini haka kajamaa haka kako kizazi cha wasomi kumbe kana uza nchi live?
Nyie ndio mnafanya JF siku hizi kionekane kijiwe cha wajinga.
 
Kwa hiyo kamanda una maanisha Tundu Lissu ndio alikuwa ana wasiliana na amabeberu kutuhujumu na kutusaliti?
Inahusianaje na niliyo andika? Mbona una akili nzito utadhani ni Katibu wa ccm wa kata?
 
Nadhani najadili hili na mtoto mdogo au MTU mzima asiye jielewa.
Mungu anaadhibu wakosaji lakini haadhibu kwa usiri kutumia watu wasiojulikana.
Anaogopa nini mpaka afanye kwa usiri mkubwa? Ukitaka kumhusisha Mungu jambo lolote kaa chini utafakari kwanza ukuu wake na sio kuropoka tuu
Nasikia ilikuwa mchana kati ya saa sita na saa nane! Nadhani najadiliana na mtu mzima anayejielewa.
 
Ni suala la muda tu, yanaendelea kufumuka taratibu. hatimae wataanikwa wote na hawa watakuja kufikishwa 'mnazi mmoja' kwa ajili safari ya jehenam. Muda ni mwalimu mzuri
 
Basi alipata alichostahili!

Na huyu anazidi kujivua nguo! Anafikiri anaongea ukweli kumbe anajianika jinsi alivyokuwa analisaliti taifa!
Subiri tutamuinesha adhabu yake hapo oktoba.
Yani kilaza Kama wewe umzidi akili lissu Hadi ujue anajianika.

Yani wewe standard 7 ujilinganishe na Alumni wa Warwick University.

Pumbavu.
 
Kwa hiyo lisu amekiri kuwa alikuwa anaiba taarifa nyeti za nchi yake ili kuwasaidia mabeberu!. Nafikiri Afrika hakujawahi kuwa chama cha upinzani chenye itikadi za hovyo km cdm, haiwezekani Taasisi ya Urais wampe kugombea mtu ambaye hana uzalendo na nchi yake.
 
View attachment 1543623
Mgombea Urais wa Chadema katika uchaguzi mkuu ujao mwishoni mwa mwaka huu, ametoa madai mazito mjini Njombe jana katika ziara zake za kutafuta wadhamini, akimuhususisha Rais, kuhusu jaribio la kuuawa kwake, lililofanyika September 7 mwaka 2017.

Akihutubia umati wa wananchi, alikumbushia historia ya tukio lake la kumiminiwa risasi, ambapo aliponea chupuchupu kuuawa na kukimbizwa nchi za nje kwa matibabu.

Akisimulia mkasa huo alieleza kuwa kuna "connection" kati ya hotuba aliyoitoa Rais Magufuli, ya uzinduzi wa ripoti ya tume ya madini, masaa takribani mawili, kabla ya kupigwa kwake risasi, aliyotoa akiwa Ikulu, jijini Dar-es-Salaam.

Aliendelea kueleza kuwa katika hotuba hiyo aliyotoa Rais Magufuli, ambayo alidai ipo ndani ya YouTube, alimnukuu Rais akiyatamka maneno yafuatayo "Katika mapambano ya kijeshi, huwa wana kawaida ya kumwua, askari yeyote ambaye anawasiliti katika mapambano yao, vile vile katika vita ya kiuchumi ambayo nchi yetu inapigana hivi sasa, hatuwezi kuruhusu ku-survive kwa mtu mmoja, ambaye imebainika amekuwa akiwasiliana mwanasheria wa kampuni hiyo ya madini, Deo Mwanyika, ili kumwibia taarifa mbalimbali nyeti, katika lengo lao wakishirikana na mabeberu kutoka nje ya nchi, katika kutuhujumu malipo yetu ya madini, hastahili kabisa ku-survive" mwisho wa kunukuu.

Tunajua kuwa katika tukio hilo la kupigwa kwake risasi mwaka 2017, Tundu Lissu, Jeshi la Polsi limekuwa likutaaminisha kuwa uchunguzi wa tukio hilo unakwamishwa na Tundu Lissu, muhanga mkubwa wa tukio hilo, pamoja na Dereva wake, ambao wote walikuwa wameenda nchi za nje kwa matibabu.

Hivi sasa Tundu Lissu amesharudi nchini na amewapa "hints" ya kilichompata siku ile ya kutisha sana, ambapo "watu wasiojulikana" walimpiga risasi mfululizo 16 mwlini mwake katika jaribio la kutaka kumwua na ameeleza mwenyewe nini kilimtokea siku ile, ambapo Jeshi letu la Polisi, limekuwa likidai kuwa limekwamishwa kuendelea na uchunguzi wake, kutokana na kukosekana ushahidi huo wa Tundu Lissu

Kwa hiyo nadhani Jeshi la Polisi lingeanza kufanyia uchunguzi wa tukio lile sasa, kwa "hints" alizozitoa yeye mwenyewe muathirika wa tukio lile Tundu Lissu.
Kwahiyo Lissu anakili yeye ni msaliti?
 
Mkuu usinilishe maneno, yeye ndio kasema alipigwa risasi sababu ya usaliti kwa nchi

Kwani wewe hukuwepo hapa nchini alipokuwa anasemwa kuwa msaliti ndiyo umesikia kwa Lissu hayo maneno hujawahi kusikia yakisemwa na wenye mamlaka ya kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria maana usaliti ni kosa la jinai
 
Si alisema amesamehe tena akiwa amesimama madhabahuni? Kumbe bado anahasira ee? Hizo kura za hruma hatumpatii.
 
Back
Top Bottom