Tundu Lissu akamatwa na Polisi akiwa Ngorongoro hotel Wilayani Karatu
Ndo maana waliofeli form four ndo walijiunga Upolisi.Nyerere alikuwa na agenja kwa kweli.Imagine waliofeli ndo walikwenda Kusomea upolisi na ualimu. Nyerere hivi ulijua utaishi milele hadi kutuharibu namna hii ,kufanya ujinga uwe kizazi baada ya kizazi.
 
Zipo taarifa kwamba mh lissu kakamatwa, huu ni uonevu ,tutaonewa mpaka lini, tumechoka na unyanyasaji
Itisha kikao cha dharula cha kamati kuu,

Toeni tamko kwa nchi nzima tujue tufanye nini inatosha

Thanks
Wewe unakula raha huko unataka nani akapigwe mabomu!!? Tangulia wewe mbele ukavunjwe miguu ili akili ikukae sawa!
 
Kuna tetesi kuwa Tundu Lissu amekamatwa na Polisi asubuhi hii akiwa hotelini huko Karatu.

Taarifa zaidi kukujia hapahapa jukwaani.

UPDATE:
Waliokamatwa Karatu hadi sasa ni

  1. Makamu Mwenyekiti CHADEMA Tundu Lissu
  2. Walinzi wote wa Tundu Lissu
  3. Katibu wa BAWACHA Catherine Ruge
  4. Mzee Hashim, Mwenyekiti Wa Baraza La Wazee CHADEMA Taifa
  5. Suzan Kiwanga na
  6. Mwandishi wa Jambo TV (Oscar).

Polisi wanaendelea kuwatafuta wengine walio ambatana na Tundu Lissu Wilayani Karatu

View attachment 2744826

====

Leo Septemba 10, 2023 Majira ya saa nne asubuhi Jeshi la Polisi wilaya ya Karatu lilifika Hotel ya Ngorongoro iliyopo Karatu na kuizingira, Polisi hao wakiwa na mitutu ya bunduki pamoja na mabomu. Jeshi hilo liliwaeleza wahudumu wa hotel hiyo kuwa wanataka kujua chumba alicholala Makamu Mwenyekiti wa Chama Bara Mhe. Tundu Lissu wakaelezwa na kwenda kwenye chumba hicho.

Baada ya purukushani ya Jeshi la Polisi na walinzi wa Mhe. Lissu, Jeshi hilo lilingia kwa nguvu katika chumba alichofikia Mhe. Lissu na kuondoka nae bila kueleza wanaenda nae wapi.

Baadae wengine waliokamatwa na Jeshi hilo ni Mhe. Susan Kiwanga, Mjumbe wa Kamati Kuu, Mhe. Catherine Ruge Katibu Bawacha Taifa, Mhe. Twaha Mwaipaya, walinzi wa Mhe. Lissu pamoja na watu wengine.

Tunaendelea kufuatilia kinachoendelea Karatu.
Bila polisi ccm ina wakati mgumu sana kwa wananchi, alishasema muda tu
 
Sababu za kukamatwa ni zipi?? Mbona hii nchi inamambo ya ajabu ajabu. Kweli wa Afrika tunalaana hasa hawa polisi hizi kazi ni za laana hawa majamaa wamelaaniwa sio bure. Anatokea mzalendo (Tundu lissu) kuwatetea haki zao na maslahi yao dhidi ya mafisadi ccm halafu wanamkamata sasa hao wanatofauti gani manyani wasiojielewa ukiangalia maisha yao ya shida, familia zao zinaishi maisha magumu lakini bado wanakaza fuvu njaa njaa zimewajaa
Polisi sababu yao kuu wanasemaga waliapa😂

Sasa sijui waliapa kiapo cha UJINGA au nini 😂😂😂
 
Sikiliza hotuba za mama Rais, anaweza akawa anacho zungumza sicho ana maanisha.. ila waliopale juu wanafata kile asicho maanisha ndio shida hapo.. Kama taifa na watendaji wake, sanaa ya kutafsiri kauli za viongozi wenye mamlaka ya juu kabisa, bado sana.. Kiongozi anaweza sema nyeusi kumbe ana maanisha pink
Anahofu nini? Kwanini nyeusi asiite nyeusi?
 
Kazi ya vyama vya upinzani, si kuisifu na kupongeza serikali iliyopo madarakani. Ni pamoja na kuwaonyesha wananchi, madhaifu na kasoro za serikali ili wasiwarudishe madarakani.

Ni jukumu la watawala kuwaaminisha wananchi uhalali wa yanayofanyika. Si kuwalazimisha kuamini wanachokifanya.
 
Sikiliza hotuba za mama Rais, anaweza akawa anacho zungumza sicho ana maanisha.. ila waliopale juu wanafata kile asicho maanisha ndio shida hapo.. Kama taifa na watendaji wake, sanaa ya kutafsiri kauli za viongozi wenye mamlaka ya juu kabisa, bado sana.. Kiongozi anaweza sema nyeusi kumbe ana maanisha pink
Lugha za kijasusi hizo.. na ndomana huwa yanaendelea haya. Huenda ndo maelekezo hayo wanayopewa
 
Hao badala ya kufanya siasa wamegeuka kua wanaharakati wakudandia matukio na kuchonganisha serikali na raia, sisi upinzani hatujui siasa,....tumeshindwa kujenga grassroot ofisi za chama na kufungua matawi kwa kuuza philosophy za chama tunatafuta umaharufu kupitia matukio mbali mbali.
Kuna haja ya kupata chama cha siasa ambacho kinaweza kujenga sera mbadala ya chama tawala sio kupunga kila jambo bila kuonyesha mbadala wake, Lissu amakua mwanaharakati sio mwana siasa tena bora angefungua NGO ya kutetea hakati zake, kama ni mazingira au haki za binaadamu ili ajulikane iko wapi.
Usichokijua ni kwamba mwanasiasa anayejielewa ni zaid ya mwanaharakati
 
Naamini kuwa , na ninajua kuwa kabla sijafikisha miaka 50 tutakuwa tushaongozwa na jeshi ., kwangu itakuwa furaha na hakika nitaingia kwenye system kama kiongozi mkubwa .

Nimeandika leo tarehe 10/09/2023 naomba nikumbushwe siku ikifika .

Weekend hii nipo nakunywa supu baada ya purukushani za usiku , sasa wewe nichukulie serious nikung'oe meno

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
Ndio kwanzaaa Nida inasoma una 20yrs mpk kufika 50yrs kuna miaka 30 mingine kama hiii ya sasa au mibaya kuliko hii ya sasa ambayo inatucost
 
Usi

Usichokijua ni kwamba mwanasiasa anayejielewa ni zaid ya mwanaharakati
Ila sasa wabadilike wawe wana siasa hizo harakati hazipeleke chama popote, hatuja pata mbadala wa ccm mpaka leo, hao watu ni uchu wa madalaka hawana mikakati yoyote.
 
Back
Top Bottom