Tundu Lissu akamatwa na Polisi akiwa Ngorongoro hotel Wilayani Karatu
Kuna tetesi kuwa Tundu Lissu amekamatwa na Polisi asubuhi hii akiwa hotelini huko Karatu.

Taarifa zaidi kukujia hapahapa jukwaani.

UPDATE:
Waliokamatwa Karatu hadi sasa ni

  1. Makamu Mwenyekiti CHADEMA Tundu Lissu
  2. Walinzi wote wa Tundu Lissu
  3. Katibu wa BAWACHA Catherine Ruge
  4. Mzee Hashim, Mwenyekiti Wa Baraza La Wazee CHADEMA Taifa
  5. Suzan Kiwanga na
  6. Mwandishi wa Jambo TV (Oscar).

Polisi wanaendelea kuwatafuta wengine walio ambatana na Tundu Lissu Wilayani Karatu

View attachment 2744826

====

Leo Septemba 10, 2023 Majira ya saa nne asubuhi Jeshi la Polisi wilaya ya Karatu lilifika Hotel ya Ngorongoro iliyopo Karatu na kuizingira, Polisi hao wakiwa na mitutu ya bunduki pamoja na mabomu. Jeshi hilo liliwaeleza wahudumu wa hotel hiyo kuwa wanataka kujua chumba alicholala Makamu Mwenyekiti wa Chama Bara Mhe. Tundu Lissu wakaelezwa na kwenda kwenye chumba hicho.

Baada ya purukushani ya Jeshi la Polisi na walinzi wa Mhe. Lissu, Jeshi hilo lilingia kwa nguvu katika chumba alichofikia Mhe. Lissu na kuondoka nae bila kueleza wanaenda nae wapi.

Baadae wengine waliokamatwa na Jeshi hilo ni Mhe. Susan Kiwanga, Mjumbe wa Kamati Kuu, Mhe. Catherine Ruge Katibu Bawacha Taifa, Mhe. Twaha Mwaipaya, walinzi wa Mhe. Lissu pamoja na watu wengine.

Tunaendelea kufuatilia kinachoendelea Karatu.
View attachment 2744848
Samwel Welwel
Huyu aachiwe 2028 🤣🤣🤣
 
Wewe kweli alfu lela ulela? Yaani ulichokiandika hapa ndiyo unaita siasa?
Aliyewaharibu ni huyo aliyewafundisheni habari za siasa na uana harakati.
Sababu yeye mwenyewe uwezo wake uligotea mahala.
Hakuna siasa isiyo na harakati. Msipende kukariri vitu kama vile mmekatazwa kutumia akili zenu. Jambo lolote lile, iwe dini, siasa, Taaluma au kingine chochote kile ili kuweza kukieneza kinahitaji harakati.
Kuna tofauti kati mwanaharakati na mwana siasa, activist vs politicians. Neenda akajifunze hao watu ni tofauti sana, hapa Tanzania tuna activists sio wanasiasa tena.
 
Mama alisema yeye ana ngozi ngumu sasa imekuaje ameshindwa kuvumilia spana za Kamanda Lissu.
 
Naamini kuwa , na ninajua kuwa kabla sijafikisha miaka 50 tutakuwa tushaongozwa na jeshi ., kwangu itakuwa furaha na hakika nitaingia kwenye system kama kiongozi mkubwa .

Nimeandika leo tarehe 10/09/2023 naomba nikumbushwe siku ikifika .

Weekend hii nipo nakunywa supu baada ya purukushani za usiku , sasa wewe nichukulie serious nikung'oe meno

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
Amka wewe Lisu katiwa Mbaroni utajikojolea 😆😆😆😆
 
Mama alisema yeye ana ngozi ngumu sasa imekuaje ameshindwa kuvumilia spana za Kamanda Lissu.
Matusi hayahusiani na ngozi ngumu,hujiulizi mbona Mbowe na Mnyika na wengine Huwa hawakamatwi isipokuwa huyu mtukutu? Apewe adabu zake.

Bado Slaa na Maandamano yake
 
Mbona Lissu na CDM wanafanya siasa soft sana...

Hivi waliwahi msikiliza Wakajocka au Odinga?

Kama watu yawaitaki CCM hawaitaki...

Sehemu zote zenye resources nchi hii lazima CCM iwape wageni.... sasa Kuna jipya gani mtu akisema? Makosa yalifanywa na Mwinyi, Mkapa na JK... bunduki haizuii ukweli huo.

Suala la Ngorongoro ni kweli kwamba serikal imekosea na inaoosea kuhamisha watu kwenye ardhi yao ya asili kupisha kitu kinachoitwa wawekezaji haiondoi wala haibadilish ukweli huo.

Mageuzi ya kisiasa Tanzania ni lazima na ni muhimu kwa maendeleo ya kizaz cha sasa na kijacho.... hili hakuna wa kulizuia..
 
Mbona Lissu na CDM wanafanya siasa soft sana...

Hivi waliwahi msikiliza Wahackoya au Odinga?

Kama watu yawaitaki CCM hawaitaki...

Sehemu zote zenye resources nchi hii lazima CCM iwape wageni.... sasa Kuna jipya gani mtu akisema? Makosa yalifanywa na Mwinyi, Mkapa na JK... bunduki haizuii ukweli huo.

Suala la Ngorongoro ni kweli kwamba serikal haiondoi wala haibadilish ukweli huo.

Mageuzi ya kisiasa Tanzania ni lazima na ni muhimu kwa maendeleo ya kizaz cha sasa na kijacho.... hili hakuna wa kulizuia..
Mageuzi ya kisiasa Tanzania ni lazima na ni muhimu kwa maendeleo ya kizaz cha sasa na kijacho.... hili hakuna wa kulizuia[emoji419][emoji375]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna tetesi kuwa Tundu Lissu amekamatwa na Polisi asubuhi hii akiwa hotelini huko Karatu.

Taarifa zaidi kukujia hapahapa jukwaani.

UPDATE:
Waliokamatwa Karatu hadi sasa ni

  1. Makamu Mwenyekiti CHADEMA Tundu Lissu
  2. Walinzi wote wa Tundu Lissu
  3. Katibu wa BAWACHA Catherine Ruge
  4. Mzee Hashim, Mwenyekiti Wa Baraza La Wazee CHADEMA Taifa
  5. Suzan Kiwanga na
  6. Mwandishi wa Jambo TV (Oscar).

Polisi wanaendelea kuwatafuta wengine walio ambatana na Tundu Lissu Wilayani Karatu

View attachment 2744826

====

Leo Septemba 10, 2023 Majira ya saa nne asubuhi Jeshi la Polisi wilaya ya Karatu lilifika Hotel ya Ngorongoro iliyopo Karatu na kuizingira, Polisi hao wakiwa na mitutu ya bunduki pamoja na mabomu. Jeshi hilo liliwaeleza wahudumu wa hotel hiyo kuwa wanataka kujua chumba alicholala Makamu Mwenyekiti wa Chama Bara Mhe. Tundu Lissu wakaelezwa na kwenda kwenye chumba hicho.

Baada ya purukushani ya Jeshi la Polisi na walinzi wa Mhe. Lissu, Jeshi hilo lilingia kwa nguvu katika chumba alichofikia Mhe. Lissu na kuondoka nae bila kueleza wanaenda nae wapi.

Baadae wengine waliokamatwa na Jeshi hilo ni Mhe. Susan Kiwanga, Mjumbe wa Kamati Kuu, Mhe. Catherine Ruge Katibu Bawacha Taifa, Mhe. Twaha Mwaipaya, walinzi wa Mhe. Lissu pamoja na watu wengine.

Tunaendelea kufuatilia kinachoendelea Karatu.
View attachment 2744848
Samwel Welwel
Lissu nitatazi la kupotea kwa Dalla mtaani baada ya kukamatwa dolla zitarudi mtaani
 
Back
Top Bottom