Tundu Lissu: Baada ya uchaguzi nilitakiwa kushughulikiwa, amri ilisema wasikosee shabaha

Tundu Lissu: Baada ya uchaguzi nilitakiwa kushughulikiwa, amri ilisema wasikosee shabaha

Kama mikutano ya hadhara ni fursa ya kufitinisha na kuchafua watu tunahaja ya kuangalia. Ila pia ni vizuri kuwapa fursa watu kutema sumu
===
Tundu Lissu amesema alirejea Tanzania mwaka 2020 kwa ajili ya uchaguzi na alilazimika kuondoka tena mwaka huo kwa sababu mtesi wake alitoa amri ashughulikiwe tena bila kukosea shabaha. Tundu Lissu ambaye sasa ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA-Taifa alishambuliwa kwa risasi 16 siku ya Septemba 7, mwaka 2017 na kuondoka nchini kwa sababu ya matibabu.

Lissu amesema baada ya kupewa taarifa kuwa anatafutwa ili auawe mara baada ya uchaguzi, Oktoba 31, 2020 alijificha. Baadae alipata taarifa kuwa maficho yake yamejulikana na akashauriwa akimbie ndipo alipowasiliana na balozi wa Ujerumani ili kunusuru nafsi yake.

Alipofika katika Ubalozi wa Ujerumani, kabla ya kuruhusiwa kuingia magari matatu yalifika katika ubalozi na kutaka kumchukua kumpeleka kituo cha polisi. Lissu alibisha kwa kutaka kujua kosa lake na sababu ya kupelekwa kituoni.

Wakati wametaka kumuingiza kwenye gari, Naibu Balozi wa Ujerumani alitoka na kuwahoji waliokuwa wanataka kumchukua Lissu. Naibu balozi aliomba kama wanaweza kwenda na Lisu kwenye mahojiano ambapo waliotaka kumchukua walikubali, hivyo Naibu Balozi na Polisi na Lissu walienda wote kituoni na Naibu balozi aliuliza kuhusu muda watakao muhoji na kusubiri ili wakimaliza waondoke nae.

Baada ya majibizano, Naibu balozi alimuambia Lissu kuwa nchi hii sio salama hivyo wakampa makazi katika makazi ya ubalozi wa ujerumani. Alikaa hapo kwa siku nane akisaidiwa kupata vitu vyote vya safari ikiwemo Passport na VISA. Siku husika ya safari Naibu Balozi alimsindikiza Lissu hadi kwenye ndege ili kwenda Ujerumani kujificha


View attachment 2508265
View attachment 2508321
View attachment 2508326
View attachment 2508335
View attachment 2508336
Duh kama aliosema ni kweli basi Hayati Magufuli alikuwa na roho mbaya sana
 
Mfu Magufuli ataendelea kuwanyoosha vilaza chadema, Lissu bado anahitaji dawa ya kufungwa mdomo na bahati mbaya mwenye dawa hayupo.
 
Back
Top Bottom