Uthibitisho huo umetolewa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, ndug.Tundu Lissu jana Jumapili, Machi 05, 2023 wakati akijibu maswali kwenye hadhara iliyofanyika kwenye mtandao wa Clubhouse.
Akisema “Chama (Chadema) kimeanza kupokea ruzuku mwezi huu (Machi) ambayo hatukuichukua tangu ulipofanyika uchaguzi mkuu wa 2020".
“Tumepokea sehemu tu ya pesa hizo na kiasi kilichosalia tutapewa siku za usoni. Tumeamua kuichukua kwasababu ya ahadi ya maridhiano yanayoendelea,” alisema Lissu.
Chadema iligoma kuchukua ruzuku hiyo inayokadiriwa kuwa ni zaidi ya sh. Milioni 110 Kwa mwezi baada ya kukataa matokeo ya uchaguzi wa 2020 waliyodai haukuwa uchaguzi bali ulikuwa ni uchafuzi na najisi.
( ushahidi soma link :
March 5, 2023 – Demo Krasia
Nina mambo machache tuu juu ya hili.
Kwanza huu ni ushahidi mwingine wa wazi na tukubaliane ya kwamba ACT wazalendo ni chama kiongozi nchini ,chenye uwezo wa kuona mbele maili 100 kabla ya wengine kuona. Hii ina maana ya kwamba ACT wazalendo ni chama chenye viongozi wenye maoni,fikra yakinifu na tunduizi katika kufanya maamuzi ambayo wengine watakuja kuyafuata baadaye,hii ndiyo maana ya chama kiongozi.
Walisema hivi hapo nyuma "Uchaguzi ulikuwa najisi, hao ACT wazalendo sio wapinzani wao kuchukua ruzuku na kuingia GNU na kupeleka wabunge ni dhahiri wana halalisha najisi,sisi Chadema kamwe hatutachukua Ruzuku inayotokana na uchafuzi na najisi ya uchaguzi wa 2020".
Ninachopishana na hawa ndugu zetu ni kitu kimoja tuu ni uharaka wao wa kushambulia vyama vingine na viongozi wa vyama vingine wakidhani wao ni malaika kutoka mbinguni huku wakiwa hawana njia mbadala wala suluhu yeyote na hatimaye hujikuta wakiangukia katika njia ile ile ya waliowatukana na kuwapinga kufuata njia hiyo .Vyama hivi vya siasa ni vyama tofauti,vyenye uongozi tofauti, itikadi tofauti,mipango tofauti ,vikao vya maamuzi tofauti ila hawakuwahi heshimu maamuzi ya chama chetu yaliyotokana na vikao vya ndani na maamuzi ya wanachama wetu mbali ya sisi kuheshimu maamuzi yao na vikao vyao .Wajifunze sasa hili ni funzo kubwa kwao.
Tulipoamua kama chama kuingia serikali ya umoja wa kitaifa (GNU) ,kamwe hawakuheshimu maamuzi yetu kama chama walitutukana na kumshambulia kiongozi wetu wa chama Mh. @zittokabwe na chama chetu ,tulikaa kimya tukijua watapita njia yetu tuu.Leo hii wanataka peleka wabunge wa viti Maalumu Bungeni hatimaye wamepita njia yetu.
Tulipoamua kuruhusu wabunge,wawakilishi na Madiwani kwenda kuapa kuendelea na majukumu yao na kuchukua Ruzuku ,kamwe hawakuheshimu maamuzi yetu kama chama walitutukana na kumshambulia kiongozi wetu wa chama Mh. @zittokabwe na chama chetu ,tulikaa kimya tukijua watapita njia yetu tuu.Leo na wao wameamua kupokea Ruzuku , hatimaye wamepita njia yetu.
Tulipoamua kutafuta maridhiano na kushiriki Mikutano miwili kule Dodoma, wa tarehe 16 na tar.17 Desemba 2021 na ule wa tar .05 April 2022 Mkutano wa Haki, Amani na Maridhiano ambao Mh. Rais @samia_suluhu_hassan alikuwa mgeni Rasmi.
Ulioandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) @tcdemokrasia_hq chini ya Mwenyekiti wake Mh. @zittokabwe kwenye ukumbi wa Mikutano wa Hazina Jijini Dodoma ,kamwe hawakuheshimu maamuzi yetu walitutukana na kumshambulia kiongozi wetu wa chama Mh. @zittokabwe na chama chetu kwa kushiriki wakisema hatuna bargain cheap ya kufanya mazungumzo na Rais ,ambaye ni Mwenyekiti wa CCM matusi yalikuwa yote dhidi yetu tukiitwa CCM-B. Tulikaa kimya tukijua watapita njia yetu tuu. Leo hii wao kutwa kucha Ikulu na hadi kumualika Mh.Rais na Mwenyekiti wa CCM katika mkutano wa BAWACHA .
Tulipoamua kuingia kwenye kikosi kazi kilichoundwa wao walikataa wakisema kikosi kazi kilichoundwa na Rais ambaye ni Mwenyekiti wa CCM hakina maana na hakitaleta Matokeo yeyote ,kamwe hawakuheshimu maamuzi yetu kama chama walitutukana na kumshambulia kiongozi wetu Mh. @zittokabwe na Chama chetu .Tulikaa kimya tukijua watapita njia yetu tuu.Hatimaye kikosi kazi cha Zanzibar kilichoundwa tar. 10 Oktoba 2022 na wao Chadema walishiriki na wakatoa mjumbe kuwa katika kikosi kazi ambaye ni Makamu Mwenyekiti wao wa Zanzibar ndug. Said Issa Muhammed. Hatimaye wamepita njia yetu.
Kikosi kazi huku bara kikakusanya maoni na kigawa maazimio ya utekelezaji katika makundi matatu mambo yanayohitaji utekelezaji wa muda mfupi,muda wakati na mrefu.Mikutano ya hadhara ni jambo lililohitaji utekelezaji wa muda mfupi ,bado ndugu zetu hawa wakaibuka wakatukana na kutushambulia tulikaa kimya sababu tulijua matunda ya maridhiano na kikosi hata wao watapongeza na kufurahia na kunufaika ,tulijipa muda sababu tunaona mapema kuliko wao.
Hatimaye tar 3/Jan/2023 Rais Samia akatengua zuio la mikutano ya hadhara akirudia mara zote kusema "Jambo hili ni katika maazimio ya kikosi ya muda mfupi na nina kipongeza kikosi kazi". Ndugu zetu katika hili wakajitokeza kusifu ikiwa walipinga kikosi kazi na mchakato wake wote.Tulijua matunda haya ni wote kwa maslahi ya wote hata kwa waliotukana na kukashifu .
Leo hii wamefuata nyayo za ACT WAZALENDO katika kila tulichoamua kukifanya licha ya wao kututukana leo hii wamegeuka kukifanya wao leo wanahubiri maridhiano ambapo walitutukana tulipo hubiri,wamepokea ruzuku ambapo walitutukana tulipopokea ,wamekuta na Rais ambapo walitutukana tulipokutana nae, wanataka wapeleke wabunge Bungeni viti maalumu ambapo walitutukana tuliporuhusu wabunge wetu kwenda Bungeni na wawakilishi, sasa wanawatambua madiwani wao wote nchini waliotokana na uchaguzi na uchaguzi wa 2020 ,ambapo walitutukana tuliporuhusu madiwani wetu .
Maswali kwao.
Je,unajisi wa uchaguzi wa 2020 umeisha lini? hadi kupokea Ruzuku waliyokataa wakisema inatokana na najisi ya uchaguzi wa 2020 wakitukana ACT wazalendo kwa kupokea Ruzuku. Na waaminiwe kwa lipi lingine watakalogomea?
Je, wanaonaje matusi yote waliyotukana ACT wazalendo sasa wajigeuzie wao? .kama kweli wanapenda haki na usawa.
Maswali hayo yakikosa majibu iwe ni somo kwao kujifunza na kuheshimu maamuzi ya vyama vingine na wakubali ACT -wazalendo ni chama kiongozi.
Ahsante.
Abdul Nondo.
Mwenyekiti wa Ngome ya vijana ACT-wazalendo Taifa.