Hufahamu ni kupitia kudharau hao hao wananchi Hosni Mubarak ,Muamar Ghadafi walijikuta hawana msaada hata kwa majeshi waliyokuwa wakiyalipa hata kiasi ambacho Tanzania hamlipi wanajeshi wenu?
Hosni Mubarak aliwaita waandamanaji ni vichaa na wapuuzwe , akamwaga jeshi mtaani jeshi lilizidiwa na hadi likawaunga mkono wananchi akabaki yeye na familia yake tu.
Muamar Ghadafi yeye alisema hakuna wa kumtoa uongozini maana hata wasiofanya kazi anawalipa vizuri tu mwisho wa mwezi na hatokwenda uhamishoni , alijikuta ametoka ikulu hadi kuishi jangwani kutoka mamia ya walinzi hadi walinzi wanne.
Nimejaribu kukupa mifano michahe ya historia , na historia ina tabia ya kujirudia.