Tundu Lissu nisikilize, upepo wa kisiasa uko kwako 100% lakini mkakati wa kuibiwa kura umeshaanza kusukwa, jiandae

Tundu Lissu nisikilize, upepo wa kisiasa uko kwako 100% lakini mkakati wa kuibiwa kura umeshaanza kusukwa, jiandae

Joined
Nov 27, 2024
Posts
43
Reaction score
127
Mimi sio mwanachama wa Chadema na sifurahii siasa zao za kutukana tukana viongozi hivyo hasa vijana wao wanavyofanya harakati za kijinga mitandaoni jambo linalosababisha wawaudhi viongozi wa serikali na ndio maana wanakamatwa kamatwa hivyo lakini najaribu kulinganisha sifa za uongozi kati ya Mbowe na Lissu.Nimekuwa namfuatilia sana Mbowe, huyu kiongozi ni mtulivu sana, mvumilivu na sio mwanaharakati.

Utulivu wake, uvumilivu wa kisiasa, kufanya majadiliano na serikali jinsi ya kuleta amani kunamfanya awe na mvuto sana kwa watu.

Sasa kuna huyu Domokaya Tundu Lissu, huyu aina ya siasa zake za kutukana bila mipaka, tukio la kupigwa risasi akiwa anatoka bungeni, kuongea maneno magumu ya kuhatarisha usalama wa nchi ndio kumewafanya vijana wengi wa chadema wampende.

Kisiasa, upepo kiukweli uko kwa Lissu.Kama uchaguzi utakuwa huru na haki, hakutakuwa na makando makando Lissu anakwenda kumdondosha Mbowe kwa kura nyingi sana.

Vijana waliochoka maisha ndani ya chadema wanapenda varangati na dola, ndio maana wengi wamepata dhoruba za dola.

Hawa vijana hawajui kuwa haya wanayoyafanya leo Mrema ameshawahi kuyafanya sana akiwa NCCR akashindwa.CUF ya Lipumba ilikuwa moto, Prof Lipumba amejeruhiwa sana katika harakati za CUF jino kwa jino, nao walishindwa.

Chadema hawajafikia hata robo ya kash kash za CUF ya enzi ile sio mchezo.Sasa wanamuona Lissu ndio anaweza mambo hayo.

Nna uhakika Lissu hawezi kupewa uenyekiti, atashinda lakini ataibiwa kura zake, kwa sababu akishinda akina Mnyika, Boni Yai na wengine wote watakwenda na maji.Kwa hiyo hao hawawezi kukubali Lissu awe mwenyekiti.

Mnalalamika dola inaiba kura kumbe nyie pia mnatengeneza mikakati ya kumuibia kura Lissu.
 
Weka ushahidi wa Mpango huo wa wizi wa kura.
 
Hiki ni Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
 
Back
Top Bottom