Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Rais Magufuli alitoa rushwa Kibiti Mil. 5 na akanunua jogoo laki moja wakati kashapitishwa kugombea Urais. Nitamuwekea pingamizi

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Rais Magufuli alitoa rushwa Kibiti Mil. 5 na akanunua jogoo laki moja wakati kashapitishwa kugombea Urais. Nitamuwekea pingamizi

Kifungu ukichokitaja kinaleza kabisa kutoa pesa,zawadi,ajira,au upendeleo wowote ule ni makosa aidha iwe kipindi cha nomination process, election au campaign period
Kwani kaanza jana kutoa hizo pesa? Si mnemueleza rais wenu mtarajiwa wa FB TWITTER NA INSTAGRAM kwamba ana miaka mitano anagawa pesa mitaani kama Askofu wa Mererani. Naona hafahamu ama dawa alizopewa ni kali sana
 


Mhe. Tundu Lissu mgombea Urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA ameendelea kusisitiza kuwa hawezi kufungwa kwa kesi alizo nazo Mahakamani na kwamba haziwezi kumzuia kugombea Urais.

“Hafungwi mtu hapa” “Nina kesi sita Kisutu na zote ni za uchochezi.” Baraza Kuu la chama cha upinzani nchini Tanzania CHADEMA, limemchagua Tundu Lissu kuwa mgombea wake wa Urais katika Uchaguzi Mkuu 2020.

Mhe. Lissu ameenda mbali zaidi kwa kusema kuwa si yeye tu anayeweza kuwekewa pingamizi la kugombea Urais bali hata Mhe. Rais Magufuli pia anaweza kuwekewa pingamizi.

"Nani aliyesema kwamba CCM hawawezi kuwekewa mapingamizi? Nani aliyesema mgombea urais wa CCM, John Magufuli hawezi kuwekewa mapingamizi.? " Tundu Lissu, Mgombea Urais wa CHADEMA"

Kwenye fomu ya mapingamizi, kwenye sababu 16, la 16 Magufuli amekiuka Mambo yaliyokatazwa moja wapo ni rushwa maana ukishaingia kwenye uchaguzi huruhusiwi kutoa rushwa, Magufuli akiwa anatoka kumzika Mkapa Lupaso, alifanya nini Kibiti? " Tundu Lissu, Mgombea Urais wa
CHADEMA

Lissu amesema kitendo cha Rais kutoa fedha Kibiti, kununua jogoo kwa Laki Moja ni rushwa wakati wa uchaguzi.

Mhe. Lissu katika moja ya sera zake amesema iwapo atashinda basi atakuwa na jukumu kubwa la kurudisha uhusiano wa nchi kimataifa.

"Tukishinda urais wa Tanzania, mimi nitakuwa Rais wa Katiba mpya. Kama tunataka mfumo mzuri wa utawala, mahali pa kuanzia ni Katiba mpya. Hii ndilo tutaanza nalo. Haina maana hatutajenga shule, kuboresha Sekta ya Afya '

MY TAKE: Bado tutandelea kushuhudia matamko mengi kwenye Uchaguzi huu ni juu yetu watanzania kumpima kila mgombea ili tupate kiongozi bora kwa maslahi mapana ya Taifa letu.

Lissu nae dishi limeyumba siyo!?, Ashaona wapi rushwa inatolewa kwa namna ile!?.

Hebu aache utopolo wake aongee vitu vyenye mantiki bhana. Ujue wapiga kura wanasikiliza tu upuuzi wake huo ohoooo.
 
Hapa nafikiria sana kwanini lisu ashaanza kujihisi kunyimwa fomu? kama yuko clean why anaanza kutengeneza picha ya kunyimwa fomu na inajulikana huyu ni mwanasheria sasa kama anazijua sheria hofu yake ni nn?

Atulie mpk siku iyo atakayoenda kuchukua !
Mi pia najiuliza kwanini anakomalia kuingia barabarani sio mahakama kuitafuta haki yake! Naanza kupata wasiwasi huyu jamaa kaja kufanya fujo sio uchahuzi
 
Kwahio sasa hivi Magufuli si Rais tena ni mgombea uRais tu? Kwa maana hii hawezi tena kufanya majukumu yake kama Rais?
 
Kesi ya kitumbafu kabisa hii.

Rais alikuwa kwenye majukumu yake ya kila siku, Bado NEC haijampitisha kama mgombea kwa nafasi ya Urais, Bado kampeni hazijaanza Rasmi.
Bado NEC haijampitisha....nimeelewa.
 
Si ungoje umuwekee pingamizi. Kelele za nini? Mbona unafanya mambo kama LAYMAN na wewe ni wakili Msomi? Kwa nini kuweka silaha zako hadharani kama unaona zitakusaidia!? Nyamaza usubiri utende. Tuone. PERIOD!
 
Anahaki ya kujinadi mkutanoni kwake..

Kikubwa tu waje watushawishi uraiani maana hizo zote ni kelele.
 
Katiba Mpya inahitajika hili taifa sio Mali ya mtu mmoja au kundi la watu wachache wanaojiamulia kufanya lolote kwa matakwa yao

Sio Jambo jema mtu kujiamulia kufanya maamuzi makubwa bila kufuata utaratibu hasa wa kibunge

We really need changes but not like this ...
 
Bado NEC haijampitisha....nimeelewa.
Rais ndio amekuwa nominated na CCM kugombea nafasi ya Urais.

Ila Bado hatupo kwenye Campaign process ambapo ndipo vyama huuza sera baada ya wagombea wake kuidhinishwa na NEC.

Pia hatupo kwenye Election. (Uchaguzi).

Rais yupo kwenye majukumu yake ya kawaida kabisa.

Hivyo Hawa wapiga kelele hawana hoja.
 
Mi pia najiuliza kwanini anakomalia kuingia barabarani sio mahakama kuitafuta haki yake! Naanza kupata wasiwasi huyu jamaa kaja kufanya fujo sio uchahuzi
Kama anadhani hapa, Tanzania, ni mahali pa kufanyia hizo fujo, KAKOSEA SANA na hata hao waliomtuma wanapajua hapa. Yeye afanye siasa tu kama ndio zilizomrudisha SIYO FUJO. Kama hapajui vizuri BASI ATAPAJUA! Huo ndio ukweli na siyo vitisho kwani hajui kuwa dawa ya moto ni moto?
 
Kama anadhani hapa, Tanzania, ni mahali pa kufanyia hizo fujo, KAKOSEA SANA na hata hao waliomtuma wanapajua hapa. Yeye afanye siasa tu kama ndio zilizomrudisha SIYO FUJO. Kama hapajui vizuri BASI ATAPAJUA! Huo ndio ukweli na siyo vitisho kwani hajui kuwa dawa ya moto ni moto?
Ibeni kura tu fujo zitafanyika tu!
 
Mi pia najiuliza kwanini anakomalia kuingia barabarani sio mahakama kuitafuta haki yake! Naanza kupata wasiwasi huyu jamaa kaja kufanya fujo sio uchahuzi
Ulishawahi sikia Tanzania Mahakama zinaruhusu kura za nafasi ya Urais kama zimeibwa kesi inapelekwa mahakamani?
 
Back
Top Bottom