Tundu Lissu: Rais Samia amenilipa stahiki zangu nilizonyimwa na Magufuli

Tundu Lissu: Rais Samia amenilipa stahiki zangu nilizonyimwa na Magufuli

Johnny Sack

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2017
Posts
8,984
Reaction score
19,288
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu amesema Rais Samia amemlipa stahiki zake kama Mbunge ambazo ni kiinua mgongo, Serikali ya Rais Magufuli ilikuwa imekataa kumlipa.

Pia, Serikali ilimuambia aandike barua pamoja na kuambatanisha na nyaraka ili apewe fedha zake za matibabu ambazo Serikali ya Rais Magufuli pia ilikataa kumlipa.

Pia Tundu Lissu amesema wanachama wa CHADEMA ambao walifungwa ama kuwekwa mahabusu kipindi cha Magufuli wameachiwa kasoro kesi chache ambazo nazo zinashughulikiwa.

Tundu Lissu alikutana na Rais Samia alipotembele nchini Ubelgiji ambapo waliongea mambo kadhaa ikiwemo stahiki hizo.

 
Pongezi kwa Samia.

So, Samia kamlipa stahiki zake zote ila bado hajamkubalia kurudi nyumbani? au alishakubaliwa kurudi nyumbani ila yeye ameamua kubaki Ubelgiji kwa mambo yake binafsi?

Atuweke wazi na kwenye hilo, sababu huwa anatoa ahadi za nitakuja tarehe fulani, halafu tarehe hiyo ikifika haonekani bila kutuambia kwanini hajarudi, ili kama lawama zibaki kwa Samia na serikali yake tujue, au kama lawama ni za Lissu binafsi tujue.
 
Back
Top Bottom