Ingawa Rais Samia, kama mwanadamu, anaweza kuwa na mapungufu yake, lakini kwa kweli katika utu, hekima, ubinadamu na busara, Mungu amemjalia. Tumshukuru Mungu kwa kutupa nafasi mbili zilizo kinyume:
Alitupatia kiongozi katili asiye na busara, ili tuone umuhimu wa kuwa na kiongozi mwenye busara.
Akatupatia kiongpzi mwenye busara, ili kutuoneshe ilivyo jambo jema na la furaha kuwa na kiongozi mwema.
Rais Samia, kwa hekima yake, ataheshimika na wengi, tofauti na mtangulizi wake ambaye ameendelea kudharaulika kwa ukatili wake, hata wakati akiwa ameondoka Duniani.
Maombi yetu, Mungu azidi kumjalia busara Rais Samia, maana busara ya kiongozi ni faraja kubwa kwa wanaoongozwa.