Tundu Lissu: Walionipiga risasi ni Kikosi Kazi cha Ofisi ya Rais chini ya Mkuu wa TISS, Balozi Kipilimba

Pascal utaacha lini kujipendekeza hata pasipostahili?

Unasema kwamba anatoa tuhuma kwa vyombo nyeti vya usalama,

Je kwako ni mara ya kwanza kusikia tuhuma kama hizi achilia mbali kutoka kwa Lissu?

Au unataka kujifanya haukusia malalamiko tena makali kutoka ndani ya mhimili mkubwa wa dola (bunge) juu ya utesaji na mauaji yanayo fanywa na hao tiss ? Rejea kauli za wabunge Bashe, Nape, nk ndani ya bunge, Je uliwahi kuwaonya hao wabunge?

Kama wao (vyombo nyeti vya usalama) wamekuwa wakisikia tuhuma hizi kutoka kwa Wananchi mbona hawajawahi kuzitolea ufafanuzi wa maana ili jamii iachane na lawama dhidi yao?

Na ufafanuzi pekee wa kuondoa lawama hizi ni kufanya uchunguzi wa kile kinacholalamikiwa ikiwa ni pamoja na mauaji/ majaribio ya mauaji ya watu yaliyotokea.

Ama kuhusu Rais kukutana na Lissu ni kweli ameonesha nia ila bado kuonesha nia haitoshi bali ni vema nia hiyo ikaandamana na matendo ya kujitenga na uovu. Ilipaswa hata kama ni kwa "kuzuga" Lissu angeoneshwa japo dalili za serikali kuwa kinyume au kutowabeba wale wanaotuhumiwa katika sakata hili.

Wewe Pascal kujipendekeza pasipostahili punguza na zaidi lisaidie taifa letu kwa kusema ukweli.
 
Kama ni kweli kuna "kikosi kazi" basi kama amri hiyo amri ya "Eliminate" Lissu haijatenguliwa bado, ajichunge.

Nani wa kuifuta?
Amri ilishafutika baada ya yule shetani wenu wa chato kufutika.
 

Wewe ulichanga ngapi ndugu?
 
Nasisitiza alichokisema Tundu Lissu hapa ni Ukweli mtupu tena kwa 100% ila ukiwa Mnafiki, Zuzu na Mfia Chama Cha Mauaji kamwe huwezi Kukubaliana nae.
Kwamba ulikuwepo au maelezo ya Lissu ni ushahidi unajitosheleza?
Mbona hujibu swali
 
NAMPINGA LISSU KWA HOJA: 1. Yeye ni mwanasheria anajua umuhimu wa ushahidi kabla ya kutoa tuhuma. Yeye amezungumza tu sawa na mwendawazimu yeyote anavyoweza kuzungumza barabarani, kwani hana ushahidi wowote ambao mimi au wewe utauamini.

2. Lissu, alikuja nchini hapa 2020 na kafanya kampeni nchi nzima. Kazungumza alichotaka ikiwemo kumshambulia Dk. Magufuli ambaye alikuwa Mkuu wa nchi, Rais na Amiri Jeshi Mkuu. Lakini watu walimpuuza. Hicho kikosi anachokijua yeye kingekuwepo na huo ubaya anaouzungumza kingemkosa?

3. Kwa hiyo hapa sioni LOGOS ( maana hakuna facts kwa hata nyaraka moja, hivyo pia sioni logic, zaidi ya maneno MINGI.

4. Lissu, ni mwanasheria hivyo anapaswa kujua utendaji kazi wa mamlaka ya Rais na mihimili mingine. Ndiyo Good governance. Rais siyo mtunza fedha za pensheni au malipo ya wabunge. Ndiyo maana Rais kamjibu atalifanyia kazi. Kuna Bunge, wanasheria lazima wachambue taratibu. Yaani Rais arudi tu aseme Lissu alipwe! No way!

5. Mwisho na kwa umuhimu; Lissu awe na nidhamu anapojadili kitu kumhusu Rais au mamlaka nyjngine halali za nchi. Lissu hana nidhamu ya ulimi na ubongo ndiyo maana aliwahi kumjadili Baba wa Taifa kirahisi.🙏🙏🙏
 
Hatimaye wasiojilina sasa washajulikana, ukishampata Kipilimba basi utakuwa ushawapata wapendwa wetu wote waliopotea ama kuumizwa kwa nyakati tofauti toka 2015 hadi 2021.

Sehemu ya kuanzia ishapatukana.
Tusimsahau ssh naye ni shehemu ya uovu huo ndio maana anaongea lugha yao eti upelelezi hauwezi kufanyika mpaka Lissu awepo
 
Mkuu Mbogi, kila siku humu if, wanaingia madogo wapya, hivyo hawawezi kujua nani aliwahi kusema nini kuhusu wasiojulikana TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe!
Na ufafanuzi pekee wa kuondoa lawama hizi ni fanya uchunguzi wa kile kinacholalamikiwa ikiwa ni pamoja na mauaji/ majaribio ya mauaji ya watu yaliyotokea.

Wewe Pascal, lisaidie taifa letu kwa kusema ukweli.
Kwenye hili la wasiojulikana, nimejitolea hata kufanya uchunguzi





Mabandiko hayo ni uthibitisho wangu kulisaidia taifa kwenye hii issue ya wasiojulikana.

P
 
God of Nazareth anahusika vipi ,Hivi haya mauwaji Na mateso Itakuwa wewe ni katika watu wa kikosi kazi
 

Pascal kumbe nawe umo?
 
Bila sababu za msingi amri halali kiutaratibu ya kumwua Lissu kama ilivyokuwa kwa kina Ben, Mawazo na wengine ilitolewa.

Tofautisha nchi kuwa salama na amri ya kumwua mtu kutolewa.

Vipi amri hiyo ilishaondolewa? Anayetoa amri kama hizo ni Sirro?
Hiyo amri ya kuwaua hao uliowataja ilitolewa na nani, lini na wapi?
 
Kuwajua wahusika waliompiga lisu risasi hakuitaji uwe na elimu hata ya chekechea.
Vinginevyo watuambie wameshindwa kutulinda na hatuko salama
 
Mimi sio nimo, kuna vitu mimi viko kwenye damu, born and bred mumo humo.
P

Walau isiwe kwenye damu Kuna kutesa Na kuwaua binadamu wenzako, mmaisha ni mafupi Na mifano ni mingi tunaiona malipo yake mwisho huwa vipi
 
hii ndio shida ya huyu dogo Pascal amekuwa ni mtu wa kutegesha tu ili anase lakini mitego yake ilishakwama siku nyingi tangu enzi za kakayake MEKO alisha mchana LIVE kuwa kikwao Malaya..oops!!! sorry MAYALA ni NJAA KALI hivyo dogo njaa yake mpaka leo hii naona haijaisha bado anajipendekeza tu kwa mama nae alisha msoma kwamba ni MUNAFIKUNA na hana mpango nae kabsaa hata wa kumpachika ujumbe wa mtaa. MAYALA njaa itammuua
 
Mnafiki Juha huyo achana nae tafadhali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…