Tundu Lissu: Walionipiga risasi ni Kikosi Kazi cha Ofisi ya Rais chini ya Mkuu wa TISS, Balozi Kipilimba

Tundu Lissu: Walionipiga risasi ni Kikosi Kazi cha Ofisi ya Rais chini ya Mkuu wa TISS, Balozi Kipilimba

Walimuita kistaarabu wakajua ni muungwana mwenye hashima zake ataitika akipata wasaa... Bahati mbaya kabla kuitika akaona maisha yako hatarini akakimbilia ubalozin akatiimua

Kumbuka vizuri huyo balozi alimchukuwa wapi , wacha kupakazia
 
Kwa maoni yangu, Tundu Lissu anahitaji ushauri nasaha. Binadamu ukipitia maswahibu na mapito kama aliyopitia, unaathirika ki fizikia, ki emosheni na kisaikolojia, (physical, emotional and psychological), hivyo anahitaji ushauri nasaha jinsi ya kutoka kwenye jinamizi hili na kuendelea na maisha.

Huku kutaja taja majina ya watu, na kutangazia ulimwengu kuwa vyombo vyetu tukuka vya ulinzi na usalama kuwa ndio walio husika, shambulio lake, bila ushahidi wowote, ni kuzidi kuibagaza tuu nchi yetu!.

Ametaja Kikosi kazi kinachojumuisha Polisi, JWTZ na TISS,, hawa ni askari wetu, trained, how could they do such a messy dirty job?. Kwa trained snipers, only one single shot would have finished the job!. Hili hata Mama Samia amewahi kuizungumzia, askari wetu trained wakimiss target by two shots, wanaandika maelezo kujieleza!.

Mimi kwa upande wangu naendelea kusisitiza Tuacheni ramli chonganishi: Tusihukumu tusije tukahukumiwa. Karma ndio pekee hutoa hukumu ya haki hapa duniani!

Pia Lissu niliisha mshauri na namshauri tena, ajifunze kunyamaza.

Kitendo cha Rais Samia kukubali kukutana na Lissu ni uthibitisho tosha wa kauli na matendo she is healing this nation.

kwenye bandiko hilo nilisema

P

Umeandika

Ametaja Kikosi kazi kinachojumuisha Polisi, JWTZ na TISS,, hawa ni askari wetu, trained, how could they do such a messy dirty job?.

Mbona huku Zanzibar hao ndio vinara wa machafu mengi tu toka 1964 au unatafuta mlo kwa mama ??
 
Huyu bwana ni mlalamikaji wa kiwango cha PHD. Kama Rais kafunga safari mpaka Belgium na akataka waonane, ni lazima nia yake iwe ni njema.

Akumbuke kuwa rais ni taasisi yenye watu wengi nyuma wenye majukumu mbalimbali. Hivyo aondoe wasiwasi aliokuwa nao.

Kufariki kwa JPM kumaifanya taasisi ya urais iwe na mabadiliko makubwa. Aondoe shaka.
Nakubaliana kwa kiasi fulani na hoja hii.
Lisu kaketi na kuongea na mama Samia huko Ubelgiji.
Anayosema Lisu hawakuyaongea?
Kama sivyo waliongea nini haswa!
Body language ya mkutano ule ni kwamba wasiojulikana sasa hawapo na waliondoka na mtangulizi wa mama Samia.
Na experience ya mwaka huu mmoja imedhihirisha hili.
Nia ya Lisu , aidha ni political capital juu ya suala lenyewe-kitu ambacho kina ukakasi, au Lisu anataka waliohusika wapelekwe mahakamani, suala ambalo ni vema likafanyika ingalau gumu kulitekeleza.
 
Kuna watu hamjaelewa hitaji lake. Kwani waliotaka kumuua mchana kuepo walishindwa nini kumkamata na kumpeleka mahakamani instead wakaamua watekeleze Unyama ule?..kwanini hawajakamatwa mpaka leo,kwanin Pamoja na haya yote bado hawakuona huruma Spika akamua kunyongelea mbali ubunge wake na stahkki zake? Kuna watu wenye mbongo ndogo hawataki kufikiri hata kidgo. Wanadhani watu ni wajinga!
Keshaeleweka

Tatizo Hana jipya…. Ni hoja hiyohiyo tuuuuu

Hata akiulizwa swali la uzazi wa mpango, ataingiza joja za kipilimba, posho zake, usalama wake na kudhani mama Samia hataki kuachana na na ya magu

Na kuhusu idadi ya 400 people waliokufa, nadhani kuna changamoto pale - hivi wale jamaa waliokimbilia Delgado bila mkono wa chuma tungewezA kuwakimbuza?
 
Alianza na JPM ndio katuma watu kumuua... sasa hivi karukia kwa Kipilimba baadae atahamia kwa Samia.... ndio huwa namwona Samia mama yetu ni kiazi tu kuwapa waha kenge open room ...anajitia mama maridhiano hata kwa mambo ya kijinga.
 
Sijawahi amini kama jamaa alikuwa mchungaji kweli. Siamini na sintaamini. Bila shaka alikuwa akichunga kundi la tiss
Mtu amejitolea uhai wake kuwalindeni ninyi na maslahi yenu, tena kwauaminifu wote, leo mnamtuhumu, hivi mnachokifanya mnakifahamu?

Mnaungana na maadui wa taifa ambao wameshindwa kulinda matamanio yao kuwavunja moyo watu ambao wapo macho masaa yote for 60 years nchi ikawa kama ilivyo?

Mungu na akawalaani ninyi kizazi chenu na wenye haiba kama zenu nyote; mipango yenu miovu ikavurugike na kusambaratika, mkawe aibu mbele ya mataifa na watanzania kwa umoja wao wakawakatae na kuwazodoa. I declare and decree in the name of the most high God, Jesus Christ of Nazareth; Mungu ambaye yeye amemtumikia kwa uaminifu wake wote. Na sasa ikadhihirike wazi kati yake na ninyi nani ni wa upande wa usaliti kwa taifa lake, Amen!
 
Keshaeleweka

Tatizo Hana jipya…. Ni hoja hiyohiyo tuuuuu

Hata akiulizwa swali la uzazi wa mpango, ataingiza joja za kipilimba, posho zake, usalama wake na kudhani mama Samia hataki kuachana na na ya magu

Na kuhusu idadi ya 400 people waliokufa, nadhani kuna changamoto pale - hivi wale jamaa waliokimbilia Delgado bila mkono wa chuma tungewezA kuwakimbuza?
Bila shaka na yeye ndiye mshirika wao
 
Usalama wa Taifa kazi zao ni zipi? KUVAA MASHATI YA CCM TU? Wajitokeze sasa na kutueleza ni akina nani walipiga risasi Lissu.
Si bosi wenu lissu ameshawataja au nayeye hamna uhakika naye!!??
 
Ni jambo la kawaida kwa kila raia mwenye mashaka na usalama wake kutoa taarifa na kuhakikishiwa ulinzi kwa mujibu wa sheria.

Kuna ugumu gani kwa Mama Samia kama mkuu wa vyombo vya ulinzi na usalama kumhakikishia mhanga huyu usalama wake kwa mujibu wa sheria?
Mama Samia hayupo kuhangaika na mtu mmoja, yeye kama Rais wa Nchi alishasema Nchi iko salama na ni mahali salama kwa Watanzania wote kuishi kwa amani, nini cha ziada akiongee?
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Alianza na JPM ndio katuma watu kumuua... sasa hivi karukia kwa Kipilimba baadae atahamia kwa Samia.... ndio huwa namwona Samia mama yetu ni kiazi tu kuwapa waha kenge open room ...anajitia mama maridhiano hata kwa mambo ya kijinga.
Nakubaliana na wewe except hilo la kumkashifu Rais. Kama yeye ni kiazi watanzania waliomwamini ni viazi zaidi yake...
 
We jamaa bana, we mwenyewe ukipewa pesa za serikali za mradi unazila, sasa unazungumzia mafao ya mtu afanye nayo charity? Unafikiria kweli ama umekalia waya unaopeleka network kwenye ubongo?

Na wewe ukistaafu utafanya charity?
Ila binadamu wa siku hizi siasa imewafanya muwe na chuki sana

Ninachojua hao unaowaita wenye roho
nzuri mrabaha wa kubadili gia angani umewatokea puani. Lissu alichangiwa matibabu hana budi kurudisha fedha za stahiki yake ya matibabu anayo dai Bunge kwenye charity ili zisaidie wahanga wengine wa maandamano walioko cdm na wasio na watu wa kuwasemea ili wasaidiwe. Kama hiyo huko kwenu ndio mnaita chuki nakupa pole nyingi sana.
 
Huyu kipilimba anatajwa katika uovu mwingi sana nchi hii, ni wakati wa nae kushughulikiwa atambue kuwa kila anaeua kwa upanga nae atakufa kwa upanga
 
Kwa maoni yangu, Tundu Lissu anahitaji ushauri nasaha. Binadamu ukipitia maswahibu na mapito kama aliyopitia, unaathirika ki fizikia, ki emosheni na kisaikolojia, (physical, emotional and psychological), hivyo anahitaji ushauri nasaha jinsi ya kutoka kwenye jinamizi hili na kuendelea na maisha.

Huku kutaja taja majina ya watu, na kutangazia ulimwengu kuwa vyombo vyetu tukuka vya ulinzi na usalama kuwa ndio walio husika, shambulio lake, bila ushahidi wowote, ni kuzidi kuibagaza tuu nchi yetu!.

Ametaja Kikosi kazi kinachojumuisha Polisi, JWTZ na TISS,, hawa ni askari wetu, trained, how could they do such a messy dirty job?. Kwa trained snipers, only one single shot would have finished the job!. Hili hata Mama Samia amewahi kuizungumzia, askari wetu trained wakimiss target by two shots, wanaandika maelezo kujieleza!.

Mimi kwa upande wangu naendelea kusisitiza Tuacheni ramli chonganishi: Tusihukumu tusije tukahukumiwa. Karma ndio pekee hutoa hukumu ya haki hapa duniani!

Pia Lissu niliisha mshauri na namshauri tena, ajifunze kunyamaza.

Kitendo cha Rais Samia kukubali kukutana na Lissu ni uthibitisho tosha wa kauli na matendo she is healing this nation.

kwenye bandiko hilo nilisema

P

Karma unayoongelea, waswahilihuita "Dua la kuku." Kama sisi kama nchi tutegemee, kwanini basi magereza yasifunguliwe, mahakama zikifutwa, na polisi na majeshi vikawa abolished tukaiachia karma kuchukua mkondo wake?

Kwamba aliyopitia Lissu ni mazito na hayapaswi kubagazwa? Labda huo ndiyo uliopaswa kuwa msingi wa hoja yako vinginevyo unabakia kuwa ukakasi mtupu.

Kwamba risasi ngapi zingehitajika? Kwani kwa Hamza au Kombe walitumia ngapi?

Tuachane na wazungu wa nani hii hawa mjomba:

Hawa waliamuru Lissu kuuwawa. Yumkini amri hiyo ingalipo. Lissu anahitajika kuhakikishiwa kama amri hiyo haipo tena.

Kwani Charles Snowden anaweza rejea Marekani bila hakikisho la usalama wake?
 
Back
Top Bottom