Ubaya Ubwela
JF-Expert Member
- Jul 24, 2024
- 1,353
- 3,060
Enyi watu wabaya mjulikanao kama 'watu wasiojulikana,' nimezisikia njama zenu. Mnataka kuniumiza halafu mumsingizie Mwenyekiti wetu wa chama, Freeman Mbowe.
Ndivyo mlivyofanya wakati wa kifo cha marehemu Chacha Wangwe. Ndivyo mlivyofanya tena wakati mliponishambulia tarehe 7 Sept '17. Na ndivyo mlivyofanya miezi michache iliyopita mlipomteka nyara na kumuua Mzee Ali Mohamed Kibao.
Ndivyo mnavyofanya kila mnapoua watu wasio na hatia. Mnasingizia watu wengine ili nyie mnaohusika msiwajibike na udhalimu wenu.
Huyo mnayedhani mnamtumikia alitoa ahadi hadharani kuwa nitakuwa salama nikirudi nyumbani. Waziri wake Masauni alirudia ahadi hiyo bungeni.
Mkiniumiza kama mnavyopanga mjue lawama yote itaangukia kwa Samia Suluhu Hassan. Badala ya kumlinda mtamchafua zaidi. Na kama ilivyokuwa kwa Magufuli baada ya 7 Sept '17, ndivyo itakavyokuwa kwa Samia.