Vishu Mtata
JF-Expert Member
- Dec 15, 2019
- 15,954
- 35,415
Maamuzi yanatolewa kulingana na comments za instagram.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mtumishi wa serikali hafukuzwi kipuuzi hivyo kama unavyofikiri. Kuna sheria nyingi zinamlinda. Alichokisema huyo Waziri, ni kuwavua vyeo vyao vya ualimu mkuu. Na hivyo watabakia kuwa walimu wa kawaida tu.Kama kweli wamefanya huo ujinga,ni lazima wafukuzwe kazi hakuna jinsi!!!
Tena mtimueeDah nikikuta mwanangu anaimba hizi nyimbo za mtoto zuchu kiasi flan itanipa huzun maana si ngazi yake
Kwanini waliuruhusu uchezwe Redio I?Wimbo wa kukata viuno, siyo nzuri ni ku inculcate sense ya "ngono" kwa watoto
KUna zile nyimbo za utamaduni mashuleni kukata viuno unaongeleaje piakwahiyo ushenzi huo uhalalishwe mashuleni? kwani USWAZI kuna maadili? ndiyo maana kukaitwa uswahili, uncivilized society.... ni derogatory term kwa watu wa huko USWAZI...
Kuna ndugu zangu hawapigi nyimbo za kidunia nyumbani kwao, lakini nimeshangaa watoto wao wanaimba hizi nyimbo za kina zuchu mwanzo mwisho loh. Watoto wala hawawazi mnayoyawaza nyie.Wanasiasa ni watu wapumbavu sana, maamuzi ya kukurupuka kujipendekeza na uchawa tu vichwa vyao vinawaza kusifiwa na kujikomba komba kwa mamlaka hivyo anatafutwa mnyonge na mnyonge siku zote ni mwalimu,
Waanzie majumbani wawavue vyeo wazazi na walezi hizo nyimbo hazipigwi wala kusikilizwa shuleni ila wanafunzi wanazijua.
walimu walizingua, na nyimbo pia inatakiwa kufungiwa.Waziri husika huyo ni nani!?
Hao Walimu wamefanya kosa gani!??
Ahhh!!!
shida ni content za hiyo nyimboKUna zile nyimbo za utamaduni mashuleni kukata viuno unaongeleaje pia
Kilichomuudhi Waziri ni watoto kutamka maneno "baby my sweet wangu etc"Hapa nakataa nilichokiona ni burudani Tena wote walimu na wanafunzi wanainjoy mziki. Kwani kucheza mziki na kuburudika ni kosa!? Kama siyo mziki unafikri ni kipi kingewaburudisha hao wanafunzi kiasi hicho!?
Na kwani huo mziki una kitu Gani au maneno yapi ya kusema ya haribu watoto!? Kwangu ni "BIG NO" wameonewa walimu, nilitegemea wapongezwe kwa ubunifu wa kupiga mziki watoto wanapenda.
Sio kwenye sherehe tu. Sie tuliosoma boarding tulikuwa na muziki na wanaalikwa boys kutoka shule mbalimbali tunacheza pamoja na kufurahi. Miziki ya kila aina ilikuwa inapigwa.Aliyewasimamisha kazi atakuwa ni mpumbavu.
Huyu Zuchu si juzi kaalikwa Geita kwenye ziara za CCM akatumbuize!
Si ndio nyimbo hizo alikuwa anaimba?
Shule miziki kama hii kwenye sherehe ni kawaida..na ilianza Toka enzi za Mwalimu,la Saba wanapomaliza mitihani huwa kunaambatana na sherehe na miziki..
Labda kama huyo waziri na CCM wao walisoma Burundi.
Waache upumbavu.
Watoto mtaani wanacheza hii nyimbo sana maana imekaa kitoto .
Kama wapo serious basi wangeifungia ama waanze kuwaadhibu wote wanaoicheza..ambapo wataadhibu watoto wote sasa..hakuna mtoto hajui hiyo..tunajionea mtaani huku.
Hebu jiulize hao watoto wamejifunzia wapi huo wimbo na wanajua kucheza na kuimba. Watoto wengi wanaujua huo wimbo na wanaucheza.Hivi Watanzania akili tumemkopesha nani siku hizi? Huo wimbo una maadili gani ya kumfundisha mtoto? Umeyasilikiliza vizuri hayo maneno yanayotamkwa kwenye huo wimbo? Tunatetea vitu vya kijingaa
Mamlaka ndio zinatakiwa zi control hizi nyimbo maana kwa wazazi inakuwa ngumu. Wanajifunza mashuleni etc. Kila kona hii miziki inapigwa hovyo, kwenye pikipiki, baa , daladala etc. Watoto watazijua tu hata ukikataza kwako.Nchi hii sasa hivi tuna mizazi ya hovyo hovyo sana! Hii ndiyo inaona hata watoto kuwa mashoga ni sawa tu maana ndio usasa huo!
Mkenda ni great thinker kwenye taaluma yake, kwenye siasa ni kiazi kabisa.Nina wasiwasi na maamuzi ya prof.. kashinikizwaa bila ku think twice..ahah hapana prof tunamjua ye ni great thinker..natumaini angepata muda wa kutafakari angepuuza..cz alichokifanya ni kuziba tundu la panya kwa mkate.. kama kweli alinaanisha basi karuka process za kutatua tatizo.. Ambazo wao wametufundisha kwenye research. Asante kwa taarifa pia nawakumbu Elimu ya msingi mwsho darasa la sita kuanzia 2027.
Kwa hiyo kwa sababu mna sheria nyingi zinazo walinda ndiyo maana mnaona kufanya ujinga wenu ni halali kabisa!!?? Ebu tafakari kama mtu mzima kwanza! Hapa waziri anagusia kuhusu swala zima la malezi kwa watoto wetu!!Mtumishi wa serikali hafukuzwi kipuuzi hivyo kama unavyofikiri. Kuna sheria nyingi zinamlinda. Alichokisema huyo Waziri, ni kuwavua vyeo vyao vya ualimu mkuu. Na hivyo watabakia kuwa walimu wa kawaida tu.