Tunduma: Wakuu wa shule wavuliwa nyadhifa kisa wimbo wa Zuchu (Honey)

Tunduma: Wakuu wa shule wavuliwa nyadhifa kisa wimbo wa Zuchu (Honey)

Kizazi Cha Sasa ni Cha nyoka. Waziri angeacha watu wajifanyie wanavyo taka. Maana Kuna kipindi BASATA walikuwa walifungia nyimbo watu wanawaijia juu. Pia sio kwa ubaya, kwanini wasanii watu wanapenda kuimba matusi na mambo ya chumbani?. Mbona akina Prof J, Mr Two, Wagosi wa kaya waliwika Sana bila kuimba matusi. Leo nyimbo zote zinafanana na hakuna ubunifu.
Na serikali hiyohiyo itaandaa tuzo kuwazawadia akina Zuchu[emoji23]
 
Leo nimeona video ya wimbo wa Whozu ft Billnass na Mbosso unaitwa Umeyatimba,
Kipande anachoimba Mbosso kuna sehemu anasema "Nyoooo na Nyokoooo", pia ile video inaonesha anambaka Mwanamke chumbani huku Wanaume wapo sitting room wanashangilia, anampaka hadi mafuta ya nazi....

Nimeshindwa kuelewa mamlaka husika hawajaona haya lakini na hawa wasanii kwanini wanafanya hivi, lengo lao hasa ni nini kutoa nyimbo za namna hii huku wakijua wahanga wakubwa ni watoto na vijana wadogo!??
Wasafini mawakala wa shetani pumbafu zao
 
Kwa kweli watoto wadogo tena wengine hata chekechea hawajaanza huimba nyimbo za wasanii zinazo trend. Basata walizembea kuacha kuupiga ban wimbo huo uliojaa mapenzi waziwazi. Kingine ni hao show maker wanapoenda kutoa misaada mashuleni wawe wanachagua nyimbo za heshima zisizochochea mapenzi waziwazi wala kutukuza ulevi na uhuni
Mbona asilimia kubwa ya nyimbo za bongo fleva zinaongelea mapenzi?
 
Hongera sana mh Waziri tusiruhusu watoto wetu wakachezeshwa Huo upupu wa Zuchu Bora ingepigwa reggae wimbo mmoja wa Bob Marley au Lucky Dude.
Kwa hiyo hizo nyimbo wanajifunza shuleni?
Kama hazifai kwa nini hazikufungiwa?
 
BASATA kazi wanayo

Nguvu wanayotumia kubana miziki

Ya kina nay,roma watumie kubana pia miziki inayozungumzia na kusupport ushg,kuf713 kunyanduana

Ova
 
Vitoto vya kiyao tena asili tu kunyanduuana na mnawaongezea
Na mambo ya zuchu tena

Ova
 
Mbona asilimia kubwa ya nyimbo za bongo fleva zinaongelea mapenzi?
ni kweli, kuna lebo nne za wasanii wanaowika sana miaka hii zote zina wasanii wengi na kila msani albam yake yote imejaa mapenzi tu, mambo ya kutongozana. Bongo fleva ya mwanzo nyimbo za mapenzi zilikuwa chache sana na mapenzi yenyewe ilikuwa ni kusifia au kuonya mpenzi mkorofi. Wasanii wa zamani walikuwa na mada nyingi za kuimba, wengine walisifia mageto yao kuwa ni mazuri, waengine walisifia mavazi, ugali, umasikini, mila na utamaduni wa makabila yao, wengine waliungana wakasifia mikoa yao wanakotoka. Na video zao hazikuwa na mamodo wanaovaa nusu uchi
 
View attachment 2801642

Baada ya kipande cha video kinachowaonesha watoto wa shule za msingi wakicheza wimbo wa msanii Zuchu ‘Honey’ wilayani Tunduma kusambaa mitandaoni, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda ameagiza walimu wakuu wawili wa shule hizo wavuliwe vyeo.

Amesema hayo nje ya Bunge jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu video hiyo ambapo pia amepiga marufuku wanafunzi kucheza nyimbo zisizo na maadili na kuwataka walimu kuwa wasimamizi wa maadili pindi wanafunzi wawapo shuleni.

“Tumeshatambua shule yenyewe iko Tunduma, kulikuwa na kikundi kimeenda kutoa msaada shuleni pale, baada ya kutoa msaada ule kikaweka na muziki halafu wanafunzi wakacheza, na maudhui ya muziki wenyewe kila mtu ameusikia sina haja ya kuurudia,” amesema Profesa Mkenda.

Ameongeza, “tumeongea na wadhibiti ubora wapeleke taarifa kule, mkurugenzi awaondoe walimu wakuu wa shule mbili; moja shule ya Tunduma na nyingine ambazo ni kama shule pacha, waondolewe madaraka ya ukuu wa shule watafutwe wakuu wengine wa shule. Tunafanya hivi ili kutuma ujumbe, walimu wakuu tusaidieni msiruhusu vitu kama hivi viingie mashuleni.”

Kwa upande wake Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima amempongeza Profesa Mkenda kwa kukemea kitendo hicho na kutoa wito kwa watoa huduma wote na wanaohudumia watoto kusimamia malezi na makuzi ya watoto.
Haya wengine Hawa Huku🤣
 
Attachments

  • IMG_3521.MP4
    3.7 MB
Sasa walimu wataweza vipi kuzuia tabia binafsi za watoto walizozitoa kwao.

Viongozi wapumbavu ndio kama hawa.
 
Leo nimeona video ya wimbo wa Whozu ft Billnass na Mbosso unaitwa Umeyatimba,
Kipande anachoimba Mbosso kuna sehemu anasema "Nyoooo na Nyokoooo", pia ile video inaonesha anambaka Mwanamke chumbani huku Wanaume wapo sitting room wanashangilia, anampaka hadi mafuta ya nazi....

Nimeshindwa kuelewa mamlaka husika hawajaona haya lakini na hawa wasanii kwanini wanafanya hivi, lengo lao hasa ni nini kutoa nyimbo za namna hii huku wakijua wahanga wakubwa ni watoto na vijana wadogo!??
Washapigwa chuma.
 
Attachments

  • Screenshot_20231106_164600_Chrome.jpg
    Screenshot_20231106_164600_Chrome.jpg
    153.3 KB · Views: 3
Leo nimeona video ya wimbo wa Whozu ft Billnass na Mbosso unaitwa Umeyatimba,
Kipande anachoimba Mbosso kuna sehemu anasema "Nyoooo na Nyokoooo", pia ile video inaonesha anambaka Mwanamke chumbani huku Wanaume wapo sitting room wanashangilia, anampaka hadi mafuta ya nazi....

Nimeshindwa kuelewa mamlaka husika hawajaona haya lakini na hawa wasanii kwanini wanafanya hivi, lengo lao hasa ni nini kutoa nyimbo za namna hii huku wakijua wahanga wakubwa ni watoto na vijana wadogo!??
We are living in a Failed State
 
Mmh najaribu kutafakari na kuona kosa la walimu mpaka kuvuliwa nyadhifa zao sioni.

Tujiulize haya!

1.Je kosa ni kurekodiwa na kuwekwa katika social media au

2. Mziki kupigwa maeneo ya shule na watoto kucheza.

3. Je ingekuwa siku ya mahafali ya Darasa la saba na wimbo huo ukapigwa na wanafunzi wakaucheza je mwalimu angevuliwa nyadhifa yake?

Kiukweli tunakemea mmomonyoko wa maadili katika jamii yetu lakini mpaka wimbo umepita basata walichuja wapi na kuona utatumika kwaajili ya wakubwa tu na watoto hawata sikiza wimbo huo?

Watoto wanavyoimba inaonesha wanaujua wimbo tangu awali, this means kwamba kwa siku hiyo tu mwalimu mkuu hajasababisha mmomonyoko wa maadili kwa wanafunzi.

Kumvua cheo mwalimu mkuu ni Kuiambia BASATA kuwa walikosea kuruhusu wimbo huo.
Kwa maoni yangu mwalimu mkuu hana makosa ya kumvua cheo chake.

Yani Kiukweli mawaziri hukurupuka sana katika maamuzi, sijui ni poor kantiri ndo maana na mindset zetu zipo kama hali yetu ya uchumi.

Honeeey.
Hoooney
 
Back
Top Bottom