Tunduma: Wakuu wa shule wavuliwa nyadhifa kisa wimbo wa Zuchu (Honey)

Tunduma: Wakuu wa shule wavuliwa nyadhifa kisa wimbo wa Zuchu (Honey)

Sijui labda macho yashakuwa ya uzee tena.... lakini sijaona kosa hapo la kufikia wakuu wa shule kuvuliwa vyeo tena ikiwa mari kutoka kwa waziri 🙁
Tena walimu wenyewe wanacheza kawaida tu

Hata watoto wanaonyesha kufurahia

Itakuwa mkenda mawazo yake machafu anadhani kila mtu anayo.
 
Wimbo kukosa maadili ni akili yako msikilizaji unawaza nini, Sion tatizo na wimbo wa Zuchu huo Honey kwa maana sada hivi watoto wanajua mpaka kondomu, viongiozi wanaongea kondomu hadharani kwenye mikutano na hata katika televisheni neno kondomu ni kawaida sasa mtu kuimba Honey inakuwaje sio maadili. Ni sawa na ule wimbo wa Maua sama, kaimba SITAKI KIBAMIA MWANAUME MASHINE ila kwa kuwa BASATA imejaa wahuni ndio wakafsiri yale ni matusi lakini katika lugha fasaha au lugha ya kila siku una uwezo wa kusema neno KIBAMIA na hamna atakaekusitaki tofauti na ukisema neno ambalo ni tusi kama MNGESE au MAKU na mengine. So mi naona tatizo la akili chafu ndio chanzo tunaona nyimbo hazina maadili.

Na kwanini upeleke watu kwenye tafsiri?. Kwani huwezi kuimba vitu vya kueleweka?
 
Huyohuyo Zuchu unayemwita Malaya
Alialikwa na hao hao mawaziri,mwezi uliopita huko Geita,
Akaenda kuimba huo huo upuuzi wa honey, na upuuzi mwingine wa kwikwikwi sijui sugar sukari,,huku akiwakatia mauno na wakamshangilia.


Kama kweli wanataka kukomesha huu upuuzi,waanze wao kujitumbua ,waachie ngazi,
Ndio waje kutumbua walimu.

Na bado anapeta tu kwenye tasnia
Hakuna kitu wamemfanya.

Viongozi wanazingua.
 
Kizazi Cha Sasa ni Cha nyoka. Waziri angeacha watu wajifanyie wanavyo taka. Maana Kuna kipindi BASATA walikuwa walifungia nyimbo watu wanawaijia juu. Pia sio kwa ubaya, kwanini wasanii watu wanapenda kuimba matusi na mambo ya chumbani?. Mbona akina Prof J, Mr Two, Wagosi wa kaya waliwika Sana bila kuimba matusi. Leo nyimbo zote zinafanana na hakuna ubunifu.
 
Sijui ni mazingira ya eneo husika au laah! Binafsi huwa sipendi na huwa sifuatilii nyimbo za bongo fleva kwa sasa mimi ni mpenzi wa bongo fleva mongwe na zilipendwa za akina TX Moshi. Ila kwa kuwa dunia imebadilika muziki kwa sasa ni biashara na kuna mpango wa kuanzisha masomo ya amali mashuleni ambayo pia yatachukua na huo muziki, sijajua huo muziki utakao takiwa kufundishwa utazingitia soko la sasa la dunia au laah!
 
Tunaviongozi wavivu wenye fikra duni wanashughurika na matokeo badala ya kudeal na chanzo cha matatizo.

Wimbo umeshatoka na unapigwa kila sehemu hakuna tamko la kukataza wimbo leo unamvua mtu cheo kisa wimbo WFK

Hili Taifa sijui lina watu wa aina gani.
Atiiii... WTF
 
Naunga mkono waziri, kama ingekuwa ni shule yangu binafsi hao walimu nafukuza kazi. Lazima utofautishe nyimbo za shuleni zenye maadili na zile za kihuni
 
Mh waziri yupo sahihi , mtoto ukimpasua ubongo na Akili ni gharama kubwa kumrejesha katika reli .

Natamani Wcb wajitafakari Sana pia wazazi na walimu ipo sababu ya kuacha ubinafsi na kuwa na utu , UPENDO na moyo wa Huruma kuhusu hiki kizazi ili kisipotee mazima.

Nipo temeke niseme watoto wanapotea kwa kasi kubwa Sana .😒🤢
 
Badala ya kufungui miziki ya hovyo unawvua nyadhifa walimu
 
Kosa la Walimu lipo wapi?

Nimesikiliza, watoto wanajua kila neno na mistari ya wimbo tena kwa kufuata midundo.
Wanaimba kwa pamoja bila kukosea, na wanacheza kwa mirindimo sawia

Watoto walijua huu wimbo kutoka majumbani kwao. Hao wazazi wanaolalamika walikuwa wapi?

Kilichotokea hakina uhusiano na Walimu, kinatuonyesha ubovu wa malezi majumbani kwetu! tuanzie huko

JokaKuu Pascal Mayalla
 
Leo nimeona video ya wimbo wa Whozu ft Billnass na Mbosso unaitwa Umeyatimba,
Kipande anachoimba Mbosso kuna sehemu anasema "Nyoooo na Nyokoooo", pia ile video inaonesha anambaka Mwanamke chumbani huku Wanaume wapo sitting room wanashangilia, anampaka hadi mafuta ya nazi....

Nimeshindwa kuelewa mamlaka husika hawajaona haya lakini na hawa wasanii kwanini wanafanya hivi, lengo lao hasa ni nini kutoa nyimbo za namna hii huku wakijua wahanga wakubwa ni watoto na vijana wadogo!??
Hizo hazina shida,kuimba matatizo ya jamii ndiyo mbaya.
 
Back
Top Bottom