Tunduma: Wakuu wa shule wavuliwa nyadhifa kisa wimbo wa Zuchu (Honey)

Kama kweli wamefanya huo ujinga,ni lazima wafukuzwe kazi hakuna jinsi!!!
Mtumishi wa serikali hafukuzwi kipuuzi hivyo kama unavyofikiri. Kuna sheria nyingi zinamlinda. Alichokisema huyo Waziri, ni kuwavua vyeo vyao vya ualimu mkuu. Na hivyo watabakia kuwa walimu wa kawaida tu.
 
kwahiyo ushenzi huo uhalalishwe mashuleni? kwani USWAZI kuna maadili? ndiyo maana kukaitwa uswahili, uncivilized society.... ni derogatory term kwa watu wa huko USWAZI...
KUna zile nyimbo za utamaduni mashuleni kukata viuno unaongeleaje pia
 
Kuna ndugu zangu hawapigi nyimbo za kidunia nyumbani kwao, lakini nimeshangaa watoto wao wanaimba hizi nyimbo za kina zuchu mwanzo mwisho loh. Watoto wala hawawazi mnayoyawaza nyie.
 
Kilichomuudhi Waziri ni watoto kutamka maneno "baby my sweet wangu etc"
 
Sio kwenye sherehe tu. Sie tuliosoma boarding tulikuwa na muziki na wanaalikwa boys kutoka shule mbalimbali tunacheza pamoja na kufurahi. Miziki ya kila aina ilikuwa inapigwa.
 
Hivi Watanzania akili tumemkopesha nani siku hizi? Huo wimbo una maadili gani ya kumfundisha mtoto? Umeyasilikiliza vizuri hayo maneno yanayotamkwa kwenye huo wimbo? Tunatetea vitu vya kijingaa
Hebu jiulize hao watoto wamejifunzia wapi huo wimbo na wanajua kucheza na kuimba. Watoto wengi wanaujua huo wimbo na wanaucheza.
 
Hizo nyimbo ndizo wazazi wao wanawawekea, upo pia wimbo unaitwa bia ni tamu, mwingine sijui nini na huyo basha wako, yaani watoto wanapata makuzi magumu.

Hao waalim 😎😎
 
Nchi hii sasa hivi tuna mizazi ya hovyo hovyo sana! Hii ndiyo inaona hata watoto kuwa mashoga ni sawa tu maana ndio usasa huo!
Mamlaka ndio zinatakiwa zi control hizi nyimbo maana kwa wazazi inakuwa ngumu. Wanajifunza mashuleni etc. Kila kona hii miziki inapigwa hovyo, kwenye pikipiki, baa , daladala etc. Watoto watazijua tu hata ukikataza kwako.
 
Mkenda ni great thinker kwenye taaluma yake, kwenye siasa ni kiazi kabisa.
Jimboni kwake huko Moshi hamna kitu, yaani hata balozi wa nyumba kumu anamzidi.
Hajui siasa, hajui vipaumbele tangu awe mbunge ameweza kuanzisha mkenda Cup ambapo ni takrima kwa kila mbunge wa CCM.
 
Mtumishi wa serikali hafukuzwi kipuuzi hivyo kama unavyofikiri. Kuna sheria nyingi zinamlinda. Alichokisema huyo Waziri, ni kuwavua vyeo vyao vya ualimu mkuu. Na hivyo watabakia kuwa walimu wa kawaida tu.
Kwa hiyo kwa sababu mna sheria nyingi zinazo walinda ndiyo maana mnaona kufanya ujinga wenu ni halali kabisa!!?? Ebu tafakari kama mtu mzima kwanza! Hapa waziri anagusia kuhusu swala zima la malezi kwa watoto wetu!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…