Tupeana updates za kuhama kwa Wamachinga
Mtu yoyote anayetetea namna machinga wa magufuli walivyokuwa wanafanya kazi nashindwa kumuelewa. Mimi Kariakoo hawa jamaa walipasua kipasso changu kisa, wako barabarani na mm ndio wakawa wanataka niwapishe. Ni bahati mbaya kwamba sikuwa na pa kuwapishia na hivyo nikaishia kuadhibiwa bila sababu. Kila jambo linahitaji kuwa na utaratibu, bila hivyo ni fujo tupu. Na machinga wetu walikuwa wanafanya fujo kila mahali. Serikali ya mama iungwe mkono kwenye hili, machinga wapelekwe sehemu sahihi kwa ajili ya biashara na sio kuharibu sehemu za huduma nyingine.
Machinga ni moja ya njia ya kufikisha huduma na bidhaa hasa kwa watu wa kipato cha chini kwa urahisi, haraka na nafuu. Serikali inashindwa ku strategise namna ya kukusanya kodi zitokanazo na bidhaa na huduma wanaenda kuhangaika na machinga wakifikiri ndo wanakwamisha wao kukusanya kodi ya kutosha kutoka kwa wafanyabiashara.

Kimsingi wafanyabiashara wa kiafrika ni wakwepaji wakubwa wa kodi ukilinganisha na wazungu na kuthibiti wamachinga siyo suluhisho la wao kutoendelea kukwepa kodi.

Serikali inatakiwa kubuni njia mbadala za kukusanya kodi kwenye bidhaa na huduma, badala ya kuingilia mifumo ya ufanyaji biashara unaolenga kuwakandamiza wafanyabiashara ndogo ndogo, waliobandikwa jina la wamachinga ambao kimsingi ndo wanasaidia kundi kubwa la watu wa kipato cha chini na kati na kuishia kuwalinda maslahi ya wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa.
 
Muhimu waelekeze juhudi kubwa kusafisha masoko kama Tandika, Tandale,ilala Boma, Mwenge, Temeke fukwe zote kama magogoni, kawe, oysterbay.

Masoko inabidi yapangwe upya na yawe na miundombinu ya kutosha ya vyoo na visafi, sehemu za kuweka uchafu, (Dustbins) miundombinu ya kuchukua maji taka na maji ya mvua, meza, nafasi za kutosha kwenye njia za kupita watembea miguu ndani ya soko, roof, sakafu za cement / zege, parking za kutosha, na taa/mwanga wa kutosha etc.

Muhimu sana wahakikishe wafanyabiashara wote wanaendelea kupata sehemu zao za kuuza zilizo safi, salama kwa kila mtu anayetembelea soko.

Wawekeze pia kuwa na bustani njingi mjini, na kupanda miti, majani, maua katikati ya barabara kubwa na pembezoni ya barabara zote.
Lakini pia tusiwe na fikra kwamba kila kijana awe mchuuzi/machinga.
 
KUMEKUCHA, Nasikia dar imefanyiwa usafi ndani ya usiku mmoja na hawa vijana, watu wameamka asubuhi hawaamini wanachokiona ,sehemu ambayo ilikua haipitiki saivi unapita bila kugusana.

vibanda vyote vimevunjwa hivi vya service road sasa ufanyike usafi wa kwenda jiji liwe safi zaidi

kumbe inawezekana aisee khaa Suma jkt sio wa mchezo mchezo, waendelee kupewa tenda hawa vijana
Wewe Umesikia tu, sie tunataka picha tuthibitishe.
 
Back
Top Bottom