Tusichukulie Kirahisi, Rais Samia anaweza kufika Mahakamani kuwa prove wrong. Hivyo Lissu ajiandae kisawasawa

Tayari huko mawakili wa serikali ya hovyo wameanza kumkingia kifua asiende mahakamani! wakijua kabisa akienda atakaangwa vibaya, unafikiri lisu muoga muoga?
Je kama atafika kesi itaendaje?
 
duh sasa hakujua haya bwana lisu ?
Anajua na alijua..

Lakini ziko sababu ya kufanya hivi...

1. Ni kuweka precedence au kumbukumbu kuwa "Rais aliitwaga lakini akaogopa kutokea mahakamani"

2. Ni kuonesha udhaifu wa mfumo wetu wa utoaji haki (mahakama), wa sheria na wa kikatiba

3. Yeye na serikali yake yote ndiye alitishiwa kuuwawa/kupinduliwa na TL!

Ni lazima waje Ili wadodoswe, how exactly walitishiwa?

Kwa ishu ya kutoa ushahidi au kutotoa, soma maelezo hayo mpaka mwisho..

"Kwa hiari yake" anaweza kutoa ushahidi wake kwa maandishi pasipo kusimama kizimbani au kwa "njia zingine" labda ikiwemo kuwakilishwa only if sheria inaruhusu..

Lakini kama anaheshimu sheria kweli, atatokea..
 
Kwani Mahakama imesemaje leo,Lissu ana kesi ya kujibu au hana?
 
Jibu la Hoja

Nakubaliana kwamba Lissu hapaswi kutegemea kutofika kwa mashahidi kama njia ya ushindi. Mahakama ni sehemu ya ushahidi na hoja, hivyo kila upande unatakiwa kujiandaa kwa lolote.

Lakini pia tusihitimishe mapema kwamba Rais Samia atafika mahakamani au kwamba ushahidi fulani tayari unaelekea upande mmoja. Mwisho wa siku, mahakama itaangalia ushahidi uliowasilishwa, si hisia wala dhana za mitandaoni.

Lissu ajiandae kisawasawa, na upande wa pili nao ujiandae. Hapo ndipo ukweli na haki vitakapopata nafasi ya kuonekana.
 

Sahihi kabisa.

Ila aliyemhanga anapaswa kujiandaa zaidi. Hiyo ndio hoja yangu
 
Sio Rais tu wote aliowataja upande wa serikali hataenda hata mmoja.
 
Kama mawakili wanachemka peupeeee mpaka wanafedheheshwa tena kwa aibu na TAL basi hao mashahidi kamwe hawataweza toa utetezi wowote wa maana mbele ya TAL. Ila sema kwa kuwa judges wanaendeshwa kwa rimoti basi TAL hatopata haki yake.
Je kama hawatafika kesi itaendaje?
 
Itakuwa Maajabu ya Karne! Itaandikwa hata kwenye Guiness Book! Yaani utegemee Mama anavyomwogopa Lissu aje kutoa ushahidi mahakamani kweli?
bi kizmkaz atachafua hali ya hewa buree mahakamani kwa kihoro
 
Hapa umethibitisha uwezo wako mdogo sana wa masuala ya kisheria. Tena hata yasiyohitaji mtu kuwa na degree ya sheria mkuu. Kisheria mwenye wajibu wa kuthibisha tuhuma ni mleta mashtaka siyo mshtakiwa. Tumia hata Google kuelewa kwamba kukutwa na kesi ya kujibu ni hitaji dogo sana la kisheria. Linaitwa "probable cause". Probable cause haimaanishi kwamba umekutwa na hatia. Ni tuhuma tu - haijalishi ukubwa wa tuhuma. Umeshawahi kusikia dhana ya "you are innocent until proven guilty (hauna hatia mpaka ukutwe na hatia pasi na shaka)"? Hiyo ndiyo dhana ya kisheria inayotumika hata kwa sheria za Kitanzania.
 
Hatari sana hapo.
Lakini ili mtu awe shahidi anatakiwa kuwaje au iweje?
Awe anahusika kwenye kesi moja kwa moja huwezi tu kuita mtu yeyote ili mradi Tundu Lissu kwa sababu ni kesi dhidi ya uhaini ametumia fursa japo anajua ushaidi wao hautamsaidia kwenye utetezi wake mashidi wale wengine ndio msingi wa utetezi hawa wengine ni ku-attract public attention tu
 

Very interesting.....Nigeria ya Sani Abacha na Chief Abiola๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ