niliwahi ishi na mtoto wa cousin wangu, nikienda kazini analeta maden kwangu, wanakula na kupika msosi wote uliopo. Mungu saidia akapaa kazi serikalini, bado akataka aendelee kukaa kwangu, mimi hapo nina chumba na sebule na choo basi, yeye analala sebuleni na haoni tabu. ikapita miezi mitatu ameajiriwa na hana mpango wowote wa kununua hata kijiko, dogo ananunua pamba tu, ikitokea hata umeme umeisha na haupo nyumbani nakwambia utamkuta gizani, anapendeza hatari ila jioni ndo analalila duvet chini, aah nikaona isiwe tabu nikatafuta nyumba karibia na sehemu anayofanyia kazi, nikanunua sufuria, sahani, mwiko na jiko la mafuta kama mnayakumbuka. ilivyofika jumamosi nikamwambia naomba unisindikize sehemu, basi nikaenda kumkabidhi geto lake na ikawa mwanzo wa kujitegemea.lakini naona kuna kitu alaijifunza, baada ya yeye pia kuwa na familia watu walijazana sana kwake, akaona sio maisha anayotaka kuishi, aliwapangishia wote na kuwapa mitaji wakaanza kujitegemea. tena yeye aliwapamgaishia mbali kabia na anapoishi.