Tuwasaidie wanawake wanaotembeza matunda na watoto mgongoni

Nakutana na kundi kubwa la wanawake wakiwa wamebeba watoto wadogo wakitembeza matunda mazingira ya jua Kali sana nawaonea huruma ukikuta dada anateseka juani na mtoto fanya kama unatoa sadaka tu kwa kununua matunda yake utabarikiwa sana
Lipa kodi, kodi iende kwenye elimu na afya, hutawaona huko barabarani.
Maskini mmekuwa mitaji ya tabaka tawala, nyie mnaobeba watoto mgongoni ndio nyie mnasema mitanom tena, anatosha, alafu mnakuja huku kuomba huruma.
#kila mtu ale alipopeleka mboga.
 
ukikuta dada anateseka juani na mtoto fanya kama unatoa sadaka tu kwa kununua matunda yake utabarikiwa sana
Upo sahihi kabisa japo wengine huwa wanakataa kwa hofu kuwa ukinunua yote atakosa cha kuuza
 
mkuu,heshima yako kwanza, inahuzunisha story yako kuliko huzuni yenyewe. Hakika anaptia mateso lakini msaada wako wa kibinadam unahtajika kuliko hitaji lenyewe,sahau ya nyuma jali kumsaidia! Nasubiri mrejesho!
 
NAKAZIA 📌🔨
 
Huo ushauri mzuri sana! Kwa kweli wanatia huruma.
Kwa mfano Mimi huwa wakati mwingine naacha "chenji"!
Au wakati mwingine nanunua lakini sichukui matunda nayalipia harafu namuachia.
 
Huu sasa ni ukatili
 
Mkuu umeongea kwa hasira Sana na uchungu Ila furaha ya masikini ni watoto .

Muhimu Kama hivi wazae tu watoto wachache ambao watawamudu hii itapendeza Ila sio kwamba wasizae kabisa.
Hao wanaongeza idadi ya maskini wengine duniani na gharama za serikali kuwahudumia.

Kwa nini mtu azae halafu anajua hawezi kutoa matunzo kwa mtoto?

Wanategemea nani aje kuwalelea watoto wao?
 
Huu sasa ni ukatili
Ukatili ni kuleta kiumbe duniani kije kiteseke wakati mtu anajua kabisa yeye hana uwezo wa kuhudumia mtoto pindi atakapo zaliwa.

Watu maskini bora wakose kabisa uwezo wa kuzaa.

Ndio maana Afrika umaskini hauishi na hautakaa uishe, kwa sababu ya watu maskini kuendelea kuzaliana kuongeza idadi ya maskini wengine duniani.
 
Hao wanaongeza idadi ya maskini wengine duniani na gharama za serikali kuwahudumia.

Kwa nini mtu azae halafu anajua hawezi kutoa matunzo kwa mtoto?

Wanategemea nani aje kuwalelea watoto wao?

Acha wazae hakuna MTU anajua mambo ya baadae.

Swala ambalo nkubaliana na wewe ni kuwa wazae watoto wachache ambao watawamudu.

Ila kutozaa kabisa hiyo hapana nchi yetu Ina umasikini lakini sifikirii Kama ukiwa masikini utashindwa kulea watoto 2-3 .

Acha wazae mkuu.
 
Sikubaliani na wewe , uzuri ni maandishi tu, acha wazae
 
Kuna kamoja kalikuwa kanasoma kamenona vibaya sana mjomba wake ni rafiki yangu. Anko akaanza kukashauri hata hakakusikia kakaacha shule. Kakampata sharobaro fulani akakaoa mara pa kakanasa mimba aise nimekutana nako juzi sokoni kameshazaa kamefuria mpaka kamekausha.
Nikakaita karipogeuka aise kidogo kakimbie.

Kamekonda kama mbwa aliyekosa matunzo . Nikakauliza vipi maisha kakasema yule sharobaro alikakimbia sasa kamepanga mjini kanaungaunga tu.

Nikampigia rafiki yangu yaani mjomba wake .Jamaa akanijibu tu shoti .Asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu.

NAMIMI SHUKA CHINI NAMALIZIA KWA KUSEMA "NIMWENDO WA KUGARAGARA."
 
Lipa kodi, kodi iende kwenye elimu na afya, hutawaona huko barabarani.
Maskini mmekuwa mitaji ya tabaka tawala, nyie mnaobeba watoto mgongoni ndio nyie mnasema mitanom tena, anatosha, alafu mnakuja huku kuomba huruma.
#kila mtu ale alipopeleka mboga.
Serikali mbona inakusanya Kodi nyingi sana ungejiuliza kwanini miradi inayosimamiwa na serikali inakufa jibu utalipa kumbe ata usimamiaji wa Kodi zetu Kuna shida
 
Lipa kodi, kodi iende kwenye elimu na afya, hutawaona huko barabarani.
Maskini mmekuwa mitaji ya tabaka tawala, nyie mnaobeba watoto mgongoni ndio nyie mnasema mitanom tena, anatosha, alafu mnakuja huku kuomba huruma.
#kila mtu ale alipopeleka mboga.
Serikali mbona inakusanya Kodi nyingi sana ungejiuliza kwanini miradi inayosimamiwa na serikali inakufa jibu utalipa kumbe ata kwenye usimamiaji wa Kodi zetu inawezekana Kuna shida
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…