Uchaguzi 2020 Ubunge Arusha sasa upo wazi kwa Godbless Lema

Uchaguzi 2020 Ubunge Arusha sasa upo wazi kwa Godbless Lema

Heshima sana wanajamvi,

Mbio za ubunge katika jiji letu la Arusha sasa zipo wazi kabisa kiasi kwamba hata kipofu ni rahisi kujua na kufahamu nani atashinda ubunge.

Mara baada ya Mheshimiwa Mrisho Mashaka Gambo kupitishwa na kamati kuu kugombea ubunge Arusha Mjini kulikuwa na sintofahamu kubwa miongoni mwa wanaCCM kindakindaki. Wengi walijiuliza kulikoni kamati kuu kupitisha jina la mgombea ambae tayari alishasemwa hadhani na mheshimiwa Rais na hata Katibu Mkuu wa CCM Taifa Dr Bashiru.

WanaCCM wengi walikubaliana pengine kamati Kuu iliangalia nani mwenye uwezo wa kushinda nafasi ya ubunge na kuviweka vigezo vingine kando ikiwemo tuhuma za rushwa, uchonganishi (kiwanja cha Msikiti Mkuu Bondeni), kukwamisha ujenzi wa stand mpya, kuhujumu ujenzi wa shule mbali mbali kwa kisingizio cha udogo wa viwanja na nk.

CCM iliamini na kujiaminisha kwamba Mrisho Mashaka Gambo angewavusha salama katika uchaguzi mkuu, hapakuwemo mgombea mwingine wa kumzidi yeye.

Katika hali ya kushangaza sana kama si kusikitisha Mrisho Gambo Mashaka amepwaya kweli kweli, zile amri zake za ukuu wa Mkoa hazifui dafu katika kuomba kura. Mrisho bila ngoma,mdundiko na wacheza show hawezi kufanya mkutano,Mrisho bila kukusanya watu toka kata mbali mbali za wilaya ya Arusha Mjini,Arumeru hawezi kufanya mkutano, Mrisho Gambo bila usaidizi wa Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa hawezi kufanya mkutano. Mrisho Gambo yuko hoi bin taaban kisiasa na kiuchumi. Matajiri wengi wamejiweka kando na kampeni zake hawataki kutoa fedha tena wanamwangalia kama gari bovu.

Zipo tuhuma sijui zimetoka wapi, sijui nani kazianzisha zimesambaa kwa kasi ya ajabu juu ya kuungua soko la Samunge loooh hata kuandika naogopa soko la Samunge ni kaa la moto si mtaji tena wa Mrisho.

Naomba kuwasilisha.

Ngongo safarini Bukoba kwasasa nipo Katerero sokoni.
Hapo Katerero wape salaam zangu
 
Wasio ijua Arusha ndio watapinga ukweli huu ila gambo hawez fikisha ata40%.CCM apa wamebugi kumpa mzaramo nafasi yakupambana na Lema.
 
Wala usiogope , kuhusu soko la Samunge kuna tuhuma kwamba lilihujumiwa na Gambo ili apate nafasi ya kuchangia mabati kwa lengo la kupata kiki (ni kweli alitoa bati ) japo hakununua yeye bali yeye ndiye aliyejulikana katoa, hata hivyo hali imekuwa ngumu kiasi ambacho yasemekana anafikiria kujitoa
Daah! Masisiemu ni mashetani. Mtu anathubutu kichoma soko ili achangie kwa lengo la kuonekana.???
 
Wajumbe wa Arusha walipaswa kujifunza toka kwa wenzao wa Kigamboni!
 
Bwashee majimbo ya Tunduma, Mbeya mjini, Iringa mjini, Moshi mjini, Hai, Arusha, Karatu, Kigoma mjini na Tarime yote labda uje muujiza wa Yesu ndipo CCM itayachukua! Acha ukweli ubaki kuwa ukweli tu.

nakuonea huruma. lissu na mbowe walivoenda moshi kilichowatokea ni Mungu alikua tu pamoja nao! wakanyage tena moshi watajua umuhimu wa maisha, arusha usituweke kwenye huo upuuzi wenu kwanza juzi madiwani wenu sjui 10 wamehamia ccm
 
Huyo mzaramo labda akawe mbunge wa kisarawe,chuga maendeleo yote yamefanywa na madiwani wa cdm...ccm miaka 56 walikua wanakata mauno tu...jamaa kapoa kama kanywa alkasusu ya maziwa ya kenge
Nipo Arusha, Mrisho Gambo anashinda saa 2 asubuhi, Lema anaulizwa alichofanya Arusha amekosa jibu, alishindwa hata kuwapa pole wana Samunge waliounguliwa na soko, kwa aibu ametunga uongo wa soko kuchomwa, Lema ana hali ngumu sana, safari hii anaondoka.
 
Umeandika yaani Mtu akisoma anasema Mrisho kaisha kweli. Hahahaha mwisho wa siku Mrisho anaibuka Kidedea kama ilivyokuwa kura za Wajumbe. Kishindo tu. Mrisho ndio Mbunge makini atakuwa.
Kwa msaads wa polisi atashinda, lakini kwa jura halali hata 15,000 hapati
 
Tatizo la JF ndio hilo, mtu anaweza kuwa zake Nyang’wale au Uyole huko na Dar hapajui lakini anashupaza msuli wa shingo kueleza nani atashinda Kawe!
 
Duniani hasa mataifa ya afrika kinapokaribia kipindi cha chaguzi mbalimbali kwenye haya mataifa, baadhi ya makundi huingiza pesa haramu kufadhili vyama ,au makundi mbalimbali ili yaunde serikali kwa makubaliano flaniflani yenye lengo la kuweka watu wao ambao watakua -remoted.

Fedha hizo huingizwa nchini si kwa ajili ya kufanyia kampeni ,bali hutumika kuandaa vikundi mbalimbali vya kihalifu kwa lengo la kufanya hujuma na mashinikizo flani yenye maslahi ya wachache na si kwa nchi husika .

Niipongeze serikali hasa vyombo vya ulinzi na usalama kwa kuliona hilo mapema sana .

Ifahamike vyama hasa vikubwa vya upinzani nchi kwa mujibu wa sheria vinapokea ruzuku kila mwezi, na pia huchangishana ,kazi ya fedha hizo ni pamoja na kuzitunza kwa ajili ya chaguzi mbalimbali ukiwemo na uchaguzi mkuu wa mwaka huu .

Inasikitisha kuona mgombea anatoka hadharani kulalamika ya kwamba pesa imezuiliwa kuingia nchini ,ooh! wafanyabiashara tuliokuwa tunawategemea wamehama nchi ,ni kina nani hao waliohama nchini ?na wanapodhamini uchaguzi nini matarajio yao kama si ukwepaji wa kodi?,

Suala la kujiuliza kwanini pesa hizo zije kipindi hiki cha uchaguzi ?,nani mfadhili wa hizo pesa ?anatarajia nini kwa anaowafadhili?,imani yangu kuna nia ovu dhidi ya taifa.

Uchaguzi ni mchakato wa muda mrefu wenye maandalizi ya kina yalioratibiwa kwa ustadi makini sana .

Namalizia kwa kusema wote ambao mnagombea dhamira zenu ni kujinufaisha binafsi na si taifa mtashindwa kwa aibu sana
Mgombea ambae hajui kwanini umeme uko juu,miaka 56 mmetawala hamna lolote zaidi ya ufisadi,kununua ndege, sgr kujenga airport kwake bado tu hajaelewa kwanini umeme uko juu
IMG_20200917_103801.jpeg
 
Back
Top Bottom