Uchambuzi wa Kiufundi naunga mkono nchi yetu kununua umeme kutoka inje nchi kuliko kusafilisha hadi kaskazini

Kama pesa za kununua umeme Etjiopoa zipo, kwanini za kuboresha hayo mbwawa ya Nyimba ya Mungu, Hale na Pangani hakuna???
 
Wazee wa shortcut.

No wonder bila Magufuli kukomaa na bwawa la Nyerere mpaka sasa tungekuwa bado tunakomaa na bwawa la Mtera na vikampuni uchwara vya kuuza umeme vya Dowans, Songas na IPTL.

Kweli pesa haikai nyumbani kwa mpumbavu, inapita tu.
 
Kasome economies of scale, mfano wako haufiti hapo. Usambazaji wa umeme hauendi kwenye nyumba moja kama mfano wa maji kwenye nyumba dsm na dodoma. Anyways upo kufanya uchawa na namba ya simu umeacha go ahead do your things.
 
Kasome economies of scale, mfano wako haufiti hapo. Usambazaji wa umeme hauendi kwenye nyumba moja kama mfano wa maji kwenye nyumba dsm na dodoma. Anyways upo kufanya uchawa na namba ya simu umeacha go ahead do your things.
Na wewe kasome power loss na power factor katika transmission!

Hapa nimetumia lugha rahisi kabisa ili hata mwananchi wa chini aelewe!

Ukitaka niongee lugha za umeme mwanzo mwisho wengi wasingeeelewa!

Hata nchi zilizoendelea zinanunua kutoka inje, Tanzania haitakuwa ya kwanza!

Na kingine ambacho huwezi kukijua unapoongezea umeme kutoka inje unakuwa umeongeza flexibility katika gridi ya taifa .
Note; Gridi ipo lakini huo umeme wa kutoka inje ni plani B, wakati Plan A Ikiendelea taratibu hatua kwa hatua.
 
Kama pesa za kununua umeme Etjiopoa zipo, kwanini za kuboresha hayo mbwawa ya Nyimba ya Mungu, Hale na Pangani hakuna???
Kuna ukame! Imetazamwa Plan B, wakati taratibu za uboreshaji zikiendelea taratibu za plan A.

Huwezi wazimia umeme wakazi wa kaskazini ili ufanye marekebisho makubwa! Unatakiwa uwe na umeme mbadala ambao ndio huo wa plan B ili kukata huu wa zamani kwa ajili ya matengenezo makubwa ya mabwawa ya nyumba ya Mungu!
 
Ndugu kwahiyo unataka nikujibu kipi hapo?
Unaelewa kwanini umeme mkubwa hautakiwi kupita juu ya bomba kubwa la mafuta? Unaelewa ni kwa nn?

Unafaham mikoa ya kaskazini inapokea megawatts ngapi na ina upungufu wa megawatts ngapi?
Jibu swali mkuu, electrical frequencies na gasoline vinashabihiana vipi? Kuna connection gani kati ya frequencies za umeme na mafuta?
 
Waingize tu uo umeme nasi tukiwa na wakutosha wao wakipungukiwa tutawauzia kupitia kaskazini simple
 
Kwa moves zinazofanywa na Wizara nyingi hapa Tanzania hata wewe Lumumba Buku Saba usiyejua wapi pa kutumia "l" na "r" unaweza kuwazidi akili vizuri tu.
 
Kumbe kuimbishwa kote kwamba bwawa la Rugiji likikamilika matatizo ya umeme itakuwa mwisho ilikuwa ni siasa tu!
Haikuwa siasa mkuu, binafsi naamini haikuwa siasa, ila ubovu wa mifumo ndio unafanya ionekane hivyo. Hakuna mifumo thabiti ya kusimamia mipango na utekelezaji wake ndio maana maono ya kiongozi mmoja yanafifishwa pale tu mwingine anapoanza madaraka.

Fikiria wakati wa JPM hakukuwa na shida ya kukatika umeme, huko kaskazini tunakoongelea leo kila mtu alishangaa imewezekanaje, leo tunasoma hadithi nyingine za kuongeza umeme kwa sababu hata hazieleweki.
 
Jibu swali mkuu, electrical frequencies na gasoline vinashabihiana vipi? Kuna connection gani kati ya frequencies za umeme na mafuta?
Sheria za pipeline transmission haziruhusu power line transmission kukatiza juu kwa usalama!
 
Ethiopia, Uganda, Zambia watu Plan B yao ya umeme wamenunua wapi?

Unasema huwezi kuzima umeme kufanya matengenezo mboma wanazima kilamsiku, hata Dar ilikuwa kwenye mgawo juzi tu hapa.

Unazungumza kuhusu ukame, kwani Ethiopianumeme wao ni Nuclear??

Wanatumia Bwawa na tena Ethiopia ninmchi ambayo inakabiliwa na ukame kuliko sisi?
 
Kwani si tunayo grid ya taifa tayari? Kuna haja ya kujenga miundo mbinu mipya kupeleka umeme kaskazini?
 
Sheria za pipeline transmission haziruhusu power line transmission kukatiza juu kwa usalama!
Mbona uliongelea mambo ya frequencies?

Tanzania has a vastland, kama kuutoa Kenya kuja TZ inawezekana, hoja ya kwamba pipelines under power transmission line ni porojo na hazina mashiko propaganda za ajabu sana.
 
Kufanya matengenezo ya kudumu katika bwawa la nyumba ya mungu linahitaji si chini ya misimu miwili ya mvua!
Msimu wa kwanza nikuondoa maji yote katika bwawa ili kuongeza kina cha maji na kufanya matengenezo na kuongeza transfoma!

Msimu wa pili ni kujaza maji kabla ya kuwasha mitambo!

Unataka serikali iwakatie umeme wananchi miaka yote hiyo miwili ya matengenezo?

Inaposema inaleta umeme kutoka inje inataka kuboresha kiwango cha umeme wa ndani kiwe super zaidi kwa gharama nafuu!

Yale matengenezo ya kila siku huwa ni matengenezo madogo ya nguzo zilizochoka, na dharula ndogo ndogo za masaa kadhaa!

Bwawa siyo bakuli kwamba utaliosha siku moja ukamaliza
 
mtoa mada na ww ubongo wako wa konokono, wengi wanapiga kelele kwasababu waliopewa dhamana wamekosa maono, na ni wanaangalia vizazi vyao.

kiuhalisia ethiopia ni wapili Africa kwa uzalishaji wa umeme, lakini asilimia zaidi ya 90 ya umeme wao unatokana na hydropower. ambapo gharama ya uzalishaji ni kama tz tu, iweje wao wauze bei rahisi sisi tuuze bei kubwa.

tukija kwa tanzania tuna mavyanzo mengi ya umeme ambayo hayana hata faida mtu akikurupuka na wazo la umeme wa biogas ataupamba ni bei rahisi na tuna akiba ya kutosha mwisho wa siku 63% ya umeme wa Tanzania ukawa ni from biogas na hakuna cha bei kushuka wala nn.

akaja rais awamu ya 5 akataka kututoa kwenye kifungo cha kutoshuka bei kwa umeme akaturn kwenye uwekezaji mkubwa wa hydropower, mradi ulipromise kushuka bei kwa umeme kwasababu uzalishaji wake hauna gharama, lakini tukatangaziwa umeme hauwezi kushuka.

nafikiri hoja kubwa ipo hapa "kwanini kila chanzo cha umeme tanzania kunachoonekana ni relief ya bei ya umeme kikianzishwa hakileti hiyo relief ya bei kama ilivyotarajiwa"

nina imani kama bei ingekuwa chini hakuna ambaye angeenda kuhangaika na umeme wa nje ya nchi.

ukilijua hili mtoa mada utaacha kutetea ujinga usioujua.
 
Kwa hilo tuombe tu uhusiano wetu na hao majirani uwe mzuri. Ila siku mambo yakiharibika kuna hatari ya kuzimiwa huo umeme. Mifano tunayo mingi sana hapa duniani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…