1. Mtazamo wa Kidini (Theolojia)
Katika imani nyingi za kidini (kama Uislamu na Ukristo), sifa kuu ya Mungu ni kwamba yeye ni wa milele—hana mwanzo wala mwisho.
Mungu kama Chanzo: Imani hizi zinafundisha kuwa kila kitu kilichopo kiliumbwa, lakini lazima kuwe na "Chanzo kisichochimbika" (Uncaused Cause). Ikiwa Mungu angekuwa ameumbwa, basi huyo aliyemuumba angekuwa "Mungu" zaidi yake, na mfululizo huo ungeendelea bila mwisho.
Nje ya Muda na Nafasi: Dini zinaeleza kuwa "kuumbwa" ni tendo linalohitaji muda na nafasi. Kwa kuwa Mungu anachukuliwa kama muasisi wa muda na nafasi, yeye yuko nje ya sheria hizo. Kwa hiyo, swali "aliumbwa na nani" halimtahini yeye kwa sababu yeye si kiumbe.
2. Mtazamo wa Kifalsafa na Mantiki
Wanafalsafa hutumia hoja ya Mstari wa Sababu (Infinite Regress):
Sababu ya Kwanza: Ili ulimwengu uwepo, lazima kuwe na kitu cha kwanza ambacho hakikuhitaji kusababishwa na kitu kingine. Kama kila kitu kingehitaji muumbaji, basi tusingekuwa na mwanzo kabisa, na ulimwengu usingekuwepo leo.
Hoja ya Aristoteli: Mwanahisabati na mwanafalsafa Aristoteli aliita dhana hii kama "Unmoved Mover" (Mwenye kusogeza asiyesogezwa). Ni nguvu au hulka ambayo ilianzisha kila kitu bila yenyewe kuanzishwa.
3. Mtazamo wa Kisayansi
Sayansi (kama Fizikia ya Quantum) mara nyingi haijibu swali la "Mungu," bali huangalia chanzo cha ulimwengu (kama vile Big Bang). Hata hivyo, changamoto inabaki pale pale: Nini kilisababisha Big Bang? Wanasayansi wengine wanahoji kuwa nishati au kanuni fulani za kifizikia zinaweza kuwa zilikuwepo daima.
Kimantiki, ikiwa Mungu aliumbwa, basi huyo aliyemuumba ndiye angekuwa Mungu wa kweli. Ili kuepuka mfululizo usio na mwisho wa waumbaji, hitimisho la kifikra ni kwamba lazima kuwe na asili ya kwanza ambayo haikuumbwa na yeyote—na hiyo asili ndiyo watu wanaiita "Mungu."
"Umezungumzia udongo na maji vizuri, lakini sasa nataka tuiangalie 'Saa ya Muda' (Timeline). Dini za Ibrahimu zinatupa picha kuwa binadamu na dunia vina umri wa takriban miaka 6,000 hivi. Lakini tukiacha maandiko na kuangalia mazingira:Kwa asilimia kubwa umejibu hoja zangu,usijali kuhusu maandiko marefu huwa hayanipi shida huenda kwasababu kusoma ni sehemu ya hobby yangu
Pamoja na maelezo mazuri ambayo yamejibu hoja zangu,kuna sehemu nataka kukuchallenge.
Katika hoja yako ya mwili wa binadamu sasa kuwa na elements ambazo hazikuwepo miaka kadhaa nyuma ikiwemo plastics na element nyingine ambazo umezitaja sina haja ya kuzirudia hapa
Umenichallenge kwa kusema je,Mungu atakuwa amebadilisha udongo katika uumbaji? Sasa hoja yako au maelezo yako yangekuwa na uzito kama bado mpaka leo hii tungekuwa tumeumbwa au kutokana na udongo,kwa maana ya kwamba kungekuwa hakuna kuzaliana na sote tungeumbwa kwa udongo hapo sasa ndio tungejiuliza je,udongo umebadilishwa?
Kwahiyo utaona kwamba kama hoja ya binadamu ametokana na udongo ni sahihi,basi tutasema udongo wa mwanzo ndio ambao tunaupa kipaumbele,kwasababu kizazi kilichofuatia kimetokana na maji kwahiyo ni sahihi kizazi kuwa na element ambazo huko nyuma hazikuwepo,na hii ni kutokana na mabadiliko ya mazingira na mwanadamu kuwa exposed na mambo mbalimbali katika zama hizi
Huwa napata mashaka na historia za miaka mingi namna hiyo,ikiwa tu miaka 2,000 toka kuwepo kwa Yesu kuna taarifa nyingi zenye kuchanganya na masimulizi yenye mkanganyiko mkubwa,vipi iweje unazungumzia miaka 60,000 au 30,000"Umezungumzia udongo na maji vizuri, lakini sasa nataka tuiangalie 'Saa ya Muda' (Timeline). Dini za Ibrahimu zinatupa picha kuwa binadamu na dunia vina umri wa takriban miaka 6,000 hivi. Lakini tukiacha maandiko na kuangalia mazingira:
Huoni kwamba hapa ndipo 'manipulative tools' za dini zinapotupa majibu mepesi (miaka 6,000) ili kutuziba macho tusiione safari ndefu na ya ajabu ya binadamu iliyochukua mamia ya maelfu ya miaka?"
- Mataifa kama China, India, na hata wenyeji wa Australia (Aborigines) wana historia na kumbukumbu za kuwepo kwao zinazovuka miaka 30,000 hadi 60,000. Je, hawa watu walitokea wapi ikiwa kalenda ya 'uumbaji' inasema binadamu ana miaka 6,000 tu?
- DNA Molecular Clock Ubadilikaji wa DNA (mutations) unatuambia kuwa imechukua mamia ya maelfu ya miaka kwa binadamu kufika hapa tulipo. Sayansi ya vinasaba inathibitisha kuwa 'Mababu' wetu wa kwanza waliishi zaidi ya miaka 200,000 iliyopita.
- Mabadiliko ya Mwonekano Inachukua muda mrefu sana kwa udongo na mazingira kubadili DNA ya binadamu mpaka atokee mweusi sana au mweupe sana. Miaka 6,000 ni muda mfupi mno kutoa utofauti wa watu wote tunaowaona duniani leo.
Mbona leo hii haviendelei kutokea?Kama Mungu hakuumbwa kwa nini hamuamini kuwa vitu duniani vilitokea vyenyewe tu
Maana sio kila kitu lazima kiumbwe kama Mungu hakuumbwa 😅
Kumbe ndio ww hata huamini kwenye power greater than yourself.Inabidi mpatane kwanza imani zaidi ya 200000 mje na Mungu mmoja kwanza , ili mje na hoja zenye mashiko.
umewahi kufika india au china? au hata misri?Huwa napata mashaka na historia za miaka mingi namna hiyo,ikiwa tu miaka 2,000 toka kuwepo kwa Yesu kuna taarifa nyingi zenye kuchanganya na masimulizi yenye mkanganyiko mkubwa,vipi iweje unazungumzia miaka 60,000 au 30,000
Ishu hapa inakuja je kuna ukweli kiasi gani wa hizo historia,na kibaya zaidi huko nyuma hatukuwa na fasihi andishi useme taarifa zimehifadhiwa vizur na hata kama ilikuwepo ni ile ndogo sana,hapa ukweli wa taarifa ukoje
Kwa nini unataka vitokee kwa mara ya pili 🤔Mbona leo hii haviendelei kutokea?
Chief unanipa raha sana,piga spana1. Wewe mwenyewe unaamini mambo mengi ambayo hayathibitishwi kwa sayansi. Unaamini kwamba maumivu ni mabaya sayansi haiwezi kuthibitisha hilo. Unaamini kwamba ukatili ni mbaya sayansi haiwezi kuthibitisha hilo. Hizi ni imani za kimantiki na kimaadili na hisia za mmwili wako si za kisayansi. Kwa hiyo mfumo wako mwenyewe una mambo yanayokwepa sayansi. unaamini Julius Caesar alikwepo na vitu vinavyofanana na hivi ingawa haviwezi kuthibitishwa kisayansi
2.Unasema kuumizwa ni mbaya kwako nakubaliana nalo. lakini Problem of Evil haizungumzii preference yako au mapendelo yako binafsi. Inazungumzia madai ya maadili ya ulimwengu wote kwamba ukatili ni mbaya kwa kila mtu, wakati wote, mahali pote. Preference yako ya kibinafsi haifikii hapo. kuna mtu anapenda kuumiza wengine ana preference yake pia na nikitu kinachomfurahisha kwaiyo kwake ni kiziri preference yake ni halali sawa sawa na yako. Kwa nini yako ni sahihi zaidi?
3.Unasema vita za kidini ni ushahidi wa ukatili wa Mungu. lakini vita za kidini zimefanywa na binadamu si Mungu. Binadamu wamechukua jina la Mungu na kutumia kwa maslahi ya nguvu, siasa, na ubinafsi. Kulaumu Mungu kwa matendo ya binadamu wanaotumia jina lake vibaya ni kama kulaumu Einstein kwa silaha za nyuklia aliandika equations, watu wengine walichagua kuzitumia vibaya. au kumlaumu mtu aliyetengeneza kisu kwasababu kuna watu wanauawa kwa kuchomwa visi
pia una logical fallacy inayoitwa Argument from Ignorance kusema kwa sababu hatujui kwa uhakika, kitu hakipo. Lakini ukweli wa kitu hautegemei uelewa wetu wa kitu hicho. Kwa maelfu ya miaka binadamu hawakujua vijidudubkama bakteria vipo je, vijidudu havikuwepo? Hawakujua galaxies nyingine zipo je, hazikuwepo? Kutojua au kutokubaliana juu ya kitu hakuthibitishi kitu hicho hakipo.
Unasema Mungu angekuwepo, mjadala usingekwepo. lakini hata kama Mungu yupo na anajithibitisha binadamu bado wangeweza kukataa. Hii si nadharia binadamu wanakataga ushahidi wa kisayansi ulio wazi kila siku. Watu wanaamini dunia ni flat licha ya ushahidi wote. Kwa hiyo hata ushahidi wazi haumalizi mjadala kwa sababu tatizo si ushahidi, tatizo ni binadamu na uhuru wao wa kukataa.
poa kwakonaona pattern moja katika hoja zako zote: unabeba mzigo mkubwa wa assumptions ambazo wewe mwenyewe hujazithibitisha kwamba maadili yanaweza kuwepo bila msingi wa nje ya binadamu, kwamba Mungu mwenye upendo lazima aondoe matokeo yote ya uhuru, kwamba uthibitisho wote lazima uwe wa kisayansi. Kila assumption hiyo yenyewe inahitaji mjadala mrefu.
Kwanini wewe umejiamulia ku assume hivyo ?
Kama ulimwengu ulivyotokea wenyewe tu au viumbe vilitokea vyenyewe tu basi hakika utaratibu huo ungeendelea kutokea tu,kwakuwa hakuna formula maalumuKwa nini unataka vitokee kwa mara ya pili 🤔
Ukishasema Mungu ni wa milele umesha contradict habari kwamba kila kilichopo kina muumba.
Ukisema Mungu ni special, yeye tu hahitaji muumba, hiyo ni special pleading logical fallacy.
Ukisema Mungu amekuwapo milele, swali linakuja, kama unasema Mungu kawepo milele, ushakubali kwamba kuwapo milele kunawezekana, sasa, kwa nini ulimwengu usiwe umekuwapo milele bila Mungu, haujaumbwa na Mungu? Ushakubali kuwapo milele kunawezekana. Sasa kwa nini ulimwengu usiweze kuwa umekuwapo milele na haujaumbwa na Mungu?
Maana katika hoja kubwa za kutetea uwepo wa Mungu ni kwamba Mungu ndiye kaumba ulimwengu.
Huoni kuwa ukishakubali kuwepo milele kunawezekana, hata kwa Mungu, unaondoa umuhimu wa Mungu kuwepo kama muumba ulimwengu, kwa sababu inawezekana ulimwengu ukawa ulikuwepo milele na haumuhitaji Mungu kuuumba?
2. Infinite regress haituoneshi kuwa Mungu lqzima awepo, inaonesha tu kuwa mambo hayawezi kurudi nyuma bila chanzo chabasiki. Chanzo cha asiki si lqzima kiwe Mungu, kusema hivyo ni logocal nonnsequitur fallacy. Kama ulimwengu umekuwapo milele bila kuhitaji muumba hapo hakutakuwapo na infinite regress wala Mungu.
Umekimbikia kusema ulimwengu umeumbwa na Mungu kabla hata ya kuonesha ulimwengu hauwezi kuwa umekuwapo tu milele.
3. Bog Bang haielezei chanzo cha ulimwengu inaelezea bdeakdown ya sayansi kueleea ulimwengu umeanza vipi katika singularity ambapo sayansi yetu ya Einsteinian Relativity na Quantum Physics haiwezi kujibu tunahitaji sayansi moya ya Quantum Gravity.
Zaidi, Big Bang inaelezea ulimwengu huu tu wakati kuna nadharia za multiverae zinazoelezea kuwa Big Bang na ulimwengu huu ni kioande kidogo tu katika multiverae iliyo na malimwengu mengine kama haya matrilioni na matrilioni yenye Bog Bang zake tofauti na sheria za fizikia zake tofauti. Nilikiwekea video post namba 27 lakini naona hujaiangakia na kama umeiangakia hujaielewa.
Ikiwa asili iliyoumba vyote ni ulimwengu ambao hauna muumbaji, ipo tu miele, utasema ulimwengu huo ndio Mungu?
Na utakubali kuwa Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na uoendo wote hayupo?
Ukisema kwamba Aristotle aliamini ulimwengu ulikuwepo milele na pia aliamini Mungu alikuw aunmobed mover, unaonesha cobtradiction.Wanafalsafa kama Aristotle waliamini ulimwengu ni wa milele, lakini bado waliamini kuwepo kwa "Mungu" (Unmoved Mover).
Hoja: Hata kama ulimwengu umekuwapo milele, kwa nini unafuata sheria fulani za hisabati na fizikia? Kwa nini kuna mpangilio badala ya fujo (chaos)?
Mtazamo: Katika hali hii, Mungu si "Muumba" wa malighafi, bali ni "Akili" au "Kanuni" inayofanya ulimwengu uendelee kufanya kazi kwa utaratibu. Mungu hapa ni kama sheria ya uvutano iliyo hai.
3. Pantheism: Ulimwengu NDIO Mungu
Kama ulimwengu ni wa milele na haukuhitaji muumba, wanafalsafa kama Baruch Spinoza walisema basi ulimwengu wenyewe una sifa zote tunazompa Mungu.
Hoja: Ulimwengu ni mkubwa, hauna mwisho, una nguvu zote, na ndio chanzo cha uhai.
Matokeo: Katika mtazamo huu, "Mungu" na "Ulimwengu" ni neno moja lenye maana mbili. Hapa, dhana ya Mungu haiondoki, bali inabadilika kutoka kuwa "Mtu" (Person) na kuwa "Asili" (Nature).
🖕Kumbe ndio ww hata huamini kwenye power greater than yourself.
Au higher power
wanakazaga vichwa kama vile hawaelewi kabisa kinachoongelewaChief unanipa raha sana,piga spana
Hakuna manachoweza thibitisha zaidi ya mashudu tu, ya kuzunguka zunguka mara ni super power wa dini sio ,mwisho wa siku mnarudi mule mule tu.wanakazaga vichwa kama vile hawaelewi kabisa kinachoongelewa
Mkuu,Huu mjadala wa mungu utakuwa mwepesi sana siku tutaweza kuwasiliana na aliens kutoka sayari nyingine.
UKo sahihi lakini kuna jambo moja ningependa kukurekebisha"Umezungumzia udongo na maji vizuri, lakini sasa nataka tuiangalie 'Saa ya Muda' (Timeline). Dini za Ibrahimu zinatupa picha kuwa binadamu na dunia vina umri wa takriban miaka 6,000 hivi. Lakini tukiacha maandiko na kuangalia mazingira:
Huoni kwamba hapa ndipo 'manipulative tools' za dini zinapotupa majibu mepesi (miaka 6,000) ili kutuziba macho tusiione safari ndefu na ya ajabu ya binadamu iliyochukua mamia ya maelfu ya miaka?"
- Mataifa kama China, India, na hata wenyeji wa Australia (Aborigines) wana historia na kumbukumbu za kuwepo kwao zinazovuka miaka 30,000 hadi 60,000. Je, hawa watu walitokea wapi ikiwa kalenda ya 'uumbaji' inasema binadamu ana miaka 6,000 tu?
- DNA Molecular Clock Ubadilikaji wa DNA (mutations) unatuambia kuwa imechukua mamia ya maelfu ya miaka kwa binadamu kufika hapa tulipo. Sayansi ya vinasaba inathibitisha kuwa 'Mababu' wetu wa kwanza waliishi zaidi ya miaka 200,000 iliyopita.
- Mabadiliko ya Mwonekano Inachukua muda mrefu sana kwa udongo na mazingira kubadili DNA ya binadamu mpaka atokee mweusi sana au mweupe sana. Miaka 6,000 ni muda mfupi mno kutoa utofauti wa watu wote tunaowaona duniani leo.