Ufafanuzi wa Kujadiliana na watu wasioamini uwepo wa Mungu

Huko kusema "mpangilio huu una ashiria" tayari ni assumptions zisizo na ushahidi wowote ule.

Kwa hivyo una assume tu, kwa vile ulimwengu una mpangilio basi hapohapo unahitimisha Mungu ndiye designer. Wakati hata hujathibitisha uwepo wa huyo Mungu.

Thibitisha uwepo wa huyo Mungu, yeye kama yeye bila kumhusisha na ulimwengu.

Kwa nini unatumia mpangilio wa ulimwengu kuuhusisha na huyo Mungu?

Unafanya logical fallacy ya non sequitur.

Unaunganisha vitu viwili tofauti visivyokuwa na uhusiano wowote ule kuunda hitimisho potofu.
 
kweli
 
AI inaweza
 
Zipo jamii zinaamini MUNGU wao ni Mmoja na hauondoi ukweli wa jamii zingine wanaoamini miungu Yao iko mingi. Kwa sababu kuu ni kuwa wote hawawezi kuthibitisha.

Robert Heriel Mtibeli na min -me .
Naona Hamuamini uwepo wa Mungu. Lakin naona kwenye comments na post zenu mbali mbali mnasisitiza Hekima, uungwana na namna bora ya Kuishi kama Binadamu.

Hii namna bora mnayofikiria inatoka ndan ya nafsi zenu, na ndio mnahisi ni sahihi sisi binadamu tuishi kwa namna hiyo. (Regardless na Dini).

Na kama bas mngepewa kudra kuelekeza watu waishi bas bila shaka mngewaongoza waishi namna hiyo. Si ndio?.

Sasa mjue tu kuwa na yenyewe ingeitwa Dini.

Hii ni Bila hata kusema mnamuamini Mungu mmoja. Au Miungu weng au mizimu au hamumini kabisa.

Kwasababu Dini ni taratibu, tamaduni na Miongozo jinsi ya Kuishi maisha yako Duniani.

Mm naamin Mungu yuko, ila namna ambayo anaelekeza watu wake waishi ndio iko tofauti.

NB;: hata wale wanaoamini Miungu Mingi. Mfano Hindus .Pia wanaamin kuwa hiyo Miungu (chiva) anapata nguvu zake kutoka sehem moja. (Centre ya supreme power).

Haya Ni mawazo Yangu.
 
Hoja ya Kusababishwa (Cosmological Argument)
Kila kitu tunachokiona kina chanzo chake. Hakuna kitu kinachoweza kujisababisha chenyewe kuwepo.
Kama hakuna kitu kinachoweza kujisababisha chenyewe, Hata huyo Mungu hawezi kujisababisha mwenyewe.
Hoja: Ikiwa ulimwengu upo, lazima kuna kitu kilichosababisha uwepo wake. Sayansi ya sasa (kama nadharia ya Big Bang) inakubali kuwa ulimwengu ulikuwa na nukta ya kuanza.
Hoja: Ikiwa Mungu yupo, lazima kuna kitu kilisababisha uwepo wake.

Mungu huyo hawezi kuwepo tu, from nowhere.
Ikiwa hakuna mwanzo, inakuwaje leo tupo hapa?
Mwanzo kutoka wapi?

Mwanzo kuanzia wapi?
Huwezi kufika 'leo' kama kulikuwa na idadi isiyo na mwisho ya siku zilizopita (Infinite Regress)."
Cosmological arguments hazithibitishi uwepo wa Mungu.

Cosmological arguments ni assumptions tu, zinazo jaribu kuelezea uwepo wa huyo Mungu.
 
kwa akili za binadamu zinafikiri kila kitu kimetokea wapi

Mungu ndiye mwanzilishi
hapakuwa na kitu ila yeye
akaumba ulimwengu
hata muda aliumba.
muda haumlimit yeye
na mawazo yake sio kama yetu
 
your faith healed u
 
kwa akili za binadamu zinafikiri kila kitu kimetokea wapi
Kwa nini unafikiri kila kitu kimetokea sehemu fulani?

Kwa nini hufikirii kitu kinaweza kuwepo chenyewe bila kutokea sehemu fulani?
Mungu ndiye mwanzilishi
hapakuwa na kitu ila yeye
akaumba ulimwengu
hata muda aliumba.
muda haumlimit yeye
na mawazo yake sio kama yetu
Kabla ya kusema Mungu ndiye muanzilishi. Kwanza thibitisha uwepo wake.

Usirukie kusema Mungu ndiye muanzilishi wakati hata hujathibitisha uwepo wake.

Tutahakikisha vipi Mungu ndiye muanzilishi bila uthibitisho wa uwepo wake?
 
kuna vitu vingine banah,kwanza kumlazimisha mtu mzima mwenye ndevu na akili timamu kuwa aache kuamini Mungu hayupo huo nao ni ukichaa mwingine,akili mnazo mnataka kulazimishwa kuamini uwepo wa Mungu kama mtoto mdogo anaelazimishwa kunywa uji yee😏
 
Hoja yako inatoka kwenye Mising gan?.
Logic and reasoning.
kuna mambo yako juu ya uelewa wetu. Lakin nina amini kila kitu kina maelezo yake.
Mambo kuwa juu ya uelewa wetu sio kigezo au uthibitisho wa moja kwa moja kusema Mungu yupo.

Kutokuelewa kitu fulani haimaanishi kwamba jibu la kitu hicho ni Mungu.
 
hapo juu umemwita Kiranga na Infro, we upo upande gani? unaamini uwepo wa Mungu au hapana
naamini uwepo wa Mungu
ni kwa muda mrefu nikiwa na bishana nao kuhusu uwepo wa Mungu
nduo maana nimewatag waje huku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…