Ufafanuzi wa Kujadiliana na watu wasioamini uwepo wa Mungu

Ufafanuzi wa Kujadiliana na watu wasioamini uwepo wa Mungu

Robert Heriel Mtibeli na min -me .
Naona Hamuamini uwepo wa Mungu. Lakin naona kwenye comments na post zenu mbali mbali mnasisitiza Hekima, uungwana na namna bora ya Kuishi kama Binadamu.

Hii namna bora mnayofikiria inatoka ndan ya nafsi zenu, na ndio mnahisi ni sahihi sisi binadamu tuishi kwa namna hiyo. (Regardless na Dini).

Na kama bas mngepewa kudra kuelekeza watu waishi bas bila shaka mngewaongoza waishi namna hiyo. Si ndio?.

Sasa mjue tu kuwa na yenyewe ingeitwa Dini.

Hii ni Bila hata kusema mnamuamini Mungu mmoja. Au Miungu weng au mizimu au hamumini kabisa.

Kwasababu Dini ni taratibu, tamaduni na Miongozo jinsi ya Kuishi maisha yako Duniani.

Mm naamin Mungu yuko, ila namna ambayo anaelekeza watu wake waishi ndio iko tofauti.

NB;: hata wale wanaoamini Miungu Mingi. Mfano Hindus .Pia wanaamin kuwa hiyo Miungu (chiva) anapata nguvu zake kutoka sehem moja. (Centre ya supreme power).

Haya Ni mawazo Yangu.
Upo sawa
 
Huyo Mungu yupo so insecure hadi anahitaji kuaminiwa?

Huyo Mungu akiaminiwa yupo anafaidika nini?

Huyo Mungu asipoaminiwa, anapungukiwa nini?
yupo secure
na yeye ndiye anayekulinda.
ni inashangaza kama mtoto wako haamini kama ww ni baba yake
ndio inavyokuwa kwa wale wasioamini uwepo wa Mungu.
 
Kujadiliana na watu wasioamini uwepo wa Mungu (atheists) kunahitaji hekima, subira, na hoja zenye mashiko ya kimantiki badala ya kunukuu maandiko pekee. Katika mazingira ya Kiislamu, mjadala huu mara nyingi hujikita kwenye kutumia akili (Aql) na mazingira yanayotuzunguka (Fitra).

Hapa kuna mbinu na hoja unazoweza kutumia:

1. Hoja ya Uwepo wa Ulimwengu (The Argument from Creation)
Hii ni hoja ya msingi inayouliza: "Je, kitu kinaweza kutokea bila muumbaji?"
Mantiki: Kila kilichochongwa kina mchongaji, na kila jengo lina mjenzi.

Ulimwengu ni mfumo tata sana; hivyo basi, ni muhali (haiwezekani) kuwa umetokea kwa bahati mbaya tu.
Mfano: Ikiwa utamkuta mtu ameweka simu ya kisasa mezani na akakuambia kuwa vipande vya chuma na kioo vilijikusanya vyenyewe na kutengeneza simu hiyo kwa mamilioni ya miaka, huwezi kumwamini. Je, ulimwengu ambao ni tata kuliko simu unawezaje kutokea bila mpangaji?

2. Mpangilio na Uwiano wa Ulimwengu (Fine-Tuning)
Wanasayansi wanakubali kuwa ulimwengu una sheria thabiti (kama nguvu ya mvuto - gravity).
Hoja: Ikiwa nguvu ya mvuto ingepungua au kuongezeka kidogo sana, nyota zisingetokea na maisha yasingewezekana. Uwiano huu unaitwa "Fine-Tuning."

Mantiki: Huu usahihi uliokithiri unaonyesha kuwa kuna "Akili" (Intelligence) iliyoweka viwango hivyo, na si vurugu ya bahati mbaya.

3. Asili ya Binadamu (Fitra)
Hii inahusu lile hitaji la ndani la binadamu kutafuta kitu kikuu zaidi (Transcendence).

Hoja: Hata watu wasioamini, wanapopata majanga makubwa (kama ndege inapotaka kuanguka), mara nyingi hujikuta wakitafuta msaada kutoka kwa nguvu iliyo juu yao.

Mantiki: Hisia hii ya ndani ni utambulisho uliowekwa ndani ya roho ya kila binadamu kumtambua Muumba wake.

4. Maadili na Utu (Objective Morality)
Hoja: Ikiwa hakuna Mungu, na sisi ni matokeo ya mageuzi (evolution) ya kikemikali tu, kwa nini tunaamini kuwa kuua au kudhulumu ni "kibaya"?

Mantiki: Bila Mungu, maadili yanakuwa ni maoni tu ya watu. Lakini binadamu wote wanaelewa kuwa kuna haki na batili. Haki hii ya asili inatoka kwa Muumba aliyeweka sheria za kimaadili.

Jinsi ya Kuzungumza Nao kwa ufanisi:
Tumia Lugha ya Mantiki: Atheists wengi huamini katika sayansi na ushahidi. Badala ya kusema "Kitabu kinasema hivi," sema "Tazama mfumo wa DNA, je, unawezaje kuwa na maelekezo tata kiasi hicho bila mwandishi wa kanuni hizo?"

Kuwa na Adabu na Subira: Lengo liwe ni kufahamishana, si kushinda vita ya maneno. Quran inatuhimiza tujadiliane kwa namna iliyo bora zaidi.

Kubali Mipaka ya Sayansi: Eleza kuwa sayansi inajibu maswali ya "Vipi" (Vipi mvua inanyesha?), lakini dini inajibu maswali ya "Kwa nini" (Kwa nini tuko hapa na nini hatima yetu?). Sayansi haiwezi kuthibitisha au kukanusha uwepo wa Mungu kwa sababu Mungu hayuko ndani ya maabara.

Ni hayo tu!
Sio kujadiliana na wasio amini MUNGU, ni kubishana. Hakuna majadiliano kati ya logic na faith.
 
yupo secure
Angekuwa secure wala usingehitaji imani ya kuamini uwepo wake.
na yeye ndiye anayekulinda.
ni inashangaza kama mtoto wako haamini kama ww ni baba yake
ndio inavyokuwa kwa wale wasioamini uwepo wa Mungu.
Kwa nini uamini badala ya kujua kwa uhakika na uthibitisho?

Mimi sihitaji kuamini nahitaji kujua kwa uhakika na ushahidi.
 
Angekuwa secure wala usingehitaji imani ya kuamini uwepo wake.

Kwa nini uamini badala ya kujua kwa uhakika na uthibitisho?

Mimi sihitaji kuamini nahitaji kujua kwa uhakika na ushahidi.
Nimethibitisha kwa kuwasiliana naye na kuongea naye,
jinsi unavyokuwa karibu naye unamuona zaidi.
 
Kufuatia kauli kwamba usiabudu miungu inaonyesha hiyo ni miungu feki,mfano wahindu baadhi wanaabudu ng'ombe kwahiyo hiyo ni sehemu ya moungu feki

Kama baadhi ya wanadamu wameumbwa na miungu tofauti,je inakuaje system ya miili yetu ni moja?

Au kwanini Mungu mwingine asingeumba mwanadamu anayeumwa,mbona wote tunachangamoto zile zile?

Yehova ndiye kasema hivyo kwa watu wake waitwao Wayahudi(waisrael)
So mungu wa wayahudi ni wivu wake ndio ulipelekea kuwaagiza watu wake wasiabudu mingine kama Allah n.k
 
hapo sawa, lakini je chombo kilichoumbwa na mfinyanzi kinaweza kumwambia mfinyanzi wake kwamba hapa umekosea kuniumba, ilitakiwa hivi, je kilikuwepo wakati kinaumbwa? Kinajua kanuni zipi na mahitaji yapi vilitumika kukiumba? Chukulia hiki kitu ndo cha kwanza kuumbwa na hakina reference nyingine yoyote na kisimwambie mfinyanzi kwa nini hujaniumba niwe sawa na wewe, kwa maana mfinyanzi ana malengo yake ambacho kenyewe hakijui ni nini na yalitoka wapi hayo malengo
Logical non sequitur fallacy.

Mimi nakwambia hiyo Mungu hayupo, na hivyo hajaumba.

Wewe unaniambia chombo kilichoumbwa na mfinyanzi.

Hujaelewa hoja yangu bado.

Rudi kasome post namba 27 hapo juu.
 
Kama ambavyo wewe unaniona ni mjinga wa kuamini Mungu hayupo kwakuwa kama kila kitu kinachotokea basi lazima kiwe na chanzo chake,na chanzo kitakuwa na chanzo chake

Nami nakuona wewe ni mjinga wa kutoamini kuwa lazima somewhere kutakuwa na source ya kila kitu,lazima kila kitu kina mwanzo wake,hiyo ipo hivyo,sasa utaamini au huamini it's not my problem
Umesema kila kilichopo ni lazima kiwe na chanzo, hakiwezi kuwepo tu bila ya kuwa na chanzo.

Mungu chanzo chake ni nini?

Mbona hujajibu swali hili?
 
Robert Heriel Mtibeli na min -me .
Naona Hamuamini uwepo wa Mungu. Lakin naona kwenye comments na post zenu mbali mbali mnasisitiza Hekima, uungwana na namna bora ya Kuishi kama Binadamu.

Hii namna bora mnayofikiria inatoka ndan ya nafsi zenu, na ndio mnahisi ni sahihi sisi binadamu tuishi kwa namna hiyo. (Regardless na Dini).

Na kama bas mngepewa kudra kuelekeza watu waishi bas bila shaka mngewaongoza waishi namna hiyo. Si ndio?.

Sasa mjue tu kuwa na yenyewe ingeitwa Dini.

Hii ni Bila hata kusema mnamuamini Mungu mmoja. Au Miungu weng au mizimu au hamumini kabisa.

Kwasababu Dini ni taratibu, tamaduni na Miongozo jinsi ya Kuishi maisha yako Duniani.

Mm naamin Mungu yuko, ila namna ambayo anaelekeza watu wake waishi ndio iko tofauti.

NB;: hata wale wanaoamini Miungu Mingi. Mfano Hindus .Pia wanaamin kuwa hiyo Miungu (chiva) anapata nguvu zake kutoka sehem moja. (Centre ya supreme power).

Haya Ni mawazo Yangu.
Humanism inasisitiza kuishi kwa maadili lakini si dini, ni falsafa.

Usilazimishe mambo.
 
Umesema kila kilichopo ni lazima kiwe na chanzo, hakiwezi kuwepo tu bila ya kuwa na chanzo.

Mungu chanzo chake ni nini?

Mbona hujajibu swali hili?

Kuna kitu lazima kiwe cha kwanza na ndio kianzishe kingne.

yeye Hana Mwanzo wala mwisho. Na ndio mwanzilishi wa vingne ambavyo ndio vina mwanzo.
 
Kuna kitu lazima kiwe cha kwanza na ndio kianzishe kingne.

yeye Hana Mwanzo wala mwisho. Na ndio mwanzilishi wa vingne ambavyo ndio vina mwanzo.
Ukishasoma kila kitu lazima kiwe na kingine kilichokianzisha, unajipa kazi ya kueleza Mungu kaanzia wapi.

Ukisema Mungu hana mwanzo, yeye ni social, hapo umefanya special pleading logical fallacy na kuvunja kanuni yako kwamba kila kilichopo kina mwanzo.

Soma post yangu namba 27 nimeelezea kirefu.
 
Umesema kila kilichopo ni lazima kiwe na chanzo, hakiwezi kuwepo tu bila ya kuwa na chanzo.

Mungu chanzo chake ni nini?

Mbona hujajibu swali hili?

Hapa kuna hoja kuu nne zinazotumika kutetea chanzo cha Mungu:

1. Hoja ya Kosmolojia (Kalam Cosmological Argument)
Hoja hii inajikita katika kanuni ya sababu na athari. Inasema kuwa kila kitu kilichokuwa na mwanzo lazima kiwe na sababu iliyokisababisha.
Ulimwengu una mwanzo: Sayansi ya kisasa (kama nadharia ya Big Bang) na sheria za thermodynamics zinathibitisha kuwa ulimwengu haukuwepo milele; una mwanzo.
Sababu ya kwanza: Ikiwa ulimwengu una mwanzo, basi kuna kitu "nje" ya ulimwengu (nje ya muda, nafasi, na mata) kilichousababisha. "Kitu" hicho ndicho kinachoitwa Chanzo cha Kwanza au Mungu.

2. Hoja ya Ubunifu na Mpangilio (Teleological Argument)
Hoja hii inaangalia utata na uratibu uliopo ulimwenguni. Ulimwengu hauonekani kuwa wa bahati mbaya, bali unaonyesha mpangilio uliokusudiwa.
Marekebisho Maalum (Fine-Tuning): Sheria za fizikia (kama nguvu ya mvuto au kasi ya kutanuka kwa ulimwengu) zimekaa katika uwiano sahihi sana kiasi kwamba kama zingebadilika kidogo tu, uhai usingewezekana.
Mfano: Kama vile saa inavyoonyesha uwepo wa fundi saa, ulimwengu changamani unaonyesha uwepo wa Mbunifu Mkuu.

3. Hoja ya Maadili (Moral Argument)
Hoja hii inahusu uwepo wa maadili ya kweli na ya kudumu (objective moral values).
Binadamu wote wana hisia ya ndani kuhusu "zuri" na "baya" (kama vile kukubali kuwa kudhulumu wasio na hatia ni kosa).
Ikiwa hakuna Mungu au chanzo cha juu cha mamlaka, basi maadili yanakuwa ni maoni tu ya watu au matokeo ya mageuzi ya kijamii. Uwepo wa sheria za kimaadili zinazofanya kazi kote duniani unaashiria uwepo wa "Mtoa Sheria" mkuu.

4. Hoja ya Ontolojia (Ontological Argument)
Hii ni hoja ya kimantiki zaidi inayotokana na dhana ya ukamilifu.

Inasema kuwa Mungu anatafsiriwa kama "Kiumbe mkuu ambaye hakuna mwingine mkuu zaidi yake anayeweza kufikirika."
Kuwepo katika uhalisia ni "kuu" zaidi kuliko kuwepo katika fikra tu. Kwa hiyo, ikiwa tunaweza kufikiria kiumbe mkuu kuliko wote, lazima kiumbe huyo awepo katika uhalisia, vinginevyo hatakuwa "mkuu kuliko wote."
 
Hizi hoja zote ulizoweka hapa zilijaribu ku-assume tu uwepo wa Mungu.

Hazithibitishi uwepo wa huyo Mungu.
 
Back
Top Bottom