Ufafanuzi wa Kujadiliana na watu wasioamini uwepo wa Mungu

Ufafanuzi wa Kujadiliana na watu wasioamini uwepo wa Mungu

Watu pekee wanaoweza kufanunua uwepo wa Mungu bila jazba ni Wakristo hutumia Pschology & Theology pana kukuelewesha hadi ukaingia kwenye mfumo kumuamini Mungu wao Yahweh.. vinginevyo kutana na wale kutoka Tandale kwa Tumbo waumini wa Masjid Khomenei, ukibishia kuhusu mungu wao aitwae Allah uwe na mbio kama Ussain Bolt vinginevyo watakumwaga utumbo na kukutenganisha viungo wapate thawabu kwa mungu wao Allah
I naelekea unapenda sana porojo,lete hoja tujadili na sio bla blah blah
 
Ukishakuwa na mjadala kujadili uwepo wa Mungu tu, hususan Mungu muweza yote, mwenye ujuzi wote na upendo wote, mjadala huo tu nao ni ushahidi kuwa Mungu huyo hayupo.

Kwa sababu, kwa sifa zake hizo, Mungu huyo angekuwapo, angejulikana na viumbe wote, popote, muda wowote, bila utata, kwa namna ambayo haihitaji mjadala na mjadala hauwezekani.

Hivyo, mjadala huo, kwenye ulimwengu ambao Mungu yupo, usingewezekana kuwepo.

Hili ni jambo rahisi tu kuelewa.

Lakini unaweza usielewe.

Na usipoelewa pia ni ushahidi kuwa huyo Mungu hayupo.

Kwa sababu huyo Mungu, kama yupo, atakuwa si mkatili hivyo akunyime uelewa ndogo tu huu.
Hili si jambo geni kulisikia kutoka kwenu,mara nyingi mnasema inakuwaje Mungu muweza wa yote,mwenye upendo aruhusu vita au mauaji na mambo kama hayo

Hii inaonyesha kwamba mnamuweka Mungu kwenye daraja la binadamu,kwakuwa wewe una huruma,haupendi machafuko au vita au ukatili basi nawe unamuweka Mungu kwenye viwango hivyo hivyo,hapa mnaonyesha udhaifu wenu wa utambuzi na kufikir, mna la kujifunza zaidi
 
Mleta hoja na wajibu hoja nadhani wote kuna haja kwenda kusaka references kwanza maana naona nyote humu it's pointless,,,, natamani kuwajibu lakini ngoja niwaandalie uzi wenye kila utamu
 
Hakuna binadamu wa mwanzo.

Kama kungekuwa na binadamu mmoja tu wa mwanzo kwa binadamu wote ulimwenguni, basi kusingekuwa na utofauti wa rangi na vinasaba kwa binadamu.

Binadamu wote tungefanana kwa rangi na vinasaba, kwa sababu tumetokana na Binadamu mmoja tu.

Lakini sivyo, binadamu tunafoutiana rangi na vinasaba.

Kuna waafrika weusi, wazungu weupe, wachina, wajapani, wafilipino, wakorea, wahindi weusi, wahindi weupe, waarabu n.k

Sasa kwa huu, utofauti wa rangi na vinasaba HAIWEZEKANI binadamu wote tuwe tumetokana na Binadamu mmoja tu wa mwanzo.

Kama binadamu wote, tungekuwa tumetokana na Binadamu mmoja tu wa mwanzo, tungefanana kwenye kila kitu.
Kama binadamu walitokea tu kama unavyosema from nowhere kwanini hawakuendelea kutokea kwa stahili hiyo mpaka leo, kipi kilifanya tuzaliane?
 
Mleta hoja na wajibu hoja nadhani wote kuna haja kwenda kusaka references kwanza maana naona nyote humu it's pointless,,,, natamani kuwajibu lakini ngoja niwaandalie uzi wenye kila utamu
Karibu utuelimishe ndugu yetu
 
Kama binadamu walitokea tu kama unavyosema from nowhere kwanini hawakuendelea kutokea kwa stahili hiyo mpaka leo, kipi kilifanya tuzaliane?
umewahi kubahatika kusoma vitabu vya Dini zingine ambazo sio IBrahimic religion?
umewahi kusoma BUdha au shinto?
au Summerian?
je unajua kuwa Uhindu ni dini ya zamani sana kuliko dini yoyote ya Ibrahimic religion?
 
Sijawahi kusoma,nitafurahi kama utaweka mchango wako hapa tujifunze,lengo ni kufahamishana na kuelimishana
 
Sijawahi kusoma,nitafurahi kama utaweka mchango wako hapa tujifunze,lengo ni kufahamishana na kuelimishana
Ni kwamba its Coincidental tumezaliwa kwenye dini au madhebu tuliyopo sio by choice ni only by chance iliyotuchagua kuwa huko pemgine leo hii ungezaliwa china ungekuwa tayri kufa kutetea shinto na kuona ibrahimic religion ni uongo au kutetea Budha and etc..
lengo langu ni nini na kwanini nasema hivyo..
umezungumzia story ya uumbaji lakini hujafanya research kugundua kuwa story ya uumbaji uliyonayo ambayo unaiamini inafnaya kazi only in ibrahimic religions ila ukiama dini tu wana hadithi zao za uumbaji na hawana kiumbe anaitwa Adam wala hawa na wamekuwa wakiamini hivyo kwa miaka zaidi ya 3000 kabla ya kuzaliwa kristo na kabla ya dini ya kiyahud..

sijaiweka coincidental bahati mbaya just imagine ertugrul ungezaliwa roma italy au ungezaliwa vatican leo hii ungekuwa unaupinga uislam na hivyo hivyo kama ungezaliwa Kwa wayahudi ungekuwa unaupinga uislam na ukristo kwa nguvu zako zote..

sasa Hiyo tafsiri ya UUngu au Mungu bado imetofautiana kwenye kla dini kuna wengine wana Mungu mmoja kuna wngine wana mungu watatu na kuna wengine wanakataa mungu huyu sio wao etc..

so dhana ya Mungu its school of thought + coincidental na ni very contradictory facts na according to arristaote law of contradiction iliyopo kwenye kitabu chake cha metaphysics...Ina cancel tukio zima la uwepo mpaka tuchunguze vizuri....

so Tuanze mada mimi na wewe kama hutojali ertugrul unaweza kuthibitisha uwepo??
dizani ya kujibu hoja na kuchangia tutajifunza mengi
 
Kama binadamu walitokea tu kama unavyosema from nowhere
Binadamu hawatokei, Binadamu wanazaliwa.

Hakuna sehemu nilikwambia Binadamu wanatokea.

Binadamu wanazaliwa kwa kuzaliana wao kwa wao.
kwanini hawakuendelea kutokea kwa stahili hiyo mpaka leo, kipi kilifanya tuzaliane?
Kujamiiana(sex) ndio kunafanya tuzaliane.

Hata wewe ulizaliwa kwa sababu Baba na Mama yako wali sex.
 
Binadamu hawatokei, Binadamu wanazaliwa.

Hakuna sehemu nilikwambia Binadamu wanatokea.

Binadamu wanazaliwa kwa kuzaliana wao kwa wao.

Kujamiiana(sex) ndio kunafanya tuzaliane.

Hata wewe ulizaliwa kwa sababu Baba na Mama yako wali sex.
Mbona kama unaleta janja janja,ok tufanye kwamba hujasema binadamu wanatokea, kuzaliana kulikuja baadae baada ya kuwepo asili ya mwanadamu na ndio wakaanza kuzaliana

Hoja hapa je huyo binadamu wa kwanza asili yake ni nini? Kama katokea kutokana na mabadiliko ya kemikali au kwa mabadiliko mengine yoyote,je kwanini mabadiliko hayo hayakuendelea hadi leo?
 
Mbona kama unaleta janja janja,ok tufanye kwamba hujasema binadamu wanatokea, kuzaliana kulikuja baadae baada ya kuwepo asili ya mwanadamu na ndio wakaanza kuzaliana
Kwa nini unafikiri kuzaliana kulikuja?

Kwa nini hufikirii kuzaliana kumekuwepo milele?

Je ni lazima kwamba kuzaliana kuwe kulikuja?

Je kuzaliana hakuwezi kuwepo bila kuja?
Hoja hapa je huyo binadamu wa kwanza asili yake ni nini?
Asili ya Binadamu ni binadamu mwenyewe.

Binadamu wanazaliana wenyewe kwa wenyewe na ndio asili ilivyo.

Unataka asili gani nyingine?

Nilishakwambia hakuna binadamu wa kwanza duniani kwa binadamu wote.

Na hili linathibitika kwa kuwepo binadamu tunao tofautiana rangi na vinasaba.

Kuna waafrika weusi, wazungu weupe, wachina, waarabu, wafilipino, wakorea, wahindi weusi na weupe n.k

Sasa kwa huu utofauti, Haiwezekani binadamu wote tuwe tumetokana na Binadamu mmoja tu wa mwanzo.

Kama ingekuwa binadamu wote ulimwenguni tulianzia kwa binadamu mmoja tu wa mwanzo, basi tungefanana kwenye kila kitu. Rangi na vinasaba.
 
Ni kwamba its Coincidental tumezaliwa kwenye dini au madhebu tuliyopo sio by choice ni only by chance iliyotuchagua kuwa huko pemgine leo hii ungezaliwa china ungekuwa tayri kufa kutetea shinto na kuona ibrahimic religion ni uongo au kutetea Budha and etc..
lengo langu ni nini na kwanini nasema hivyo..
umezungumzia story ya uumbaji lakini hujafanya research kugundua kuwa story ya uumbaji uliyonayo ambayo unaiamini inafnaya kazi only in ibrahimic religions ila ukiama dini tu wana hadithi zao za uumbaji na hawana kiumbe anaitwa Adam wala hawa na wamekuwa wakiamini hivyo kwa miaka zaidi ya 3000 kabla ya kuzaliwa kristo na kabla ya dini ya kiyahud..

sijaiweka coincidental bahati mbaya just imagine ertugrul ungezaliwa roma italy au ungezaliwa vatican leo hii ungekuwa unaupinga uislam na hivyo hivyo kama ungezaliwa Kwa wayahudi ungekuwa unaupinga uislam na ukristo kwa nguvu zako zote..

sasa Hiyo tafsiri ya UUngu au Mungu bado imetofautiana kwenye kla dini kuna wengine wana Mungu mmoja kuna wngine wana mungu watatu na kuna wengine wanakataa mungu huyu sio wao etc..

so dhana ya Mungu its school of thought + coincidental na ni very contradictory facts na according to arristaote law of contradiction iliyopo kwenye kitabu chake cha metaphysics...Ina cancel tukio zima la uwepo mpaka tuchunguze vizuri....

so Tuanze mada mimi na wewe kama hutojali ertugrul unaweza kuthibitisha uwepo??
dizani ya kujibu hoja na kuchangia tutajifunza mengi
Kwanza nakubaliana na maelezo yako kwamba ni kweli kabisa wengi wetu tumejikuta kwenye imani hizi kutokana na kujikuta humo kwa mpango ambao tumeukuta,ni wachache sana ndio wamebadilika baada ya kusoma na kuchambua na kuridhishwa na hoja na taarifa za dini hizo

Kwa upande wa pili, umeuliza je naweza kudhibitisha uwepo? Hapa unakusudia uwepo wa nini?

Tatu,naam nitapenda mada iendelee nikitaraji kujifunza kutoka upande wako kwa maana kuna dini nje ya Abrahamic ambazo binafsi sijazisoma kabisa.
 
Kwa nini unafikiri kuzaliana kulikuja?

Kwa nini hufikirii kuzaliana kumekuwepo milele?

Je ni lazima kwamba kuzaliana kuwe kulikuja?

Je kuzaliana hakuwezi kuwepo bila kuja?

Asili ya Binadamu ni binadamu mwenyewe.

Binadamu wanazaliana wenyewe kwa wenyewe na ndio asili ilivyo.

Unataka asili gani nyingine?

Nilishakwambia hakuna binadamu wa kwanza duniani kwa binadamu wote.

Na hili linathibitika kwa kuwepo binadamu tunao tofautiana rangi na vinasaba.

Kuna waafrika weusi, wazungu weupe, wachina, waarabu, wafilipino, wakorea, wahindi weusi na weupe n.j

Sasa kwa huu utofauti, Haiwezekani binadamu wote tuwe tumetokana na Binadamu mmoja tu wa mwanzo.

Kama ingekuwa binadamu wote ulimwenguni tulianzia kwa binadamu mmoja tu wa mwanzo, basi tungefanana kwenye kila kitu. Rangi na vinasaba.
Ni kujidanganya kusema binadamu wamezaliana milele,lazima kuna mbegu ambayo ilikuwepo hapo awal

Sikupenda kabisa kugusia upande wa maandiko kwakuwa nyie hamuamini maandiko,lakini itoshe kusema kuna mambo sayansi haiwezi kuelezea,ndio maana unapata tabu kujua kwanini kuna wahindi,wazungu,waafrika au Any color

Hapa dini ina majibu yake,kwamba tumeumbwa kwa mataifa ili tufahamieni tu lakini katika wote hao mbora wao ni mchamungu tu

Kwahiyo kwa sayansi kushindwa kuthibitisha kwanini kuna waupe weusi au brown haimaniishi kwamba asili yetu sio moja
 
Hapa kuna hoja kuu nne zinazotumika kutetea chanzo cha Mungu:

1. Hoja ya Kosmolojia (Kalam Cosmological Argument)
Hoja hii inajikita katika kanuni ya sababu na athari. Inasema kuwa kila kitu kilichokuwa na mwanzo lazima kiwe na sababu iliyokisababisha.
Ulimwengu una mwanzo: Sayansi ya kisasa (kama nadharia ya Big Bang) na sheria za thermodynamics zinathibitisha kuwa ulimwengu haukuwepo milele; una mwanzo.
Sababu ya kwanza: Ikiwa ulimwengu una mwanzo, basi kuna kitu "nje" ya ulimwengu (nje ya muda, nafasi, na mata) kilichousababisha. "Kitu" hicho ndicho kinachoitwa Chanzo cha Kwanza au Mungu.

2. Hoja ya Ubunifu na Mpangilio (Teleological Argument)
Hoja hii inaangalia utata na uratibu uliopo ulimwenguni. Ulimwengu hauonekani kuwa wa bahati mbaya, bali unaonyesha mpangilio uliokusudiwa.
Marekebisho Maalum (Fine-Tuning): Sheria za fizikia (kama nguvu ya mvuto au kasi ya kutanuka kwa ulimwengu) zimekaa katika uwiano sahihi sana kiasi kwamba kama zingebadilika kidogo tu, uhai usingewezekana.
Mfano: Kama vile saa inavyoonyesha uwepo wa fundi saa, ulimwengu changamani unaonyesha uwepo wa Mbunifu Mkuu.

3. Hoja ya Maadili (Moral Argument)
Hoja hii inahusu uwepo wa maadili ya kweli na ya kudumu (objective moral values).
Binadamu wote wana hisia ya ndani kuhusu "zuri" na "baya" (kama vile kukubali kuwa kudhulumu wasio na hatia ni kosa).
Ikiwa hakuna Mungu au chanzo cha juu cha mamlaka, basi maadili yanakuwa ni maoni tu ya watu au matokeo ya mageuzi ya kijamii. Uwepo wa sheria za kimaadili zinazofanya kazi kote duniani unaashiria uwepo wa "Mtoa Sheria" mkuu.

4. Hoja ya Ontolojia (Ontological Argument)
Hii ni hoja ya kimantiki zaidi inayotokana na dhana ya ukamilifu.

Inasema kuwa Mungu anatafsiriwa kama "Kiumbe mkuu ambaye hakuna mwingine mkuu zaidi yake anayeweza kufikirika."
Kuwepo katika uhalisia ni "kuu" zaidi kuliko kuwepo katika fikra tu. Kwa hiyo, ikiwa tunaweza kufikiria kiumbe mkuu kuliko wote, lazima kiumbe huyo awepo katika uhalisia, vinginevyo hatakuwa "mkuu kuliko wote."

1. Unasema ulimwengu una mwanzo.

Unajuaje ulimwengu una mwanzo?

Unawezaje kuthibitisha hilo?

Umeangalia hiyo video ya post # 27?

Umeielewa?

Unajua video inaongelea nini?

Hizo hoja unazielewa?
 
Hili si jambo geni kulisikia kutoka kwenu,mara nyingi mnasema inakuwaje Mungu muweza wa yote,mwenye upendo aruhusu vita au mauaji na mambo kama hayo

Hii inaonyesha kwamba mnamuweka Mungu kwenye daraja la binadamu,kwakuwa wewe una huruma,haupendi machafuko au vita au ukatili basi nawe unamuweka Mungu kwenye viwango hivyo hivyo,hapa mnaonyesha udhaifu wenu wa utambuzi na kufikir, mna la kujifunza zaidi
Hapana

Hujaelewa hoja na sifikiri kama unaweza kuelewa.

Mimi naonesha contradictions katika hoja za kuwepo Mungu.

Napinga uwepo wa Mungu, kwa kuonesha habari za uwepo Mungu zinavyojicontradict zenyewe.

Hapa unaambiwa Mungu ana upendo wote, ana uwezo wote, ana ujuzi wote, angeweza kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani.

Lakini hakuumba ulimwengu huo, kaumba huu ambao mabaya yanawezekana.

Kwa nini?

Hapo huoni contradiction katika habari za kuwapo huyo Mungu kabla ya kuweka lolote letu tunalotaka?
 
Nani ana mwamini Mungu yupi , ni sababu moja wapo ya uwepo wa Mungu kutiliwa shaka
Kuna kitu kimoja Theists wengi na Attheists pia wote hawakielewi, vizuri.

Tunapozungumzia Mungu, Vichwani mwao wengi ( kama wewe ) mnaweka misingi ya dini Kwanza. Wengi wanaweka picha kwamba Mungu lazima atakua kama kiumbe fulani Au Baba fulani ambae amekaa sehemu fulani. Lakini Mungu ni Zaidi sana ya hapo.

Sasa ipo hivi: wengi mjue hii ( ili Theist Imani yenu isiyumbe na Theist Muelewe hii concept ) Tunapozungumzia Mungu Tunamaanisha ile supernatural power, Nguvu iliyofanya kilakitu kiwepo, Nguvu iliyofanya Galaxy ziwepo na kuzifanya ziendelee kuwepo, nguvu iliyoweka Sheria za physics.

kama unaamini kwenye Bigbang, ni Nguvu iliyofanya bigbang itokee, Nguvu iliyopo nyuma ya Evolution ( au iliyoandika Code) ambazo zinafanya evolution iendelee kutokea yenyewe.

Theist Wote tunaanini kwenye Supernatural Power, Nguvu iliyojuu ya kilakitu kilichopo. Dini zimekuja baada ya miaka mingi miaka kwa miaka, Binadamu anapojaribu ku conect Na Nguvu hiyo, hivyo baada ya miaka mingi dini zimekua nyingi,

bila kuanga lia dini kwanini ni nyingi na wanautaratibu tofauti kwasababu tukiongelea hii ina historia yake ndefu sana ila wote wana kitu kimoja, Wanaamini kwenye Supreme Power

Ukisema, Hiyo Nguvu nayo imetokana na nini, na nhiyo imetokana na nini, hapo inaonyesha udogo wa akili ya binadamu, ikijaribu kulinganishwa na kuielewa nguvu hiyo, ni kama kujiuliza infinity ni ngapi au nyuma ya infinity kuna nini.

nimeona tafiti nyingi zinazoeleza jinsi dunia imeanza, jinsi parten zinaweza kuwa formed without a creator, kuleta mpangilio mzuri kama tunavyoona kwenye maua na parten mbalimbali za nature, jinsi au unpredictability inavyotolea kutokana na feedback loop Z = Z + Z² ambayo effect ndogo sana inaweza ikakuzwa mara nyingi san na kesho ikaleta utofauti mkubwa ambayo inaleta unpredictability mfano kwenye kutabiri hali ya hewa.
Lakini hizi zote zina kitu kimoja ( zinafata kanuni au Code ambyo tayari ilishaandaliwa kabla )

I believe In Super Natural Power, the power Beyond Everything, I believe in God, I believe in Catholic Church.
 
Back
Top Bottom