Ugonjwa wa Kuota Vinyama Sehemu za Siri (Bawasiri/ Hemorrhoids): Chanzo, Dalili, Tiba na Kinga

Pole mkuu, ni uoga wako tu kipi bora kuzidi kuumia au kwenda kufanyiwa operation, ?? Mimi nilikuwa na mdogo wangu naye alikuwa na tatizo hilo amefanyiwa operation huu ni mwaka wa 5, sasa hajawahi kulalamika tena, nenda kapate tiba usije leta matatizo mengine, sema balaa lake ni kukiuguza hicho kidonda, kwani sehemu kilipo ni changamoto kubwa sana.
 
anusol kama sikosei
tafuta hii dawa na uombe maelekezo

Kwa hali yake ilipofikia hii dawa haiwezi msaidia, soln ni kufanyiwa operation tu, kwani hii huwa inasaidia pale kinapokuwa ndani lakini kikishajitokeza tu haiwezi.
 
Kwa hali yake ilipofikia hii dawa haiwezi msaidia, soln ni kufanyiwa operation tu, kwani hii huwa inasaidia pale kinapokuwa ndani lakini kikishajitokeza tu haiwezi.

mkuu ikiwa kwa ndani unajuaje?
 
Mkuu,

Namna pekee ya kuutibu huo ugonjwa ni kuacha uoga na aibu na kupata tiba.

Mwaka juzi nilimpoteza shemeji yangu aliyekuwa na tatizo kama lako. Yeye alikuwa na aibu sana na ikambidi atumie dawa za mti shamba ikiwa pamoja na kukikata na kukitoa kabisa na mtaalam wa asili. Matokeo yake alipata kansa na mpaka anakuja shtuka ishakula sana kwa ndani. Ocean Road walijaribu kumtibu kwa mionzi lakini ilikuwa 'too late'.

Acha aibu. Tafuta tiba. Utaokoa maisha yako.

Tafakari.
 
Mimi ninaeandika hapa nimefanyiwa upasuaji wa hiyo kitu hapo aga khan hospital tangu 2008, sijawahi ona kinarudi mpaka leo niko safi kabisa. Na mie nilikuwa muoga kama wewe. Nilitakiwa kufanyiwa upasuaji tangu 1998 nikaingia mitini. Lakini mwisho wa siku JF hii hii ndio ilinifanya niende.
 

nashukuru sana mkuu kwa kunitia moyo! ubarikiwe sana.
 
kimekujajeeee kwanzaaa tujuee
 

vp ilichukua muda gan kupona? mana nipo chuo nisije nikachanganya mambo!
 

nashukuru kwa ushauri wako nitafanya hivyo.
 
Dawa rahisi na ya bure kabisa ya kupona kabisa hilo tatizo ni kumwamini Mungu na kukubali kuombewa katika Jina la Yesu na kuendelea kutenda kama Mungu anavyotaka, nenda kwa yeyote kati ya Mzee wa Upako-DSM, Nabii Joshua-Morogoro, TB Joshua-Nigeria, n.k kwa ajili ya maombezi utapona kabisa na usiache kutoa ushuhuda hapahapa kwenye jukwaa. Asikudanganye mtu madaktari wote duniani huwa wanatibu tu hakuna hata mmoja anayethubutu kusema amemponya mgonjwa, Mungu pekee ndiyo mponyaji.
 
mkuu ikiwa kwa ndani unajuaje?

Ni kuwa ukienda chooni unasikia maumivu makali sana, hadi uti wa mgongo unauma, kasheshe ni pale tu unapokuwa unajisaidia utadhani kuna mtu anakukata na viwembe!
 

Toa utahira wako hapa. Hata Mungu alituambia jisaidie nami nitakusaidia. Hivi wewe hujawahi kumeza dawa?
 
Ni kuwa ukienda chooni unasikia maumivu makali sana, hadi uti wa mgongo unauma, kasheshe ni pale tu unapokuwa unajisaidia utadhani kuna mtu anakukata na viwembe!

oh my GOD tunusuru na maradhi mazito kama haya,nawe ulishaumwa mkuu?pole sana ndugu yetu mtoa mada nenda hospitali kapate tiba huku nasi tukizidi kukuombea ndalibanza
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…