Nilikuwa nina tatizo la kukosa choo, na kupata choo kigumu chenye maumivu.
Tatizo hili likasababisha jeraha kwenye eneo la ndani ya njia ya haja kubwa. Nikawa nikienda kujisaidi napata choo kigumu pamoja na matone ya damu.
Baada ya jitihada ya kutatua tatizo la kukosa choo pamoja na kupata choo kigumu (constipation), nikafanikiwa kutatua tatizo hili.
Hivi sasa napata choo ipasavyo, kilaini najisaidia kwa starehe na sio kwa shida.
Ila tatizo linalonikabili hadi sasa ni lile jeraha, linasababisha kumwaga matone ya damu kila nikijisaidia. Na kila muda unavyoongezeka kiasi cha damu kinaongezeka.
Nikimaliza kujisaidia nanawa kabla matone ya damu hayajakata. Na hali hii inasababisha nikienda haja kubwa wakati ujao natoa damu iliyoganda pamoja na damu mpya. Jamani nifanyaje kwa aajili ya kutatua tatizo hili?
Uliwezaje kupata suluhu ya constipation mkuu,maana limekua kongwe kwangu msaada pm mkuu