Ndugu Mleta mada, Ujio wa Tundu Lissu ni furaha ya kila Mtanzania. kwani ni Mwana wetu na Mtanzania mwenzetu. Inasikitisha sana watanzania tunapo jidhadhalilisja na kumtukuza mtu mmoja, na katika ARENA ya kisiasa Tanzania na Africa, tuna tabia ya kumtukuza mtu.
Mfano Baada ya uhuru kupatikana , Tulimtukuza Mwalimu pekee, ili hali kuna wengi waliomtangulia kupigania uhuru na waliokuwa nae ambao hadi leo hawajulikani. Chadema ama Upinzani kuna wengi walikuwa na uwezo mkubwa wa kufanya mengi ya ukombozi au maendeleo, lakini hatuwaoni kwa sababu ya mila ya kujenga MIUNGU WATU " MAHALI UMCHUKUAPO MMOJA , UNAWAACHA WENGI WAZURI". Tushukuru ndugu Lissu Mola aliimpa uwezo wa Maisha yake kuendelea, Jee alipopigwa Marisasi ingekuwa siku yake, jee unamaanisha leo musingekuwa na wakumikombowa.
Vijana huu ni wakati wenu kuweni na busara za kuweza kuwa na misimamo ya kujitegemea badala ya kujenga MIUNGU WATU, Kama Vijana wa Chadema mnao vijana wazuri kama akina Mnyika, Esther, Sugu, Nyalandu,MSigwa na kadhalika, kwanini hawa wasifae kuwa vinara wa ukombozi wenu, au wasiwe watu mnaoweza kuamka Alfajiri kwenda kuwapigia kura.
Wacheni kujidhalilisha