Ujue uchaguzi wa Marekani (USA) na jinsi rais wake anavyochaguliwa

Sasa wewe ndio nimekuelewa. Nilikua gizani.
 
Baadala yake Rais wa Marekani na makamu wake wanaingizwa madarakani na wajumbe wapatao 538 kutoka kwenye majimbo 50 yanayounda nchi hiyo tajiri kiuchumi na yenye nguvu kubwa za kijeshi duniani
Unapotosha kijana, hii imewekwa ili kila jimbo liwe na sauti otherwise Rais angekua anaamuliwa na New York na California. Kumbuka zile ni majimbo huru yaliyoungana so lazima kila mmoja awe na umuhimu. Hata Kenya huwezi kuwa rais mpaka upate walau 25% ya kura walau kwenye nusu ya kaunti zote 47!!

Kajifunze kuhusu D'hondt method of proportion utaelewa kwanini huu mfumo unatumika
 
Hiyo ni uongoooo, buana. Mleta-mada amefafanua vizuri sana. Rejea kwenye maelezo yake.
 
Majimbo yote yanauwiano sawa/unaokaribiana wa hawa wajumbe
California = 54
Texas = 40
Florida = 30
New York = 28
Pennsylvania = 19
Alaska = 3
Delaware = 3
Vermont = 3
North Dakota = 3
South Dakota = 3

Je, hapo unaona kuna uwiano na ukaribiano wowote wa wajumbe?
 
Kwa hiyo mgombea anaweza kupata kura chache za wananchi akaja kupata kura nyingi za electoral college votes na kushinda urais
Misleading, lazima upate kura nyingi za wananchi ili ushinde hizo electoral college votes kwa jimbo moja moja ila tofauti ni kwamba majimbo hayalingani wingi wa watu so unaweza shinda majimbo mengi ila ukapoteza popular vote.

Kwahiyo hii imewekwa ili rais achaguliwe na majimbo mengi sio majimbo mawili yatoe rais, ingekua hivo republican wasingewahi shinda Urais milele
 
Kwa mfano, katika uchaguzi wa Tz, mshindi wa kiti cha urais ni lazima apate zaidi ya 50% ya kura zote halali,
Hii labda Kenya, kwa Tanzania ni first past the Post... yaani huo mfano wa ubunge ndio huo huo kwenye Urais. Nakumbuka warioba ndio alitaka Urais lazima upate 50% ila CCM walipinga.
 
Tanzania electoral vote
 

Attachments

  • images.jpg
    28.2 KB · Views: 4
Lakini Electoral College imeshatoa Marais watano walioshindwa Popular vote wa karibuni wakiwa George Bush na Trump.
Anachosema ni kwamba hao wajumbe hawachagui rais bali popular votes za majimbo ndio huamua rais. Yaani ili uchukue votes 19 za Philadelphia ni lazima ushinde popular vote ya Philadelphia and so on. Na ukishashinda zaidi ya 270 unatambulika kama rais huwa hawasubiri eti hao "wajumbe" ndio waje kupiga kura tofauti na za wananchi, in fact miaka yote wajumbe huwa wanapiga vile vile kama matokeo yaliyotangazwa.
 
California = 54
Texas = 40
Florida = 30
New York = 28
Pennsylvania = 19
Alaska = 3
Delaware = 3
Vermont = 3
North Dakota = 3
South Dakota = 3

Je, hapo unaona kuna uwiano na ukaribiano wowote wa wajumbe?
Sasa inavokuaga ni California inakuwa ni ngome ya Democrats alafu Texas na majimbo mengine ambayo yana cancel out wingi wa Kura za California

California inawatu millioni 39-40 na uchumi wake karibu trillion 3,

Texas na Florida niza wakaazi karibu 50Mil 30, kwa 20 na uchumi ni wao ni mdogo kuliko Californi, kwa Democracy tofatuti na Marekani, Vyama vingekuwa vinafocus majimbo yenye watu wengi na kuyaacha majimbo madogo, badala yake mfumo wa wamarekani unawafanya wagombea na vyama viangalie majimbo yote kwa usawa
 
Kila mtu macho na masikio kwenye uchaguzi wa kiranja mkuu wa dunia aka baba lao aka kiwanja- USA.
 
Wew ndo umefanya nielewe vizuri sasa, asante!
 
Umesahau ulichoandika mwenyewe, au?👇
Majimbo yote yanauwiano sawa/unaokaribiana wa hawa wajumbe
 
Unawajua Ronald Reagan na Richard Nixon?
 
Kwa hesabu zako, 1 ukizidisha na 50 unapata 538? Kama unazungumzia majimbo ya uchaguzi, yenyewe yako 435. Kama ndivyo, bado kimahesabu umepuyanga mno.

Rejea kwenye maelezo ya mleta-mada, namna 538 inavyopatikana.
Majimbo 50 hayo ya kiutawala
Majimbo ya uchaguzi yako 538
Majimbo ya uchaguzi yako ndani ya majimbo ya kiutawala

Acha hisia kijana SOMA KANUNI za uchaguzi wa Marekani na uache kukariri
Kwa hesabu zako, 1 ukizidisha na 50 unapata 538? Kama unazungumzia majimbo ya uchaguzi, yenyewe yako 435. Kama ndivyo, bado kimahesabu umepuyanga mno.

Rejea kwenye maelezo ya mleta-mada, namna 538 inavyopatikana.
 
Kura za wajumbe na kura za popular zinapigwa wakati mmoja japo matokeo ya kura za wajumbe hutoka mapema ndani ya masaa 24

Wajumbe wa Baraza la uchaguzi huchaguliwa
 

Nadhani labda angerahisisha kusema hivi
Ikiwa pamoja labda trump atashinda kwa wingi wa kura za wananchi
Lakini uamuzi wa kuingia ikulu utaamua ikiwa majimbo mangapi alishida kwa kumchagua trump katika hayo majimbo 538

Yaan labda tusema kwa mfano hapa DAR ES SALAAM kuna majimbo 7 UBUNGO ILALA TEMEKE KIGAMBONI KIBAMBA SEGEREA KINONDONI
ikiwa trump wananchi wa DSM wote wapo 100 na a wakamchagua na akashinda kwa kura tuseme 70 za wananchi
basi ili aingie ikulu itaangaliwa alishinda jimbo lipi na lipi katika kama UBUNGO kulikuwa na wapiga kula 12 katika wanaounda hawa wananchi100 wa dsm
Basi itaangaliw katika kula 12 za ubungo trump alipata ngapi inamaana kama alipata kula 7 katika 12 hii inamaanisha ameshinda katika jimbo la ubungo kwa mantiki hiyo tayari anakula 1 katika jimbo la UBUNGO ambapo ndo atatoka huyo mjumbe

Kwa mantiki hiyo wanaoamua nani awe raisi ni WANANCHI wenyewe wa marekani Kwa maana msingi wa kura za Electoral college ni wamarekani wenyewe ndo maana kuna state kadhaa ikionekana umeshinda moja kwa moja unaonekana kuwa tayari wewe ni raisi mtarajiwa bila hata kuhitaji hizo kura Electoral college kutokana na kuwa zina kura nyingi mfano kama STATE YA FROLIDA NEW YORK CALIFONIA WASHINGTON nk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…