Ujue uchaguzi wa Marekani (USA) na jinsi rais wake anavyochaguliwa

Vilaza ni wengi
 
Wanaoamua siyo WAMAREKANI Mkuu ni watu wachache sana wasiozidi hata asilimia kumi ya wapiga kura
 
Hao wajumbe 538 wanapatikanaje?
Wajumbe 538 wa Electoral College hupatikana kwa njia hii hapa.

1. Msingi wa Wajumbe: Kila jimbo la Marekani lina idadi ya wajumbe inayoendana na idadi yake ya wabunge katika Kongresi ya Marekani. Kila jimbo lina maseneta wawili (2), na idadi ya wabunge inategemea idadi ya watu katika jimbo hilo.

Kwa hivyo, kila jimbo lina wajumbe kadhaa wa Electoral College sawa na jumla ya maseneta na wabunge wake.

2. Jumla ya Wajumbe:
Kwa jumla, kuna wabunge 435 katika Baraza la Wawakilishi na maseneta 100, hivyo jumla inakuwa hivi,
- 435 (wabunge) + 100 (maseneta) = 535.
- Kisha, kuna wajumbe wawili kutoka eneo la Washington, D.C., hivyo kuleta idadi kamili ya wajumbe kuwa 538.

3. Kuwakilisha Majimbo: Wajumbe hawa wanaweza kutofautiana kutoka jimbo moja hadi jingine. Kwa mfano, jimbo kubwa kama California lina wajumbe wengi zaidi kwa sababu ya idadi yake kubwa ya watu, wakati majimbo madogo kama Vermont yana wajumbe wachache.

Ova
 
District of Columbia ina wajumbe watatu [3], siyo wawili.

535+3=538.



Maelezo mazuri.

Inafurahisha kuona walau wapo watu humu ambao kidogo wana uelewa wa mfumo wa uchaguzi mkuu wa urais ulivyo nchini Marekani.

Maana kuna watu wengine humu hawajui, na mbaya zaidi, hawajui kama hawajui.

Ukiwaeleza kuwa wanavyoelewa ni makosa, wanashupaza shingo na kuleta ubishi.

Hawajui tofauti ya national popular votes na state popular votes.

Hawajui ni votes zipi ndizo zinazoamua mgombea apate EV za jimbo.

Ukiwaeleza kwamba demokrasia ya Marekani siyo ‘direct democracy’, bali ni ‘representative democracy’, ndo unazidi kuwachanganya.

Ukienda ndani zaidi na kuwaeleza kwamba, Marekani siyo demokrasia [America is not a democracy] bali ni constitutional federal republic, ndo unawapoteza kabisa na watakubatiza majina yote!

Nyongeza: electoral college votes za jimbo huongezeka na/au hupungua kuendana na idadi ya watu/ wakazi waliopo jimboni.

Mfano, jimbo la California, Abraham Lincoln alipata kura 4 mwaka 1860. Kwenye uchaguzi wa 1864 akapata kura 5.

Mwaka 1980, Ronald Reagan alipata kura 45. Mwaka 1984 akapata kura 47.

Mwaka 2000 Al Gore alipata kura 54.

Hillary Clinton 2016 na Joe Biden 2020, walipata kura 55.

2024, California ina electoral votes 54.

Hapo utaona zimepungua. Hiyo ni kutokana na jimbo kupungukiwa wakazi na hivyo kupoteza kiti kimoja cha bunge la wawakilishi.

Kuongezeka au kupungua kwake, kunafuatia matokeo ya sensa.

Sensa ya mwisho Marekani ilikuwa 2020. Matokeo ya sensa hiyo yalitolewa 2021.

Ndo maana Joe Biden 2020 alipata EV 55. Lakini mwaka huu 2024, zimepungua na kuwa 54.
 
Kila laheri Kamala Harris...
 
Maelezo sio toshelezi.
 
Na wajumbe hawa wa Electoral College mara nyingi hupiga kura kwa kuangalia Wananchi wao kwenye majimbo yao (Popular Votes) wamempa nani.
Mf. Kama Wananchi wa California kwenye Popular Votes ameshinda Kamala Harris basi wajumbe wote wa Electoral College kutoka California watampigia Kamala Harris.
Ni mara chache sana wajumbe wa Electoral College waliwahi kupiga kura kinyume na Popular Votes za majimbo yao.
 
Lakini Electoral College imeshatoa Marais watano walioshindwa Popular vote wa karibuni wakiwa George Bush na Trump.
Unarudi pale pale, wajumbe wa electoral college ambao mgombea hupewa wanazaliwa kutoka kwenye kura za popular vote za kila jimbo. Huwezi kushinda electoral college kama hukushinda popular votes za majimbo mengi au muhimu zaidi. Hata marais uliowataja walishinda popular votes katika majimbo mengi au muhimu.

Tatizo wengi mnatafsiri popular votes kiujumla jumla badala ya kuitafsiri popular votes kwa kila jimbo. Na inapaswa kuitafsiri kijimbo zaidi maana huo msingi ndio huzaa electoral college votes.
 
Mkuu ili somo wengi wanajifanya wanalijua, lakini nimegundua hawalielewi. Ni jukumu letu kuwaelewesha. Wakishindwa kuelewa, basi!
 
Hakuna jimbo muhimu zaidi, hizo electoral votes 2 za maseneta wawili kila jimbo zinawabeba Republicans katika majimbo yao yenye watu wachache na swing states.
 
Maelezo mazuri, ila hili la kura za urais Tz mshindi lazima apate 50%+, limeanza lini?
Hilo la mshindi wa urais wa Tz kuhitaji kushinda kwa 50%+ lipo siku zote kwenye katiba ya Tz tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi. Sio jambo jipya, wengi hatulijui kwa kuwa scenario zake hazijatokea.
 
Hilo la mshindi wa urais wa Tz kuhitaji kushinda kwa 50%+ lipo siku zote kwenye katiba ya Tz tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi. Sio jambo jipya, wengi hatulijui kwa kuwa scenario zake hazijatokea.
Kifungu gani cha katiba??
 
Hakuna jimbo muhimu zaidi, hizo electoral votes 2 za maseneta wawili kila jimbo zinawabeba Republicans katika majimbo yao yenye watu wachache na swing states.
Hapana.
Kila jimbo lina electoral college votes zake binafsi, hayako sawa sawa yote. Hata kimahesabu tu, majimbo yako yako 50, inakuwaje jumla ya electoral college vote iwe 538 badala ya 100 kwa hesabu zako za kila jimbo kuwa na electoral college votes mbili.

Yapo majimbo 'muhimu zaidi' huko USA. Kisiasa jimbo 'muhimu zaidi' linaweza kutafsirika ni jimbo lenye wapiga kura wengi zaidi na hivyo automatically litakuwa na wajumbe wengi zaidi wa Electoral college votes.
Kwa mfano.
Calfornia (54)
Texas (40)
Florida (30)
Alaska (3)
Delaware (3)
North Dakota (3)
South Dakota (3)

Kwa hivyo, kwa mfano mgombea anaweza kushinda jimbo la Calfornia pekee na akapata electoral college votes 54 na mpinzani wake akashinda majimbo manne (Alaska, Delaware, North Dakota na South Dakota) akaambulia electoral college votes 12 tu. Na kama uchaguzi huo ungekuwa wenye kuhusisha majimbo hayo matano tu, maana yake mshindi wa Jimbo la Calfornia atakuwa ni rais wa Marekani.
 
Kila jimbo linapata idadi ya electoral votes zake kulingana na idadi ya viti vya ubunge na maseneta, viti vya ubunge vinatokana na idadi ya raia wakati kila jimbo lina idadi sawa ya maseneta wawili, Yani California yenye watu milioni 40 ina idadi sawa ya maseneta na Wyoming yenye watu laki 5.
 
Mkuu nielimishe kidogo hizo kura za electoral college zina kazi gani wakati tayari rais kishajulikana?
 
naomba jawabu kati ya donard trump na hilal Clinton nani alipata kura nyingi kimajimbo usemavyo na akatangazwa RAIS wa marekani?
Donald Trump alishinda zaidi kwenye popular votes za jimbo kwa jimbo kuliko Hilal Clinton, kwa msingi wa majimbo mengi zaidi au majimbo yenye wapiga kura wengi zaidi.

Lakini kama utajumlisha kura za jumla za wamerekani wote (kitu ambacho hakitumiki USA, na sayansi ngumu (complex) ya kuamua mshindi wa uchaguzi wa kidemokrasia hukipinga pia) Hilal Clinton alikupata kura nyingi zaidi ya Trump.

Kuelewa hili, waza mchezo wa Soka.
Simba alicheza mechi tano
Simba vs Yanga (0-0)
Simba vs Azam (0-0)
Simba vs Kagera (8-0)
JUMLA ni points 5 na magoli 8

Yanga.
Yanga vs Simba (0-0)
Yanga vs Azam (1-0)
Yanga vs Kagera (1-0)
Jumla ni points 7 na magoli 2.

Sasa kwako kati ya Simba na Yanga nani atangazwe ni bingwa wa ligi?
 
Nimesoma mada yote ila sijaelewa sehemu moja tu hapo kwenye comasava ndo nini sasa au ni lugha gani hiyo
 
Mkuu nielimishe kidogo hizo kura za electoral college zina kazi gani wakati tayari rais kishajulikana?
Umeuliza swali zuri mnoo.
Nitakujibu hapa hapa.
Msingi wa Electoral college votes ni ku screen, seal and backup mshindi wa kura za wananchi kupitia taasisi (chama) kilichomteua mgombea. Waliotengeneza mfumo wa kumpata rais wa USA wanaamini hakuna mfumo mmoja perfect wa kutoshea kufunika mapungufu yote ya kidemokrasia ikiwa yatatokea. Kwa hiyo mfumo wa popular votes unaweza kuwa 99% uko sahihi lakini kuhakikisha hiyo 1% inayopungua ni kwa vipi inaweza kuwa na msingi wa kuingaliwa kwa umakini na kulindwa isije ikaharibu.
 
Nijuavyo

Wabunge = 435(kutoka kwenye kila jimbo kulingana na idadi ya watu)
Maseneta = 100(wawili kutoka kwenye majimbo 50 bila kujali idadi ya watu)
Washington DC = 3(Sheria ya 23 ya mwaka 1961, inawapa Nafasi 3 za ma electors japo sio Jimbo)
Juma Wajumbe = 538.

Kila chama kabla ya uchaguzi kinachagua Wawakilishi(Electors)wake katika majimbo yao ya kiuchaguzi, baada ya hapo wanasubiri uchaguzi wa Popular votes.

Wananchi wakipiga kura kumchagua Raisi technically wanawachagua pia ma Electors wao kulingana na Chama.

Kwahio katika jimbo Mkiongoza kura za Raisi, basi na jimbo hilo mnabeba nafas zote za ma electors...

Yaani kwa mfano California, Democratic akishinda Popular votes,
Basi na wajumbe wake wote 54 wanakua wamepita kupitia kura za raisi.

Hivyo basi, inabidi uwashawishi wananchi wakupigie kura, ili ushinde jimbo flani, uchukue viti vyote vya ma Electors hatimaye ufikishe 270 ambapo unakua mshindi,

Hii haijalishi idadi ya kura za wananchi umezidiwa(hii inawezekana kwa kuchaguliwa na wananchi wengi kutoka majimbo machache mfano California, Texas, Florida, NY) mwenzako akachaguliwa na wananchi wachache katika majimbo mengi ambapo na jumla ya ma electors ikazidi ya wale wa majimbo ya watu wengi).

Kwa hio basi, hakikisha wananchi wengi wanakuchagua, LAKINI ZAIDI kutoka maeneo(majimbo) MENGI TOFAUTI,
Bila kusahau majimbo yenye wapiga kura wengi yana faida ya kupata Ma electors wengi kwa mkupuo.
Mfano ukishinda majimbo 12 yale yenye watu wachache, Mwenzako akishinda California tuu, amekupiga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…