Ukifanikiwa punguza kelele kula kimya kimya, Dogo mmoja wa Twitter huko X sasa hivi wamemfelisha

Raha ya pesa ni kumiliki vitu vizuri na vya thamani, sasa ukiwa na pesa huna vitu vizuri una tofauti gani na asiye nazo? Pesa zenyewe hazitaki kujificha! Unawezaje kuzificha?
Hata kwenye kumiliki vitu vizuri vya thamani nako, kuna tofauti kati ya anayetaka kumiliki vitu vizuri vya thamani kujiridhisha yeye mwenyewe na anayetaka kumiliki vitu vizuri vya thamani kuwaringishia walimwengu.

Huyo wa kwanza anaweza kuwa na hivyo vitu ndani kwake akaridhika, huyo wapili haridhiki mpaka a post Instagram mjue anavyo.
 
watu washalisema hili ila ngoja tuone japo anacheza kwa akili mno ili asigundulike
Ukimuangalia kwa karibu ni mtu ambaye intentions zake zipo wazi ila kilichofanya ni_mute account yake ni tabia yake ya udini. Yani ni mdini na hajifichi
 
Hilo nalo neno, picha za magari makali na nyumba kaliii kuwaringishia walimwengu.
 
Nchi hizi zetu ukiwa na mfanyabiashara na una utajiri wako,, ukitala kuwa salama wewe na mali zako. Chagua kufanya biashara au siasa, ukiona unataka vyote basi hakikisha siasa zako hazishindani na maslahi ya serikali.

Ukiona huwezi kuendana na serikali basi jifanye haupo kwenye siasa na hujihusishi na upande wowote.
 
Kwakua ni matapeli ili wapate wa kuwatapeli inabidi kujionyesha
 
Ni kweli hauwezi kupanda farasi wawili kwa wakati mmoja
 
shida ya pesa unaweza ukaamua kuwa mtu mkimya, lakini asset zako, circle yako, mwenendo wako wa mahusiano ya kimapenzi,
muonekano wako, gari unazosukuma, vikachangia ku make noise.

bila shaka mnakumbuka Kambi Zuberi Seif, mmiliki wa Cambiasso Sport Academy.

jamaa alikuwa ni mtu mkinya sana, very introvert guy, mtu wa dini sana, mtu wa swala tano, kwenye paji lake la uso ana alama ya sijida, na hakuwa mtu wa mitandao.

ungeambiwa kwamba huyu jamaa ni drug dealer mkubwa sana hapa nchini, ungebisha na kugalagala.

alipojitumbukiza tu kwenye mahusiano na yule dada wa mjini anaitwa sanchi, noise zikaanza, watu wakaamza kuchimba maisha yake, biashara zake nk.

mwisho wa siku siri zikaanza kutoka kwamba jamaa ni drug dealer na ni heavy weight kwelikweli kwenye biashara hiyo.

tangu alivyokamatwa 2022, mpaka sasa bado yupo ndani anasota though kuna vyanzo vinadai atatoka hivi soon.
 
Mbunye na makebo yalimponza
 
Hata hivyo magendo sio mpango tafuta riziki ya halali utaishi bila wasi wasi
 
Hata hivyo magendo sio mpango tafuta riziki ya halali utaishi bila wasi wasi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…