Ukifanikiwa punguza kelele kula kimya kimya, Dogo mmoja wa Twitter huko X sasa hivi wamemfelisha

Ukifanikiwa punguza kelele kula kimya kimya, Dogo mmoja wa Twitter huko X sasa hivi wamemfelisha

Mimi katika matajiri wote nawapenda waarabu , hao jamaa wana matatizo ila sio washamba ;mambo yao ni kimya kimya .

Katika kuwafahamu basi tajiri mstaarabu ni ''Bill gates'' , jamaa ana skendo nyingi ila yuko kimya . Huyu Musk naye ana ushamba wa kujifanya anajua kila kitu .
Wazanzibari waarabu hao jamaa temea mbali, ukipishana nae mtaani unaeza mpiga makofi ila pesa iliyopo pale weee ACHA TU, wana life la kawaida san
 
Km hujazaliwa kwenye pesa pekee ila ukizaliwa kwenye pesa pesa unaziona kitu cha kawaida tu maana umezikuta mpaka kwenye madustbin ya ndani kwenu sasa nini cha kushangaza hapo umezaliwa kabla hujakua kuna magari yako yamepaki uwani yanakusubiri ukue uendeshe na kila siku unayaona utababaika nini kujionyesha, wengi hua wanaishi private life ila kujiproud sometimes hua wanajiproud ila sio kwenye media ni ukiongea nao personal ndio watakwambia tuvituvitu na tena hapo umewatekenya sana

Hao unawaona wanaropoka ropoka mitandaoni ni baada ya kushika pesa ukubwani tena ambazo hawakutaraji km watazishika maisha yao yote na huku amezaliwa kutoka kwenye hali ya umasikini hawajakulia kwenye pesa hawajazaliwa wakazikuta pesa zimejaa ni masikini tu tena masikini wa kutupwa ambao pesa zao hazina mfumo wowote wa kuingia na kutoka muda wowote zinapotea maana hazina mwenyewe hazijakuwepo hapo kwa miaka na miaka ni pesa ambazo zimetokea tu bila chanzo maalumu cha kuaminika na ndio maana hawaoni hatari ya kuzifanyia show off maana wanajua muda wowote hizo pesa zinayeyuka na zitakua sio za kwao
Angalia msanii davido, alafu angalia na hawa walal hoi walio pata tuhela ukubwani, wanaa fujo sana
 
Nchi hizi zetu ukiwa na mfanyabiashara na una utajiri wako,, ukitala kuwa salama wewe na mali zako. Chagua kufanya biashara au siasa, ukiona unataka vyote basi hakikisha siasa zako hazishindani na maslahi ya serikali.

Ukiona huwezi kuendana na serikali basi jifanye haupo kwenye siasa na hujihusishi na upande wowote.
Usipo jihusisha na upande wowote ni ngumu kitajirika hapa bongo niamini, kiongozi akipenda mali Yako anasema yake KESI inaanza mpaka hapo usha dhurumiwa tayari
 
ila twende mbele turudi nyuma, hivi anajishugulisha na nini haswa au anafanya kazi gani? maana toka nafuatilia post zake huwa naona tu anajipost yeye na mali zake sijui kanunua gari flani mara appartment flani au yupo vacation ila kazi anayo fanya ni ipi inayompa hiyo mipesa
Nani huyu ?, nimeangalia post za tangu nyuma ila sijaelewa anaezungumziwa ni nani
 
Kuna jamaa pesa ilichanganyia, akawa ameingia mkataba na wachimbaji wadogo kwa kuwawezesha vifaa,ikatokea kutokuelewana ikabidi RC aende kusikiliza.Pale kwenye kikao jamaa akatamka "Siwezi kukubali huu ujinga hata kama nikiwekewa 🔪 shingoni" kikao kikavurugika wakaondoka, basi bwana kumbe wakawa wanamfatilia pasipo kujua siku moja kupata mzigo wa kutosha anaenda kuuza jirani wakamdaka kisha wakaenda na kwake kukagua kama vile mwizi.Toka hapo jamaa kuporomoka ila kama asingetoa yale matamshi kwa sasa angekuwa mbali mbaya mbovu.

Mapambio ni muhimu sana katika utafutaji hata kama masharti ni magumu vipi weee kubali ila utekelezaji uwe 0
 
Back
Top Bottom