Ukifanikiwa punguza kelele kula kimya kimya, Dogo mmoja wa Twitter huko X sasa hivi wamemfelisha

Wazanzibari waarabu hao jamaa temea mbali, ukipishana nae mtaani unaeza mpiga makofi ila pesa iliyopo pale weee ACHA TU, wana life la kawaida san
 
Angalia msanii davido, alafu angalia na hawa walal hoi walio pata tuhela ukubwani, wanaa fujo sana
 
Usipo jihusisha na upande wowote ni ngumu kitajirika hapa bongo niamini, kiongozi akipenda mali Yako anasema yake KESI inaanza mpaka hapo usha dhurumiwa tayari
 
Nani huyu ?, nimeangalia post za tangu nyuma ila sijaelewa anaezungumziwa ni nani
 
Kuna jamaa pesa ilichanganyia, akawa ameingia mkataba na wachimbaji wadogo kwa kuwawezesha vifaa,ikatokea kutokuelewana ikabidi RC aende kusikiliza.Pale kwenye kikao jamaa akatamka "Siwezi kukubali huu ujinga hata kama nikiwekewa 🔪 shingoni" kikao kikavurugika wakaondoka, basi bwana kumbe wakawa wanamfatilia pasipo kujua siku moja kupata mzigo wa kutosha anaenda kuuza jirani wakamdaka kisha wakaenda na kwake kukagua kama vile mwizi.Toka hapo jamaa kuporomoka ila kama asingetoa yale matamshi kwa sasa angekuwa mbali mbaya mbovu.

Mapambio ni muhimu sana katika utafutaji hata kama masharti ni magumu vipi weee kubali ila utekelezaji uwe 0
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…