JPM alikuwa populist, propaganda nyingi, lakini hamna lolote la maana
He was a populist somehow...
Na hakuwa populist tu, lakini pia;
✓ Alikuwa hapendi kukosolewa,
✓ Kwa KUWA alikuwa hapendi kukosolewa, na hii ilimleta kwenye tabia ya ukatili kwa wote waliokomsoa...
✓ Alikuwa mwenye maamuzi yasiyofanyiwa utafiti na yalipotekelezwa yalileta damage iliyo beyond control kwa nchi na wananchi. Mfano kumwaga damu za watu, kuteka na kupoteza watu nk nk...
✓ Na udhaifu mwingine tuujuao wote...
Huu ulikuwa upande wa udhaifu wake...
=========================
Lakini JPM kama binadamu alikuwa na upande wa mazuri yake (strengths side yake pia). Hili ni jema, zuri na linakubalika aidha...
✓ Alidhibiti mfumuko wa bei kwa kiwango cha juu sana kwa kuhakikisha bei za mafuta ya petrol zinakuwa constant kwa muda mrefu sana ili kutoathiri maisha ya wananchi...
✓. Wakati wake, shida za wananchi zilitatuliwa kwa haraka. Inasemwa alijenga nidhamu ya utumishi wa umma jambo ambalo ni zuri, jema na linakubalika...
✓ Hakupenda watu wanyanyaswe kwenye ofisi za umma..
✓ Wakati wake (miaka 6 ya Urais wake) kukatika katika umeme kulipungua kwa 95%. Hili lilikuwa jema sana, nampongeza kwa hili kokote aliko...
✓ Na mazuri mengine mengi ambayo mtu yeyote anaweza kuyakumbuka....
========================
VIPI KUHUSU HUYU MAMA SAMIA SULUHU..??
Ndugu hakuna kitu hapo..
✓ Huyu ni
Ceremonial President huku akijua kabisa, kuwa kwa mujibu wa Katika ya JMT, President ndiye Chief Exacutive na ndiye yeye...!!
Na hii ndiyo maana ndugu
JF Member, mleta mada hii anamng'akia huyu mama...
Na basically, huu ndio ukweli, kwamba, this lady is
zero presidential material. Ni takwa la kikatiba tu linamweka hapo huyu bibie, otherwise she doesn't deserve that position...!
Na hii ndiyo moja ya weakness kubwa ya katiba hii ya JMT - 1977 inayoruhusu watu wasio na uwezo kushika madaraka makubwa kama huyu mama kiasi cha kuwa msiba kwa nchi nzima....!!
✓ Si ajabu huyu mama hata hajui kwamba nchi anayoingoza iko gizani - haina umeme...!!!
Huku mwenzake (aliyekufa) akiwa amemwachia nchi yenye mwanga (umeme) na kukatikakatika umeme hovyo kulishakuwa ni msamiati adimu miongoni mwetu. Hili ni jema, zuri na linakubalika..
NOTE: Sijawahi kuwa shabiki ama mpenzi wa Mwendazake Magufuli na wala sikuwahi kumpa kura yangu iwe mwaka 2015 ama 2020...
Lakini alikuwa Rais wa nchi yetu. Na kuna mambo alifanya vizuri sana kama nilivyosema. Kwa hilo kwakweli nampa kongole, na Mungu amrehemu tu huko aliko...