Ukitaka kujua nguvu na ushawishi wa Urusi waangalie Wagner Group

Hao wanafanya kazi za urusi au zisizokinzana na urusi na si kinyume chake.
 
Ha!
Mbwiga yupo kata ya Nangulungu anajadili Wagner group huku maji ya ugali yanachomeka yote
 
Hao wanafanya kazi za urusi au zisizokinzana na urusi na si kinyume chake.
 
Hao wanafanya kazi za urusi au zisizokinzana na urusi na si kinyume chake.
 
Sawa
 
Ni Kama Tanzania tunavowanyia ukoloni watanganyika kwa kuwazimisha muungano na z'ber
 
Leo tena wagner wamemponda msaliti mwingine na sleight hammer linyundo likubwa kilo kumi limesaga kichwa cha defector.
 
Labda nikusaidie kitu,

Wagner Group limekuwa likijiendesha kijeshi ndani ya Urusi kwa miaka kadhaa kinyume cha sheria na katiba ya Urusi. Limekuwa likifanya recruitments za kijeshi na kutoa mafunzo ya kijeshi kwa kutumia zana za kivita ndani ya mipaka ya Urusi.

Katiba ya Urusi inasema wazi kwamba jukumu la ulinzi na usalama wa nchi ni jukumu la dola pekee kwa maana ya 'state' na siyo majeshi binafsi. Sheria za Urusi (criminal code) haziruhusu raia wa Urusi kujiunga na majeshi binafsi ya kukodi. Hizi sheria zipo mpaka sasa ninapoandika sentensi hii, hazijafanyiwa amendment.

Nilikuuliza swali hapo awali kwamba, nje ya Urusi hilo kundi limesajiliwa kwa sheria ipi? Na, ndani ya Urusi linajiendesha kijeshi kwa sheria ipi?

Jibu ulilotoa linaonesha wazi kabisa kuwa haufahamu hata majukumu ya jeshi jinsi yalivyo kwa ukamilifu wake. Unadhani kwamba kazi pekee ya jeshi ni kwenda kurusha mabomu na risasi vitani, nje ya nchi husika.
 
Unafahamu mkataba wa nato na urusi dhidi ya mipaka ya kujitanua kwa NATO kuelekea east?
Huo mkataba umekuwa ukitajwa sana humu jukwaani lakini mara kadhaa nimekuwa nikiomba uthibitisho wa kuwepo kwake. Mpaka sasa hakuna aliyeuleta humu.

Bado naendelea kusubiri!
 
Endelea kushangilia ukijua kuna nchi inakupenda sana kuliko wao. Iko hivi Marekani, German, Ufaransa na Uingereza wamejipatia mali nyingi sana kipindi cha ukoloni na kuwa nchi za uchumi mkubwa kwa kuiba mali za Afrika. China na Urusi hawakuwepo japo wanatengeneza silaha lkn uchumi wao upo chini kwahiyo wanakuja Afrika kwa kisingizio cha kulinda amani lakini ni wezi wakubwa.
Wanatembeza kichapo? Urusi, Mchina na Marekani ni wezi wakubwa. Wanaiba mali zetu
 
Ndugu yangu, tayari nimeona umechagua upande, itakuwa ni vigumu kuchambua hili kadhia ya Urusi kwa jirani yake Ukraine wakati umesha jipambanua upande wako, itakuwa sasa ni kupingana na sio kuchambua kwa hoja ok.

Ukraine ni nchi huru, USSR tayari ilisha sambaratika na haitorudi kamwe na hicho ndo kinacho muuma Putin, ungeniwekea hapa huo mkataba wa NATO na Urusi, I think ingekuwa poa sana.

Kutoa silaha, sijui mercenaries,etc, haimanishi Urusi imevamiwa ok, Ukraine ana haki ya kujilinda as a nchi huru na kuwa marafiki anaowataka ok.

Hawa big powers in the world wana tabia ya kuyumbisha mataifa madogo kwa kuwapandikizia viongozi vibaraka watao linda maslahi yao ok.

Russia walifanya hivyo Ukraine kwa kumweka Viktor Yanukovich kulinda maslahi yao pale Kyiv, but kwa bahati mbaya kambi ya Russia ikawa imezidiwa hoja na sera na kambi waliokuwa wakipendelea EU bloc.

Ikapelekea Viktor Yanukovich kukimbia nchi kwenda kwa baba yake Moscow, lakini raia wa Ukraine walikuwa sahihi kabisa waliona wakijiunga EU watanufaika na mengi sana kiuchumi, kijamii, n.k, badala Moscow hakupenda ndo chanzo cha kunyakua Cremea na haya unayo yaona yanaendelea na wewe unashabikia.
 

Sasa hapa umeeleza nini? Na wewe hapo unajiona kabisa haujachagua upande?? Uchambuzi wako umekufikisha kuona Russia anaionea wivu Ukraine 🤣🤣🤣🤣. Uchambuzi wa kijinga sidhani ata mtoto wa darasa la plli anayejielewa akafikilia hivyo.

Miaka ya 80s kulikuwa na mahasimu wawili, USA na USSR na wote hawa, walikuwa na wafuasi wengi nyuma yao kipindi cha vita baridi

Baada ya USSR kusambalatika, Russia bado ikabaki na nguvu kibwa kieneo na kijeshi. Kwasababu uadui kati ya USA na USSR ulikuwa ni Russia kwani ndio aliyekuwa kinara wa USSR haukwisha hivyo Russia na USA iliwabidi wasaini makubaliaono ya amani na kati ya makubaliano hayo ni kutokupanuka kwa NATO kuelekea mashariki na vilevile Russia na Ukraine walisaini makubaliano na moja ya makubaliano hayo ni Ukraine kutokujiunga na NATO

Sasa inavyoonekana marekani alisaini makubaliano hayo na Russia kiunafiki na kum andamaini mrusi. Akaanza kuipanua NATO kuelekea mashariki na Russia ililalamika sana kwa kuona makubaliano yao yanavunjwa na hakuna aliyejali. USA haikuishia hapo, akataka Ukraine nayo ijiunge na NATO na kuanzisha projects zake za kijeshi mdomoni mwa Russia

Russia akaona vitendo hivyo ni uchokozi wa makusudi na ni hatari kwa usalama wa taifa lake. Hayo tunayoyaona sasa hapo Ukraine ni mlolongo wa miaka mingi na hiyo vita ni kati ya Russia na USA. Ukraine ni uwanja tu wa mapambano
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…