Ukiwa Mtu Mzima Utagundua Kwamba Salamu Ya Shikamoo Ni Mtihani

Ukiwa Mtu Mzima Utagundua Kwamba Salamu Ya Shikamoo Ni Mtihani

Kituko ukubwani, unaenda kuchumbia mke unakuta mama yake umemzidi umri na baba yake mko sawa umri. Binti anaulizwa mbona anayetaka kukuoa ni mzee? Binti anajibu nimempenda hivyo hivyo na uzee wake. Mzee unapata mama mkwe anakuamkia shikamoo!
Hii kitaalamu sijui tunaitaje😂😂
 
Kuna wakati tulienda kuchumbia mahali, tukataja wasifu feki tena mbaya kwa binti ili tumjue kama kweli anataka kuolewa. Tukataja muoaji ana miaka sitini, hana kitanda analala chini na maisha yake ni ya kubangaiza. Binti hakuchomoa akasema huyo ndio mzuri tutaanza naye maisha mapya ya ndoa hata kama ni mzee wa kuamkiwa shikamoo
Huyo binti hata mimi ningempenda kwakweli,anajua maisha ni nini?
 
Dada yangu namzidi miaka 5 tukikutana Ananishikamoo kiheshima, dogo anayefuata namzidi 8yrs yeye ni wa mambo vipi.
Madada waliobaki napokea shikamoo.
Kimbembe kumpa shikamoo mama mdogo ninayemzidi umri miaka 15 hivi
Mimi mke mdogo wa baba namwambia assalaam alaikum,tupo sawa au nimemzidi
 
Kipind nimetoka toka tu chuo nimanza kazi, mkurugenz wangu ambaye ndio mwenye kampuni alikua amenizid umri wa miaka 10 na siku pekee aliopata shkamoo yangu ni siku naingia kwenye interview. Baada ya hapo mpaka naondoka kazin sikiwah mpa shkamoo.

Ukiachana tu na wewe kuona uzito kuamkia, hata watu wazima ukitazama kwa makini utakuja kugundua kuwa hawapendelei sana kuamkiwa na vijana kuanzia rika flani , labda awe mzee may be
Kwahiyo baada ya kupata kazi ukamuona boss fala flan hivi😂😂
 
Shikamoo sio salamu ni Utumwa
Dhima ya salamu ni kujuliana hali baina ya watu wawili
yenyewe haijajutosheleza ndio ikaongezewa Haujambo sijambo

Mimi siamkiagi hadi inapobidi na najaribu kuwaelimisha wa karibu yangu zaidi
 
Kule kwa wairaq na hasa kwa wafugaji wote wanajua Shikamoo ni salamu ya Mwalimu na mtu mtu mgeni. Hivyo ukiwa mwalimu utakuwa unapokea Shikamoo za wanafunzi wa wazazi wao. Pia ukiwa siyi mtu wa kabila lao utakuwa shikamoo kwa sana.
Kwahiyo uko ualimu ni dili😂😂
 
Kwahiyo uko ualimu ni dili😂😂
Ni watumishi pekee waliokuwa wakionekana maana jamii ya wafuagji inaishi vijijini. Hivyo, kwa enzi nyingi ilikuwa nadra sana kujua kama huwa kuna taaluma nyingine tofauti na Bwana Mifugo na Mwalimu. Ni sawa na ukiwa Musoma wanachojua ni vyeo vya Jeshini maana enzi hizo karibu kila kaya ilikuwa angalau mwanajeshi moja anayehudumu JWTZ.
 
Back
Top Bottom