Ukiwa Mtu Mzima Utagundua Kwamba Salamu Ya Shikamoo Ni Mtihani

Ukiwa Mtu Mzima Utagundua Kwamba Salamu Ya Shikamoo Ni Mtihani

Mie ukiniona niamkie cheichei aloo
Ukija zenji hata hujawahi kusoma kiarabu utajua tu Asalam Alaykm
Huku kumskia mkristo anasalimia Asalam alaykm, waalaykm Salaam ni kawaida tu
Au itaskia akiulizwa vipi hali yako anajibu Alhamdulillah, kusema Insha'Allah au MashaAllah kawaida tu halafu mara moja wana adopt
Sasa hiyo iko vyema maana haioneshi nani yuko chini nani yuko juu.
 
Si
79 si una miaka 45 tu? Mbona kama mvi zimekuja mapema sana?

Mimi principle yangu ninayotumia kama MTU huna uwezo was kunizaa, sikuamkii shikamoo, maana unaweza kuta watu umewazidi umri shikamaoo, (au wanafikiri umewazidi umri wakakushangaa)

Sie wa 71 tusio na mvi atatukosea heshima huyo dogo!!
Mwambie aamkie wakubwa, mvi sio kigezo Cha kula chumvi nyingi maana mjomba alifaki akiwa kagonga 66 bila mvi
 
Watoto wanatoa shikamoo kwa watu wazima, ila kwa watu wazima shikamoo ni salamu ya heshima. Watakupa kwa sababu umewazidi uchumi (kwa wasiokujua) au watakupa kwa sababu ya namna unavyo heshimika, unavyoheshimu watu, unavyozungumza na watu (kwa wanaokujua). Kuna watu wazima (hasa wanawake) wanaamkia vijana wadogo kwa sababu hizo mbili.
 
Na wa 1980 awe na miaka mingapi!? Hesabu imekuwa ngumu kiasi hicho!?

Ni mtihani kweli, unaweza kumsalimia mtu habari za saa hizi akakushushua kwa kukuona hustahili kumuamkia hivyo anataka shikamoo. Kuna wengine nao wanakuamkia shikamoo huku unawaona hawastahili kukupa shikamoo, ni wakubwa. Ishu nyingine inakuja kwenye kutongoza, unataka kutongoza demu mara anakusalimia shikamoo wakati we ulitaka akusalimie mambo vipi? Confidence ya kutongoza inashuka kwa kuona huyo demu ni mdogo sana kwako
Mzee kwani demu akikusaliamia shikamoo ndio huwezi kumtongoza? Mbona kigezo cha ajabu HK?
 
"Habari za asubuhi" , "Mmeamkaje" n.k ni salamu zenye maana sana na kumaanisha kuliko hizi za shikamoo... tatizo wabongo mtaani wajinga wajinga ukimuambia mtu mzima "Habari ya leo", anasema umemdharau...
Way back 2000 nilikuwa nasalimia Asalaam alaykum, vipi Khali??
Si nikashtakiwa kwa wazee na mshangazi mmoja kwamba Sina adabu nitampata wapi?
 
View attachment 3347358

Hiyo namba ndio mwaka wangu wa kuzaliwa,ulivyokuwa na hamu ya kujua Etugrul Bey ana miaka mingapi utapiga hesabu bila aibu ujue nina miaka mingapi,usijichoshe hii may nimetimiza miaka 46,je kuna mwenye shida na hilo?

Nakumbuka nikiwa Chuoni kuna mtu wa Library kipindi hicho alikuwa kwenye 40's akasema ukiwa na umri huu ni mtihani,unaweza usisalimie watu kwa kuwaona mnalingana au ukajikuta unawasalimia wadogo zako kwa umri

Aisee sasa namuelewa sana,kwanza namshukuru Allah nimejaaliwa mvi za kutosha tu,ishu ni kwamba huwa sometime nashindwa kuwaamkia watu nisio wajua kwakuwa naona kama nipo sawa nao tu,lakini sometime najishtukia naona kama nilipaswa kuwaamkia

Hii salamu ya Shikamoo sio poa kwasababu inamtaka mdogo amsalimie mkubwa,lau tungekuwa na salamu flani hivi ambayo haibagui mkubwa na mdogo ingekuwa poa sana, kwa mfano salamu ya "habari za asubuhi au mchana au jioni" haina mfumo wa mkubwa au mdogo

Najua watoto wa elfu mbili hamuelewi hili kama ambavyo nami sikumuelewa yule jamaa wa kule library kule Chuoni,sasa nimemuelewa,nanyi pia mtakuja kumuelewa Etugrul Bey siku moja when u turn 40's

Kama kuna mtu ambaye anamjua alieanzisha hii salamu aniambie,kwani namhitaji huyu mtu anipe maelezo ya kina ilikuwaje wameturithisha hii salamu.

Ni hayo tu!
Amekufa, labda kama unataka ulione kabuli lake.
 
Haaahaa 😆 ☺️ kuna siku Kuna ka brother kangu kana MWILI mdogo mdogo sikuwai kuonana nako tangia nikiwa mdogo.

Siku moja nikawa nimeenda kinyerezi nikamkuta kavaa jezi yake yupo na brother angu mmoja nikasalimia habari za leo kajamaa kakagoma kakasema nikape shikamoo tukalumbana nikakasalimia kwa shingo upande.

Baadae ndio brother mwingine AKAJA aka ni introduce kwake ni brother mkubwa na ana wadhifa kubwa tuu mpaka NIKAONA AIBU Ila Kuna watu Wana miili midogo midogo mpaka wanaweza kunyimwa kiti ugenini 🤓
Inakuwaje humjui kaka yako?
Au ndugu tu katika ukoo?
 
Hii salamu ya Shikamoo sio poa kwasababu inamtaka mdogo amsalimie mkubwa,lau tungekuwa na salamu flani hivi ambayo haibagui mkubwa na mdogo ingekuwa poa sana, kwa mfano salamu ya "habari za asubuhi au mchana au jioni" haina mfumo wa mkubwa au mdogo
Mkuu mbona unajizonga, "Asalaamu Alaykum" haya ni maamkizi bora kabisa yasiyozingatia umri.
 
Kituko ukubwani, unaenda kuchumbia mke unakuta mama yake umemzidi umri na baba yake mko sawa umri. Binti anaulizwa mbona anayetaka kukuoa ni mzee? Binti anajibu nimempenda hivyo hivyo na uzee wake. Mzee unapata mama mkwe anakuamkia shikamoo!
 
Kuna wakati tulienda kuchumbia mahali, tukataja wasifu feki tena mbaya kwa binti ili tumjue kama kweli anataka kuolewa. Tukataja muoaji ana miaka sitini, hana kitanda analala chini na maisha yake ni ya kubangaiza. Binti hakuchomoa akasema huyo ndio mzuri tutaanza naye maisha mapya ya ndoa hata kama ni mzee wa kuamkiwa shikamoo
 
Back
Top Bottom